Wanaharakati Helen Kijo-Bisimba na Ananilea Nkya wakamatwa na polisi

Status
Not open for further replies.
Hivi hawa wamama wana mabwana kweli?

Hili ni swali la unyanyapaa na halina uhusiano wowote na hii mada. Hv kuwa au kutokuwa na waume kunakusaidiaje mpendwa?

Ninajua kuna wanaume wanapenda kuoa wanawake wa namna hii kwani hivi vitu na maisha ya ndani ya ndoa haviingiliani na vinaweza kufanywa pamoja hata kama wameolewa na kama hawajaolewa ndo nzuri zaidi.
HOPEFUL UMEPATA JIBU
 
if this is true, sasa naona serikali inakoleza moto uwake vizuri kwa kumwagia petrol.
 
Swali zuri sana,wamama hawa kama wameolewa mkuu waume zao watakua wanapata shida sana,yaani waume zao wanatakiwa wawe ngangari kwelikweli.Lakini mara nyingi wa mama namna hii unakuta hana mume au ameachika hebu tusikilize wadau wanaowafahamu watueleze kama wana mume manake duu.
Ya kuwa na mume na kutokuwa na mume itasaidia nini, madaktari watarudi kazini???? Je wagonjwa watapata huduma kwa kujua wanamme zao??? Madaktari watatimiziwa haja zao????? Tafadhari wacheni kupotosha malengo ya kukomboa nchi yetu, mnaleta za kuleta, mapambano bado yanaendelea!!!!

Kuandamana ni haki ya raia na si wana CCM peke yao,uvunjivu wa amani wanauleta viongozi wao wenyewe,je pinda angetumia busara hawa akina Nkya wangeandamana kwa ajili ya kitu gani?,mbona siku nyingine hawaandamani,kuwakamata wanaharakati sio ufumbuzi ,ufumbuzi wanao akina Pinda wenyewe.
Kwanza huyo Pinda asijiite tena Mwana wa mkulima,mwana wa mkulima gani ambaye hana uchungu na waana wa wakulima ?wanaoathirika na huo mgomo wa madktari sio wabunge na familia zao,wala mawaziri ni sisi akina pangu pakavu ambao hatuna uwezo wa kwenda private hospital kama Aghakan,TMJ n,k
 
Sometimes I do fail to make a distinction between genuine and dishonest human rights activists. Quite often most people who refer themselves to as activists take advantage of any social crisis to add something to their status so that they can later on stand for high-profile political positions. We should be very careful not to allow a certain group of acquisitive people who disguise themselves with a solicitude to hold hostage the current health crunch to their own advantage.

This is purely envy and worse enough is fellow but a coward women sitting in the office emitting such a nasty conclusion on two brave and daring women who undisputably deserve to be uplifted to the level of HEROS. BIG SHAME ON YOU RADHIA!!!
 
Habari nilizopata sasa hivi ni kwamba boss wa kituo cha Sheria na haki za binadamu -- Helen Kijo-Bisimba na Mkurugenzi wa TAMWA Ananilea Nkya wamekamatwa muda huu na polisi maeneo ya Muhimbili na wanahojiwa katika kituo cha polisi cha oysterbay.

Nikipata habari zaidi nitawajulisha.

Hao ni mashabiki wakishapewa pesa kutoka kwa wazungu wankuja kuanzisha matatizo. Kwani jawabu la madaktari litapatikana kwa maandamano ya NGO zenu? Nyinyi ni wanasiasa mnatuzuga tuu hapa. Mbona hamkuandamana alipovuliwa ngou mkuu wa wilaya IGUNGA? Acheni ubaguzi nyieeee!
 
Kufuatia maandamano ya amani yaliyofanywa na wanaharakati wa haki za binadamu, leo polisi wamewatia mbaroni baadhi ya viongozi akiwemo Ananilea Nkya kwa kigezo cha kuandamana bila kibali. Mwenye taarifa zaidi atujuze wandugu

Huyu mama matatizo mengine huwa wanajitakia wenyewe, sheria iko wazi kwa nn uandamane bila kibali ? mwache aonje joto ya jiwe kwanza ndio atatia akili

Sometimes I do fail to make a distinction between genuine and dishonest human rights activists. Quite often most people who refer themselves to as activists take advantage of any social crisis to add something to their status so that they can later on stand for high-profile political positions. We should be very careful not to allow a certain group of acquisitive people who disguise themselves with a solicitude to hold hostage the current health crunch to their own advantage.

So, do you think these mamas are out there seeking cheap popularity? I don't think so. Yesterday's demonstration did make the sleeping government to pull up their socks.
And take this from me, THE GOVERNMENT WILL ULTIMATELY BOW to the docs's demands.
I still commend their move as 'heroic'. KAZENI BUTI DADA ZANGU.
 
Huyu mama matatizo mengine huwa wanajitakia wenyewe, sheria iko wazi kwa nn uandamane bila kibali ? mwache aonje joto ya jiwe kwanza ndio atatia akili

Ile ni dhalura haihitaji vibali , watu wanateketea mahosipitalini.
Mungu atawapigania watawatoa tu
 
Hao ni mashabiki wakishapewa pesa kutoka kwa wazungu wankuja kuanzisha matatizo. Kwani jawabu la madaktari litapatikana kwa maandamano ya NGO zenu? Nyinyi ni wanasiasa mnatuzuga tuu hapa. Mbona hamkuandamana alipovuliwa ngou mkuu wa wilaya IGUNGA? Acheni ubaguzi nyieeee!
Masaburisis symptoms found!
 
Ukapimwe akili!
 
Tunaomba msadie wanaharakati waliokamatwa, tuma ujumbe 0754332999 kwa kamishna Mtweve kueleza kusikitishwa kwako na hatua hii

Asante kwa hii initiative Mpiganaji NICE. Tumeshatuma Ujumbe wa kulaani kitendo hiki na kuomba waachiwe bila masharti.ji
 
Hao ni mashabiki wakishapewa pesa kutoka kwa wazungu wankuja kuanzisha matatizo. Kwani jawabu la madaktari litapatikana kwa maandamano ya NGO zenu? Nyinyi ni wanasiasa mnatuzuga tuu hapa. Mbona hamkuandamana alipovuliwa ngou mkuu wa wilaya IGUNGA? Acheni ubaguzi nyieeee!

Hawa ni mashujaa, na kitendo cha jana ni cha kishujaa. lazima tuwaweke katika Historia ya Tanzania ili vizazi vijavyo waweze kujua kuwa kulikuwa na wamama mashujaaa waliojitoa mhanga kwa ajili ya kutetea Wagonjwa walalahoi.

Je, unafikiri kama siyo juhudi zao jana, huyu PINDA angelirudi toka DODOMA na kusema aliyosema ili kurekebisha mambo.

Je, kama si juhudi za hawa wamama jana, viongozi wenu legelege wangelisimamishwa wasiingie ofisini wabaki home kwao kulima mchicha hadi kieleweke. Wangekuwa bado wanakula raha tu ndani ya L/ cruiser lenye kiyoyozi.

Fikiri kabla ya kusema siyo unasema kisiasa, hapa tunajadili mustakabali wa Taifa letu na siyo mambo ya siasa.

kutokana na juhudi za wanaharakati, na sisi wanaharakati tulio hapa JF, ndio yote haya yanafanyika, na sisi tulikuwa tunalalamika ili haya yafanyike kunusuru roho zetu na ndugu zetu.

Lakini nyie MAGAMBA MPO KISIASA NA NDIO MAANA KILA UKWELI MNAPINGA!!!!!!!

MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom