Kuna habari kuwa Polisi wamewakamata wanaharakati walioanzisha maandamano jana ya kuishinikiza serikali kuongea na madaktari. Wamewakamatia Muhimbili wakati madaktari wakiwa kwenye kikao na waziri mkuu.
kuwakamata watu hawa ni kutafuta matatizo makubwa zaidi kwani wao wameonyesha ujasiri ambao sisi watanzania tulitakiwa kuuonyesha tangu mwanzo kabisa wa sakata hili. Nawashauri polisi wawaachie kwani wanaweza kusababisha balaa zaidi
si sababu ya siri siri zao - nani alijua WM anakutana na madaktari - after all kushinikiza serikali ifumue kichwa chake na kuokota kabusara kale kadogo ka kuwa na dialogue, so much over due, na madaktari kuna ubaya gani!!!!!!!
Nadhani bado tuna nafasi ya kuitaka serikali iwajibike pamoja na viongozi wake hasa waziri wa afya...kuwakamata akina bi-simba ni janja ya kutaka kuwanyamazisha hivyo naomba tuwe kitu kimoja mara watokapo mchakato uendelee....NATAMANI TUNGEFIKIA KAMA MISRI MAANA HAIWEZEKANI MKUU WA NCHI HAONI TATIZO LA WATU KUFA na wala hagusi na watumishi wake wazembe....angechukua hataua mapema wala maafa haya yasingetokea....yaani wamekubali raia wafe kwa ajili ya 10000?
Mama zangu kejo bisimba,mama nkya kaza buti.nyie ni wamojawapo wa wasomi wa nch hii wasio wanafiki.moto wenu tunausapoti na tutawaunga mkono kwa harakat zenu. Angalizo, naisi watu wa dar ni wanafiki sana.mageuz/mapinduz ya kweli yangeanzia hapo dar. Kaz ya dar isiwe kunywa kahawa,kupigwa mabomu na mafuriko bali wawe chachu ya mabadiliko
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.