Wanahabari wazalendo wako wapi.... Mbona mmenyamaza japo mwanahalisi amefungiwa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanahabari wazalendo wako wapi.... Mbona mmenyamaza japo mwanahalisi amefungiwa?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mpendwa, Jul 31, 2012.

 1. Mpendwa

  Mpendwa Member

  #1
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 55
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kufuatia uzandiki huu kwa MwanaHalisi, ninawashauri wanahabari wazalendo wa Taifa hili wamlinde Kubenea na gazeti lake kwa kugoma kuandika mazuri yote ya Serikali kwani serikali inaingilia uhuru wa vyombo vya habari na haitaki kukosolewa. kitu ambacho nimekiona hapa ni kwamba mabavu ndiyo yanayotumika na sikwa hoja kwani mtu mchonganishi anaweza kushitakiwa na si kufungia gazeti kwani kile kilichoandikwa tayari kipo kwenye minds zetu wananchi. Serikali hii fisadi imeshindwa kukanusha kwani kila kilichoandikwa kina ushahidi, wameamua kulifungia. Naomba kutoa hoja na kuwashauri wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari wazalendo kulilinda taifa letu dhidi ya serikali hii iliyojaa watekaji nyara.

  Nawasilisha​
   
 2. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #2
  Jul 31, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,800
  Trophy Points: 280
  Hoja imeungwa mkono, Pasco kwa niaba ya wanataaluma, majibu kwa kifupi tu!!!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. N

  Nyanko JF-Expert Member

  #3
  Jul 31, 2012
  Joined: Jul 27, 2012
  Messages: 371
  Likes Received: 219
  Trophy Points: 60
  Unajua mimi hainiingii akilini kabisa katika stage hii ya watu wengi kuwa wameamuka wakihitaji kupata habari za kweli halafu Serikali inaamua ugolo kama huu, hivi kweli kuna washauri wenye ueledi wa kazi yao? Maana mimi ninchokiona sasa ni watake wasitake wananchi watapigania haki yao, na ikiendelea kuzimwa mlipuko wake ukifika ni mbaya sana.
   
 4. kvelia

  kvelia JF-Expert Member

  #4
  Jul 31, 2012
  Joined: Jun 24, 2009
  Messages: 247
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hoja naiunga mkono. Mimi nafikiri ifike mahali kama gazeti moja wakilifungia liwepo lingine kimbilio basi. Nimesoma gazeti la mwananchi la leo kuhusu kisa cha Lisu kuwataja wabunge wa CCM kuhusika ktk rushwa, cha kushangaza wametaja wabunge watatu tu eti hao wengine wanne hawajawasiliana nao, kama hata hili lililotajwa tayari mnaogopa kuliandika JE, likija la kiuchunguzi itakuaje kama sio kama KUMWONA SIMBA UKAFICHA KICHWA UKAMWACHIA KIWILIWILI ETI UMEPONEA CHUPU CHUPU, Hali ni mbaya sana.
   
 5. b

  bullof New Member

  #5
  Aug 1, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hii sheria ya magazeti ya 1976 ni kati ya sheria 25 zilizo orodheshwa na Nyalali, aliyekuwa jaji mkuu, zinazotakiwa kufutwa. Sheria hii hutumika kufuta magazeti yanayo kosoa serikali na kuvitisha vyombo vingine vya habari. Kwa sheria hii ya Magazeti ya 1976 serikali ndiyo mlalamikaji, mwendesha mashitaka na hakimu. Ndiyo maana mara ya kwanza Mwanahalisi lilipofungiwa Waziri Mkuchika wakati huo akiwa waziri anaye husika na mambo ya habari aliongea kwa kiburi na kusema ana mamlaka ya kulifungia gazeti ambao hawakuridhika shauri yao. Ziko sheria nyingine ambazo zingetumika dhidi ya gazeti au mhariri wa Mwanahalisi badala ya kukimbilia kulifungia gazeti, mfano kunasheria zinazohusiana na uchochezi (sedition) na mambo ya kashfa (defamatory statement) . Kama Mtikila aliweza kufunguliwa kesi kwa uchochezi kulikuwa na ugumu gani kufanya hivyo kwa Mwanahalisi. Kama Mwanahalisi limefungiwa kutokana na taarifa za kuihusisha usalama wa taifa na utekaji wa Dr. Ulimboka, ni magazeti mangapi yaliandika hiyo habari na bado yanaendelea kuandika hiyo habari? Je huo sio ubaguzi? Hakika serikali ya ccm inajali utawala wa sheria!!

  Kwa hatua hiyo ya serikali kulifungia gazeti la Mwanahalisi imetunyima wananchi haki yetu ya kikatiba kupata habari.Tusubiri wanaharakati kuwekwa vizuizini

  Kidumu chama cha mapinduzi kwa kugoma kuongeza mishahara ya walimu na kuongeza marupurupu ya wabunge (nasikia yameongezwa kimya kimya)!! CCM hoyeeee!!
   
Loading...