Wanahabari wasio na sare za CCM watimuliwa kuchukua habari za mama Salma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanahabari wasio na sare za CCM watimuliwa kuchukua habari za mama Salma

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Fidel80, Oct 18, 2010.

 1. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #1
  Oct 18, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  Mke wa mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete mama Salma Kikwete akiwapungia mikono wanawake na wananchi wa mji wa Sumbawanga mkoani Rukwa mara baada ya kuwasili katika ukumbi wa mkutano wake wa wanachama hao eneo la Sabasaba mjini hapa leo,mama salma yupo katika kampeni za CCM mikoa ya kusini

  [​IMG]

  Waandishi wa habari wa vyombo mbali mbali mkoani Rukwa wakiwa nje ya ukumbi wa mkutano wa mke wa mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete mama Salima Kikwete baada ya kufukuzwa ndani ya ukumbi huo eneo la Sabasaba wakati mama Salima akiwa katika kampeni zake kwa wanawake wanachama wa CCM mkoa wa Rukwa leo , aliyekaa chini ni mwandishi wa gazeti la majira Bw Prosper Mgimwa ,Judyi Ngonyani ( Chanel Tena na Adolph Mbata (TBC) jumla ya waandishi wanne walifukuzwa na kuachwa wale waliovalia sare maalum za Press Kikwete 2010
  [​IMG]

  Mwandishi wa habari aliyekuwa katika ziara ya mama salma akiendelea na kazi huku wengine wakifukuzwa.

  Wanahabari zaidi ya watano wa vyombo mbalimbali vya habari mkoani Rukwa leo wamefukuzwa katika mkutano wa mke wa Rais mama Salma Kikwete katika ukumbi wa Sabasaba mjini hapa na kuachwa wanahabari waliovalia sare za Press Kikwete 2010 ambao walikuwepo katika msafala wa mama Salima.
  Kufukuzwa kwa wanahabari hao kumeelezwa na mmoja kati ya wanahabari waliopo katika msafara wa mke huyo wa Rais kuwa katika mikutano yake ya ndani mama Salma amekuwa hapendi waandishi wa habari nje ya wale ambao amekuwa akiongozana nao katika msafara wake.

  Wanahabari hao na mwandishi wa gazeti Tanzania Daima ,majira ,TBC na Chanel Teni ambao walifukuzwa muda mufipi baada ya msafara wa mama Salima kuingia katika viwanja vya ukumbi huo ambao alikuwa akifanya kampeni za CCM za ndani katika ukumbi huo kwa kukutana na wanawake wa mji wa Sumbawanga.
  Hata hivyo baada ya kutolewa ndani ya ukumbi huo wanahabari hao waliamua uondoka katika eneo hilo la kurudi katika ofisi zao kuendelea na shughuli nyingine japo tayari baadhi yao walianza kupiga picha za kuwasili kwa mama Salma eneo hilo.

  Wakizungumza na mtandao huu wanahabari hao walisema kuwa hawajutii kufukuzwa kwao ila wanasikitishwa na ubaguzi ulipo kwa kubagua waandishi na kuwaacha wale ambao wamevalia sare za Press Kikwete 2010 huku waandishi waliovalia sare za wananchi (yaani waandishi wasio katika msafara ) wakitolewa.
  Source:Francis Godwin ni mzee wa matukio daima
   
 2. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #2
  Oct 18, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  sasa hapo ndipo hao TBC wajue kuwa wanajikomba bure kwa JK na familia yake
   
 3. S

  SUWI JF-Expert Member

  #3
  Oct 18, 2010
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 548
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Hawa CCM dawa yao kuwaondoa ifikapo 31 oct 2010... Wanatia aibu kwa matendo yao machafu... Ole wao maana siku zao zinahesabika.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Oct 18, 2010
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Duh yawezekana wa ITV na Star TV walivaa Press Kikwete 2010 wakaingia ndani kuchukua habari.!
   
 5. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #5
  Oct 18, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  [​IMG]

  Mwandishi wa habari aliyekuwa katika ziara ya mama salma akiendelea na kazi huku wengine wakifukuzwa.


  Kumbe hii kitu "Press Kikwete 2010 bado ipo???
   
 6. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #6
  Oct 18, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hii hatari na ndo maana hawataki MIDAHALOOO!
   
 7. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #7
  Oct 18, 2010
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  kikwete lazima awaambie aliyemfundisha kuifanya ikulu nyumba ya walanguzi km lowasa,rostamu na ikulu mt=radi wa familia...........NATAKA AWAAMBIE WATANZANIA ALIYEMFUNDISHA NANI? NI NYERERE ANYESEMA ANAMUENZI KWA MANENO?....NI MWINYI ANAYEWAASA WATZ KUCHAGUA KIONGOZI MAKINI?............NI MKAPA AMABYE ANASEMA TUMWACHA APUMZIKE?............AU UROHO WAKE WA MADARAKA?
   
 8. F

  Froida JF-Expert Member

  #8
  Oct 18, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Huyu kweli ni mapepe hana hata akili moja anafukuza hata mtangazaji wa TBC du yaani yuko juu ya kila kitu hii kweli hii familia na masultani
   
 9. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #9
  Oct 18, 2010
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  Tofautisha muandishi wa habari na KANJANJA
   
Loading...