Wanahabari wakwepa mbinu chafu za ccm kuwalaza katika danguro mafinga

Mpandafarasi

Member
Dec 7, 2008
57
11
Wanahabari wa vyombo mbali mbali mkoani Iringa leo jana walionyesha kuwa wao si watu wa kupelekwa pelekwa na chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa baada ya kugoma kulazwa katika gesti moja mji mafinga wilaya ya Mufindi ambayo CCM ilikuwa imewaandalia wanahabari hao zaidi ya watano ambao walikuwa katika msafara wa wanazi mkuu Mizengo Pinda baada ya kubaini kuwa gesti hiyo ni maarufu kwa biashara za shoti taimu a.k.a Danguro mjini Mafinga.

CCM ambayo ilikuwa imewaalika wanahabari hao ili kushiriki matembezi ya mshikamano pamoja na sehere za miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM sherehe zilizofanyika Ifwagi Mufindi kimkoa na kuhudhuriwa wa na waziri mkuu Mizengo Pinda ,walipata kuwaandalia wanahabari hao vyumba katika gesti hiyo iliyopo mjini Mafinga .

Ila baada ya waandishi kufika katika gesti hiyo na kuingia katika vyumba vyao ndipo walipobaini kuwa gesti hiyo si ya kawaida baada ya kupishana na wageni wengine mlangoni wakitoka kufanya mapenzi ya chapu chapu a.k.a shoti taimu katika vyumba hivyo.
Kilichofanya wanahabari hao kugoma kulazwa katika vyumba hivyo ni baada ya kuona mashuka na vyumba vyao vikiwa vimetapakaa uchafu wa kuime ambao unaonyesha kuwa vyumba hivyo kutumika kabla ya wao kuingia.

Kutokana na hali hiyo wanahabari hao walilazimika kuachana na vyumba hivyo vya CCM na kwenda kupanda hotel yao ambayo walihisi kuwa na hadhi na heshima tofauti na hiyo ya CCM. Wakati huo huo posho ya wanahabari hayo iliyoandaliwa kwa ajili yao inadaiwa kutafunwa na mmoja kati ya viongozi wakubwa wa CCM mkoa wa Iringa na kujitkuta wakielezwa kuwa itifaki imezingatiwa kwa wao kuambulia posho ya shilingi 15,000 kwa kila siku kwa muda wa siku bili.

Wakati viongozi wa CCM wilaya ya Mufindi wakimtuhumu mmoja kati ya viongozi wa juu wa CCM mkoa wa Iringa kuwa ametafuna posho za wanahabari hao ,mwenyewe ajitetea kuwa si kweli na kuwa itifaki imezingatiwa.

Source: Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima
 
WANAHABARI WAKWEPA MBINU CHAFU ZA CCM KUWALAZA KATIKA DANGURO MAFINGA

DSCF9902.JPG

Wanahabari wa vyombo mbali mbali mkoani Iringa leo jana walionyesha kuwa wao si watu wa kupelekwa pelekwa na chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa baada ya kugoma kulazwa katika gesti moja mji mafinga wilaya ya Mufindi ambayo CCM ilikuwa imewaandalia wanahabari hao zaidi ya watano ambao walikuwa katika msafara wa wanazi mkuu Mizengo Pinda baada ya kubaini kuwa gesti hiyo ni maarufu kwa biashara za shoti taimu a.k.a Danguro mjini Mafinga.

CCM ambayo ilikuwa imewaalika wanahabari hao ili kushiriki matembezi ya mshikamano pamoja na sehere za miaka 35 ya kuzaliwa kwa CCM sherehe zilizofanyika Ifwagi Mufindi kimkoa na kuhudhuriwa wa na waziri mkuu Mizengo Pinda ,walipata kuwaandalia wanahabari hao vyumba katika gesti hiyo iliyopo mjini Mafinga .

Ila baada ya waandishi kufika katika gesti hiyo na kuingia katika vyumba vyao ndipo walipobaini kuwa gesti hiyo si ya kawaida baada ya kupishana na wageni wengine mlangoni wakitoka kufanya mapenzi ya chapu chapu a.k.a shoti taimu katika vyumba hivyo.

Kilichofanya wanahabari hao kugoma kulazwa katika vyumba hivyo ni baada ya kuona mashuka na vyumba vyao vikiwa vimetapakaa uchafu wa kuime ambao unaonyesha kuwa vyumba hivyo kutumika kabla ya wao kuingia.

Kutokana na hali hiyo wanahabari hao walilazimika kuachana na vyumba hivyo vya CCM na kwenda kupanda hotel yao ambayo walihisi kuwa na hadhi na heshima tofauti na hiyo ya CCM.

wakati huo huo posho ya wanahabari hayo iliyoandaliwa kwa ajili yao inadaiwa kutafunwa na mmoja kati ya viongozi wakubwa wa CCM mkoa wa Iringa na kujitkuta wakielezwa kuwa itifaki imezingatiwa kwa wao kuambulia posho ya shilingi 15,000 kwa kila siku kwa muda wa siku mbili.

Wakati viongozi wa CCM wilaya ya Mufindi wakimtuhumu mmoja kati ya viongozi wa juu wa CCM mkoa wa Iringa kuwa ametafuna posho za wanahabari hao ,mwenyewe ajitetea kuwa si kweli na kuwa itifaki imezingatiwa.
 
magamba bwana, yani mchana waumini waliwakimbia pale uwanjani sasa hivi makuwadi wao wakuu wanawagomea kupinduka??
 
Huyu itakuwa mwandishi wa Tanzania daima

Mikutano ya CCM huwa inawaalika waandishi wa Tanzania daima? Sema waandishi wa Gezati na Radio Uhuru, bila kuwasahau TBC1.

Tatizo magamba huchangamkia mtu anapomhitaji, na akishamutmia basi ndani ya trash.
 
Huyu itakuwa mwandishi wa Tanzania daima
Natumaini Dada yangu FF utakuo umeona uhalali wa vibasha. Kitendo cha kuwalipa waandishi vibahasha vyembamba vya 15,000 kwa siku ni unyanyasaji kwa waandishi wa habari. Hapa mjini vibahasha vya nauli havipungui 20,000 bado kula na kulala, halafu ulipwe 15,000!, hayo yamewezekana Iringa tuu!.
 
Huyu itakuwa mwandishi wa Tanzania daima

Umejuaje? au ni yaleyale ya utabiri wa akina Shehe Yahya. Changia mada acha ku-attack gazeti, hapa ulitakiwa ujikite katika kuhoji ukweli wa hii habari kwasababu haina hata source.
 
Aisee! Halafu huo msafara wa mizengo ulituletea usumbufu sana kwa wale waliokuwa wanasafiri mikoa ya Mbeya na Songea kwa siku ya jana maeneo ya kambi ya JWTZ kabla hujafika mizani ya Makambako.

Kwani ilitulazimu kusubiri saa mzima eti Mizengo anatoka Mafinga kuelekea Iringa kaazi kweli kweli!!
 
Huyu itakuwa mwandishi wa Tanzania daima

Usiwe mtu wa chuki na visasi muda wote; Soma kwa kifupi profile ya huyo mwandishi ama fuatilia link aliyotoa kwenye hiyo post:

Jina langu ni Francis Godwin mkurugenzi wa kampuni ya Free Community Media's yenye makao makuu Marekani na Tanzania pia mimi ni Mwandishi wa habari wa kujitegemea nchini Tanzania makao yangu ni mkoani Iringa Call.0754026299 , 0712750199 simu ya nyumbani.0262700675 barua pepe;francisgodwin2004@yahoo.com
 
Waandishi tarajieni kuendelea kunyanyasika sana mpaka pale
mtakapoungana na kudai maslahi bora toka kwa waajiri wenu
ambao wanawalipa fedha kidogo kama polisi, jambo linalowafanya
muwe ombaomba na kutarajia vibahasha kila mnapoalikwa kwenye
matukio...hivi kulikuwepo na umuhimu kwa waandishi kukodiwa pa
kulala na kukirimiwa na chama(ccm) wakati walikwenda kazini??!!
Je, hii inatofauti gani na mbunge kudai sitting allowance ilhali kuwepo
bungeni ni kazi yake??? Hivi kweli mwandishi anaweza kuandika habari
za kweli zenye negative impact dhidi ya aliyemkirimu???
LAZIMA WAANDISHI WETU MMBADILIKE, JIHESHIMUNI ILI MUHESHIMIWE
 
Hivi aljazeera wakienda kuripoti matukio ya Syria, Wanalipiwa hotel na Syria?
No wanalipiwa na aljazeera. na wako tayari kuweka maisha yao in risk sababu pesa wanayopata ni kubwa inaweza lisha familia.

Hapa hamdai chenu, mnaishia kuripoti kile akitakacho mtoa bahasha.

Waandishi amkeni mjitaftie heshima yenu, wenzenu Ulaya ni kama celebrities
 
Back
Top Bottom