mzee wa miba
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 759
- 125
Wanahabari wa Sumbawanga waliojipambanua dhahiri kama makada na washabiki wakubwa wa ccm leo wamepata kichapo na zomea zomea ya nguvu ya umma pale mahakama ilipotengua ubunge wa bw aeshi. Kadhia hiyo ilijitokeza kwa bw Sami Juma Kisika "ambaye ni repoter wa RFA Rukwa, afisa uhusiano wa Manispaa Ya Sumbawanga na katibu wa klabu ya waandishi wa habari Rukwa" na pia bw Musa Hassan mwangoka mwandishi wa gazeti la mwanachi na katibu msaidizi wa kalabu ya waandishi wa habari Rukwa.
Waandishi hao walionekana kushabikia dhahiri ccm na bw Aeshi kwani walishashindwa kuripoti lolote tangu kesi hiyo ifunguliwe mwaka juzi sababu kubwa ni kuogopa kumdharirisha mpendwa wao bw Aeshi, lakini leo wakati wa hukumu walifika mahakamani huku wakijua fika mpendwa wao bw Aeshi ataibuka kidedea kwa bahati mbaya mategemeo yakawa tofauti kabisa na hivyo mara tu baada mahakama kuu kumvua ubunge bw Aeshi hasira za mashabiki zikawageukia wao kwa kuwazomea na kuanza kuwapa kichapo bahati yao wanausalama wakawakoa.
Kwa sasa bw Sami Juma kisika ni mjumbe wa baraza la uvccm na amekuwa akionesha upendeleo wa wazi kwa ccm kwa kuwa na interest na ccm hali ambayo kwa wanasumbawanga wamekuwa wakikeleka kwa hilo kwani zaidi ya afisa uhusiano wa manispaa pia ni msimamizi mkuu wa Sumbawanga Tv sasa jamaa ni bias sana huwa habalance stori na kila mara Sumbawanga Tv ni ccm tu.
Wakuu kama wapo watu wenye tabia kama hawa waandishi njaa au uchwara ni vema wakajipambanua wakawa kwenye vyombo vya vyama husika na si vyombo vya umma kama TBC kwani nguvu ya umma inakuja kwa kasi sana
Safi kabisa hongereni wana CDM sumbawanga unajua hivi vyombo vya magamba k.v.TBsi wao wamekuwa mstali wa mbele kutubania habari za wapinzani,mara nyingi habari za uovu wa serikali na madudu ya mafisadi,au habari nzuri za Chadema hawazionyeshi,najua hicho ni kiama chao,bora watu siku hizi baada ya Tido kuondolewa tumehamia Star tivi.Aitiv na zinginezo uhakika wengi wao wamenunuliwa na mafisadi na wanaelekezwa kwa rimote control kile mafisadi na serikali legelege ya Jeikei wanayotaka yatangazwe na yale ambayo hawataki yatangazwe,ukweli ndo huo kiama chao kinakuja hata wakifanya utafiti huru Tibisi ya Tido ilikuwa juu sana na sasa wengi wa watanganyika wamepoteza imani nayo na hata mauzo ya matangazo ya biz yameshuka.