Wanahabari Sumbwanga wapata kichapo toka kwa mashabiki wa CHADEMA

Safi sanaaaaaa...
Sasa hivi silaha ni kuzomea tu...
Jk zomea...
mawaziri zomea...
Makada zomea...
Uooooooooooooooooh!
 
Wakuu inabidi popote tunapoona baadhi ya watendaji wanaenda kinyume na maadili ya utendaji kazi basi tuwazomee mpaka wakome kabisa maana wanakera sana hawa kuku.
 
Nchi yetu ni ya amani, CDM mnashabikia vurugu
ivi unaelewa maana ya amani?
au uanshabikia tu...siamini kuwa nchi yetu ni ya amani wakati kila siku mauaji yanatokea....
pita manzese usiku afu uone kama nchi hii ni ya amani ama la! pia kuonyanyaswa then ukakaa kimya
hou ni wendawazimu,(abnormality),unapigwa then unachekacheka tu na kutoa udenda? wot hell is this ebo, umenichefua,
ngoja niende jukwaa la jokes labda ntacheka.
 
Wanahabari wa Sumbawanga waliojipambanua dhahiri kama makada na washabiki wakubwa wa ccm leo wamepata kichapo na zomea zomea ya nguvu ya umma pale mahakama ilipotengua ubunge wa bw aeshi. Kadhia hiyo ilijitokeza kwa bw Sami Juma Kisika “ambaye ni repoter wa RFA Rukwa, afisa uhusiano wa Manispaa Ya Sumbawanga na katibu wa klabu ya waandishi wa habari Rukwa” na pia bw Musa Hassan mwangoka mwandishi wa gazeti la mwanachi na katibu msaidizi wa kalabu ya waandishi wa habari Rukwa.

Huyu mwandishi kweye red itabid Tido Mhando amshughulikie.....sidhani mzee wangu atavumumilia ujinga...wote tunamfahamu Tido......hawezi dhalilisha gazet makini kama Mwananchi
 
Wanahabari wa Sumbawanga waliojipambanua dhahiri kama makada na washabiki wakubwa wa ccm leo wamepata kichapo na zomea zomea ya nguvu ya umma pale mahakama ilipotengua ubunge wa bw aeshi. Kadhia hiyo ilijitokeza kwa bw Sami Juma Kisika “ambaye ni repoter wa RFA Rukwa, afisa uhusiano wa Manispaa Ya Sumbawanga na katibu wa klabu ya waandishi wa habari Rukwa” na pia bw Musa Hassan mwangoka mwandishi wa gazeti la mwanachi na katibu msaidizi wa kalabu ya waandishi wa habari Rukwa.

Waandishi hao walionekana kushabikia dhahiri ccm na bw Aeshi kwani walishashindwa kuripoti lolote tangu kesi hiyo ifunguliwe mwaka juzi sababu kubwa ni kuogopa kumdharirisha mpendwa wao bw Aeshi, lakini leo wakati wa hukumu walifika mahakamani huku wakijua fika mpendwa wao bw Aeshi ataibuka kidedea kwa bahati mbaya mategemeo yakawa tofauti kabisa na hivyo mara tu baada mahakama kuu kumvua ubunge bw Aeshi hasira za mashabiki zikawageukia wao kwa kuwazomea na kuanza kuwapa kichapo bahati yao wanausalama wakawakoa.

Kwa sasa bw Sami Juma kisika ni mjumbe wa baraza la uvccm na amekuwa akionesha upendeleo wa wazi kwa ccm kwa kuwa na interest na ccm hali ambayo kwa wanasumbawanga wamekuwa wakikeleka kwa hilo kwani zaidi ya afisa uhusiano wa manispaa pia ni msimamizi mkuu wa Sumbawanga Tv sasa jamaa ni bias sana huwa habalance stori na kila mara Sumbawanga Tv ni ccm tu.
Wakuu kama wapo watu wenye tabia kama hawa waandishi njaa au uchwara ni vema wakajipambanua wakawa kwenye vyombo vya vyama husika na si vyombo vya umma kama TBC kwani nguvu ya umma inakuja kwa kasi sana

Vipi wa Tbc hakuwepo?
 
Joshua Joel wa ITV sikumsikia wakati wote wa kesi hii sijui alikuwa upande gani?
 
Waandishi hao walionekana kushabikia dhahiri ccm na bw Aeshi kwani walishashindwa kuripoti lolote tangu kesi hiyo ifunguliwe mwaka juzi sababu kubwa ni kuogopa kumdharirisha mpendwa wao bw Aeshi, lakini leo wakati wa hukumu walifika mahakamani huku wakijua fika mpendwa wao bw Aeshi ataibuka kidedea kwa bahati mbaya mategemeo yakawa tofauti kabisa na hivyo mara tu baada mahakama kuu kumvua ubunge bw Aeshi hasira za mashabiki zikawageukia wao kwa kuwazomea na kuanza kuwapa kichapo bahati yao wanausalama wakawakoa.
Mara zote yanapotokea kama haya huwa ninatoa mfano wa kisa cha "mwenye busara aliyeibiwa nguo mtoni na chizi. Mwenye busara akatoka mtoni uchi na kumfukza chizi hadi kijijini kufuatilia nguo zake". Busara za CDM au yeyote mwenye tabia kama hizi zitakuwa ziko wapi ikiwa wataanza kumpa kichapo kila anayeshabikia CCM au asiyeshabikia CDM?

Kwa njia za kistaarabu tunaweza kuwazomea na hata kuwasusia, lakini hilo la kutembeza kichapo...ningewashauri viongozi wote wa vyama na washabiki wao wasilipalilie wala wasilishangilie sana. Tunaloliona dogo na la kufurahisha leo, kesho linaweza kuwa kubwa na la kuliza.

Ni mawazo yangu tu, kwa sauti kubwa.
 
Vipi wa Tbc hakuwepo?

Tbc walikuwepo ila jamaa anaumwa kisukali inamsumbua sana "Swima Ernst" alionekana mahakamani lakini yeye hana shida na si kada ila afya ndo changamoto inakabili sana. Na kama unakumbuka alillipoti on the sport TBC1 na TBC2 baada ya hukumu
 
Wangewachinja na kuwaulia mbali hao waandishi wa habari-ccm.

Hapana MD; Tabia hiyo wameshaianza hawa magamba kwa kuwachinja viongozi wa CDM. Ila mimi naona sio busara kulipa ubaya kwa ubaya. Nawashauri wafuasi wa CDM wawatendee mema maadui wao, hivi ndivyo dini zetu zinavyotufundisha.
 
kumbe, ndio maana hiyo habari haikutangazwa na Itv kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku
 
Mara zote yanapotokea kama haya huwa ninatoa mfano wa kisa cha "mwenye busara aliyeibiwa nguo mtoni na chizi. Mwenye busara akatoka mtoni uchi na kumfukza chizi hadi kijijini kufuatilia nguo zake". Busara za CDM au yeyote mwenye tabia kama hizi zitakuwa ziko wapi ikiwa wataanza kumpa kichapo kila anayeshabikia CCM au asiyeshabikia CDM?

Kwa njia za kistaarabu tunaweza kuwazomea na hata kuwasusia, lakini hilo la kutembeza kichapo...ningewashauri viongozi wote wa vyama na washabiki wao wasilipalilie wala wasilishangilie sana. Tunaloliona dogo na la kufurahisha leo, kesho linaweza kuwa kubwa na la kuliza.

Ni mawazo yangu tu, kwa sauti kubwa.
Tatizo busara ilishapotea toka kwa wale wanaotumia rasilimali za umma kwa ajili ya manufaa ya chama kimoja kilichopo madarakani, hebu anza kuwambia hao kwanza watumie busara. Mfano ni pale ccm wanaponyang'anya viwanja tulivyojenga kwa nguvu ya wananchi wote eti leo viwanja vyote vya ccm utadhani vilijengwa na ada zilizokusanywa na ccm. huo ni mfano tu
 
Huu ni mtandao unaoheshimika sana lakini inashangaza sana kuona kuna taarifa zinawekwa zisizo na ukweli, kuhusu suala la kupigwa wanahabari kiukweli halipo na hakuna mwandishi aliyepigwa. zaidi alizomewa Bw. Kisika na wafuasi wa Chadema. Mussa Mwangoka si katibu msaidizi wa klabu, lakini alikuwa karibu na kisika wakati kada huyo wa CCM akizomewa. taarifa.... tuwe makini tunapoweka taarifa hizi kwenye mtandao!. tutafanya mtandao huu udharaulike. kama ivyodhaurika CCM na wafuasi wake. aliyeweka hiyo taarifa si mtu makini na hajui alichokiandika.
 
Back
Top Bottom