Wanahabari na vyombo vyao wengi ni waganga njaa kuliko kutoa huduma ya habari

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
10,408
7,190
Wanahabari wengi na vyombo vyao zaidi wapo kufanya biashara kuliko kutoa huduma sahihi ya habari. Wakiwa chini ya ushawishi mkubwa wa falsafa ya kimagharibi wanaona habari za uzushi uongo kuhusu sera zinazochukiwa na wazungu ndio zinauza kuliko kuandika au kusema kweli yenye manufaa kwa maendeleo ya nchi zao.

Kwa mfano hadi wapinzani wazandiki kama lissu ambao hawataki kusema chochote chema kuhusu mwendazake magufuli wakibanwa wanakubali kwamba magufuli kafanya mengi kuhusu uchumi. Lakini wanalotaka wao lisikike kuhusu magufuli ni kibano alichowapa wala rushwa na fisadi eti ni kivunja haki za binadamu.

Wanajifanya hawajui au kuona kwamba kibano kwa fisadi wala rushwa na wazembe ni mojawapo ya mchango mkubwa kwa mafanikio iliyopata tanzania chini ya magufuli kwa maendeleo kiuchumi.

Nachotaka kusema unapokua na wanahabari na vyombo vya habari vinavyoenzi sera na itikadi za kigeni zisizokua na tija kwa maendeleo ya nchi lazima kua na sheria kuvifanya kutokua kikwazo dhidi ya mwelekeo wa taifa.

Kwa hivyo mama samia na serikali yake wawe macho na makini na ulaghai wa wanahabari. Wao wana fulsa kubwa kutoa habari za ulaghai ili waachwe kutumika na adui wa nchi au kufanya lolote mradi kupata pesa.
 
Unamaanisha wanahabari wakimataifa ama wa kwetu hapa?

Maana kama ni wanahabari wa hapa Tanzania kwa kiasi kikubwa wamekuwa mstari wa mbele kuelezea mafanikio, Sera na mikakati ya serikali ukiachilia mbali wale wanaotumikia vyombo vya habari vinavyomilikiwa na vyama vya upinzani.
 
Asee mbona mmewakomalia hawa wadau this week from monday, what's goin on there?
........ 👇🏾
 
Back
Top Bottom