Wanahabari na Kiswahili: Je, ni neno lipi la Kiswahili sanifu huanza kwa consonant "C" na vowel "O"? Virusi wale ni sahihi kuwandika Corona au Korona?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa jamiiforums

Ndugu zangu watanzania;

Je, ni neno lipi la Kiswahili sanifu huanza kwa consonant "C" na vowel yoyote ile kama "O"? Virusi wale ni sahihi kuwaandika Corona au Korona?

images (27).jpg

Kwa kawaida ya uandishi wa lugha hii ya Kiingereza maneno yanayotamkika kwa consonant "C" katika Kiswahili huandikwa kwa Consonant "K". Mfano neno "Cairo".

Cairo ni mji mkuu wa nchi ya Misri mara nyingi limekuwa likiandikwa kama "Kairo" katika magazeti na machapisho mbalimbali ya lugha ya Kiswahili.

Kama tuliweza kutohoa neno "pneumonia" na kuwa linaandikwa kama "Nimonia" kwa kuwa tulifahamu fika kwamba mpangilio wa futuatana wa consonat "ph" sio mlolongo sahihi katika kuunda neno la kiswahili, kwanini "Corona" bado haijarasimishwa na wanahabari ili lile linaandikwa kwa usahihi wake kama "Korona"?

NJE YA MADA KIDOGO: Alafu lile neno "MBASHARA" linayoandikwa na TBC ARIDHIO muda wa tarifa za habari jioni ni sahihi ama linapaswa kusomeka kama MUBASHARA? Kuna herufi "U" inasahaulika katikati ya herufi za M na B au mimi ndio mshamba?

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
ANGALIZO: Kuna watu wapo humu jamiiforums hawanipi pesa ya kula wala kuweka data ila wameanza kunipangia masuala ninayopaswa kuandika. Nitawaweka IGNORE LIST woooote. I have no time for nonesense.
 
Kwenye mbashara imetumika kanuni ya udondoshaji. Kwenye corona hatujapata mbadala wa COVID ya kiswahili hivyo neno hilo limekopwa na linatumika kama lilivyo kama tunavyotumia maneno mengine tuliyokopa tangu mwanzo.

Hivyo hakuna makosa katika uandishi wa neno corona.
 
Habari za wakati huu kaka na dada zangu wote wa hapa jamiiforums...

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
Mubashara ni sahihi na udondoshaji wa irabu (kutokuitamka herufi tajwa) hakuathiri maana ya neno baadhi wabobezi wa lugha kwa mfano wanasema ni mulienda na sio mlienda.

Kuhusu Cairo na Kairo ni kwa sababu tu matamshi ya neno kama yanavyotamkwa na wenye lugha yanasadifiwa katika matamshi na maandishi katika lugha lengwa. Hivyo si kosa katika kiswahili kuandika kairo badala ya cairo kwa sababu katika kiswahili ilitulimke jina hilo kama linavyopaswa kuwa ni lazima tuliandike kairo.
 
Bakita wametoa jina mbadala la Korona hata hivyo mimi sikukubaliana nalo kwani halikuangalia chanzo cha nina Corona, Corona si jina jipya limetumika kwa shuvhuri mbalimbali kama Corona mtambo wa kuchakata mkonge, Vorona modeli ya gari ya Japani, Womens Corona ambacho ni chama cha wanawake na Corona taji la mfalme na hapa ndipo chanzo cha kirusi kupewa jina kutokana na maumbile yake.

Kama ilivyo Kairo ndivyo zilivyo Kongo, Amerika, Afrika na kwingine kote.
 
Okay
 
CORONA si neno jipya kama wengi wanavyodhani, Corona ni taji au kofia ya mfalme au malkia, kutokana na muonekano wa umbile la kirusi husika, wanasayansi wakakipa utambulisho huo, bahati mbaya BAKITA hawakuzingatia hilo.
 
Back
Top Bottom