Wanahabari, Kikwete aliwaambia wanakula rushwa, kimya; Mkapa kasema.., kelele!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanahabari, Kikwete aliwaambia wanakula rushwa, kimya; Mkapa kasema.., kelele!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzizi wa Mbuyu, Mar 24, 2010.

 1. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #1
  Mar 24, 2010
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,495
  Likes Received: 1,052
  Trophy Points: 280
  Waandshi wetu wa habari wamenishangaza kweli kwa hatua yao ya kukaa kimya dhidi ya tuhuma kuwa wanakula rushwa kwa ujumla wao tuhuma zilizotolewa na raisi wa Tanzania ndugu Kikwete. Yaani huwezi amini zaidi ya mzee Ndimara Tegambwage kunung'unika kidogo, wengine woote wamekaa kimya kama vile hawakusika kilichosemwa juu yao!

  Sasa cha ajabu, Mzee Mkapa nae karudia hayo hayo akiwa nchi jirani ya Kenya ila yeye katumia lugha ya kiungwana kidogo kwa kusema waandishi wa Tanzania hwana uzalendo na hawana uelewa wa mambo kabisa, yaani kwa mambo ambayo hata wanayauliza?!..........Lolo! waandishi wamechachamaa, sasa wanampelekea mashambulizi makali Mkapa...

  Hii inakuwaje?... waandishi wa Tanzania wanamuogapa JK? Au wanasubiri nae astaafu?, au ni kweli kawapa rushwa ili wasimuandame?
   
 2. Mwana wa Mungu

  Mwana wa Mungu JF-Expert Member

  #2
  Mar 24, 2010
  Joined: Aug 14, 2008
  Messages: 1,007
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  wanamwogopa, kwani siri?
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Wamtukane JK wanyimwe mialiko ya Ikulu na safari za kutalii nae!
  Njaa mbaya ndugu!...kwetu tunasema "Njala likoko, yikoma na Muhavi!
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Siyo kwamba wanamuogopa. Ni unafiki tu.

  Wao wanafahamu kuwa kwa sasa ndiye anawalisha na lazima watetee tawi walilokalia.

  Pesa imewafanya wawe vipofu kiasi kwamba hata wakitukanwa, wao wanacheka tu.

  Subiri tu siku Kikwete ataondoka madarakani, ndiyo utawaona watakavyoanza kumsiliba.

  Kwani akiondoka, hawatakuwa na shida naye tena na kisima chake kitakuwa limited.
   
 5. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #5
  Mar 24, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ukiona wamekaa kimya kuhusu rushwa ujeu kuna ukweli so msg send.
  kuhusu mkapa mh sina la kuongea niwapishe greatthinkers
   
 6. Chakaza

  Chakaza JF-Expert Member

  #6
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2007
  Messages: 23,650
  Likes Received: 21,865
  Trophy Points: 280
  Ni aibu kwa kweli. Nakumbuka ile katuni ya gazeti moja la Kenya ikionyesha waandishi wakilamba viatu vya JK sasa naona ni sahihi kabisa ingawa wao walipiga kelele sana kulalamika kuwa wanadhalilishwa.
  Namsifu mzee Ndimara kwa kujaribu kusema bila woga ingawa anakosa support ya wenzake ambao wengi ni waoga na mamluki wa kiwango cha juu kabisa.
  Waandishi wa TZ wanamchango mkubwa kwa taifa hili katika kupoteza kwetu Dira,hilo haliwezi kupingika.
   
 7. N

  Nanu JF-Expert Member

  #7
  Mar 24, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ni ukweli usiopingika kuwa baadhi ya waandishi ni njaa kali na ni kweli wanapata mlungula. Kama mwandishi unapewa usafiri sehemu ya kulala chakula na fedha ya mfukoni kuna rishwa zaidi ya hiyo? hata hao unaowasikia wakiandika sana kuhusu watu fulani wao pia wako kwenye payroll ya watu fulani. waungwana ni wachache mno. JK anayajua hayo yote!!
   
 8. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #8
  Mar 24, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,566
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Hivoo, hata Kubenea?
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Ndiyo yaleyale ya kunya anye kuku... akinya bata kaharisha!!! Nakumbuka usemi wa JK wa 70% ni fuata upepo tu..
   
 10. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #10
  Mar 24, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,519
  Likes Received: 2,108
  Trophy Points: 280
  [ame="http://www.youtube.com/watch?v=JccLu3zd-t8&feature=related"]YouTube- Mkapa, Maathai reflections at media conference[/ame]
  Hivyo JF tuendeleze majadiliano na maswali ili kujaza 'vacuum' hii iliyopo ktk vyombo vya habari
   
 11. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #11
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Yuko sawa bana, mi namkubali kwa hilo!
  Vyombo vyetu vya habari vinayumba sana, njaa inavisabishia dhoruba kali!
   
 12. M

  Milindi JF-Expert Member

  #12
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 3, 2009
  Messages: 1,210
  Likes Received: 369
  Trophy Points: 180
  Ukiangalia kwa makini JK alivyokua anatafuta urais 2005,hakuna mwanahabari ambaye anaweza kubisha kuwa hakufaidika sana na mkwanja toka kwa JK.Na JK anawafahamu wote aliowarambisha anaowarambisha na atakawarambisha kuanzia sasa mpaka atakachukua utawala wa kipindi cha pili.Je unaweza vipi kumfahamu mtoa rushwa wakati wewe hutoi.Ndio maana wote wamekaa kimyaa.Wanapata habari inayomhusu kigogo fulani halafu wanamuuliza itoke au isitoke je unategemea nini hapo///????.MLINGULA.......!!!!!!
   
 13. N

  Nanu JF-Expert Member

  #13
  Mar 24, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mkapa hajatukana waandishi amesema alikuwa anataka waandishi wakija wawe wanamefanya utafiti wa kitu wanachokizungumzia na wanakijua vizuri.
  hii ina maana waandishi wasiwe watu wa kuandika umbea mtupu tu!
   
 14. Kachanchabuseta

  Kachanchabuseta JF-Expert Member

  #14
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 8, 2010
  Messages: 7,290
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Hapa mkapa hajawaponda bwana but amesisitiza waandishi kuandika vitu with clear evidence
   
 15. U

  Ubungoubungo JF-Expert Member

  #15
  Mar 24, 2010
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 2,508
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  wapi huko kwenu mkuu, manake ulivyoongea nimecheka sana. njara likoko naona kama unamaanisha njaa ni mnyama mkali....hahaha.
   
 16. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #16
  Mar 24, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Clear evidence my foot! Fedha za EPA zimechukuliwa kutoka kwenye coffers za Serikali akiwa kiongozi wa nchi na bila shaka kwa baraka zake. Ili kuweza kupata 'clear evidence' inabidi yeye akiri juu ya hilo ili waandishi waweze kupata 'clear evidence'. Je anaweza kukiri?
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu, una uhakika kweli Mkapa amerudia kuyasema aliyoyasema Kikwete?
   
 18. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #18
  Mar 24, 2010
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Of course, our country is in a serious leadership crisis in all its facets: the government, media, political parties, the civil society (hawa ndo usiseme)-largely reflected in the level of incompetence, great sense of irresponsibility and insensitivity. Tunahitahi kujipanga upya, hasa kiuongozi tukianza na uongozi wa juu kabisa!!
   
 19. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #19
  Mar 24, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Wakati yeye anaona tatizo kwa waandishi, waandishi wanaona tatizo kwenye uongozi! Na kati ya hao wawili mzigo mkubwa wa mabadiliko ya nchi yako kwa viongozi!
   
 20. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #20
  Mar 24, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,566
  Likes Received: 3,861
  Trophy Points: 280
  Naomba unifafanulie, waandishi wanafikiri ni kwa vipi uongozi unaathiri taaluma yao?
   
Loading...