Wanahabari ikulu - lugha za dharau, matusi na uchochezi kwa amani tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanahabari ikulu - lugha za dharau, matusi na uchochezi kwa amani tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jan 4, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Vyombo vya habari ni jicho la jamii niliandika katika moja ya blog mojawapo mashuhuri napa nchini siku chache zilizopita. Leo walionikandia kuhusu ushauri wangu kwa vyombo vya habari wanashuhudia Wanahabari wa Ikulu yetu tukufu na mahali pa heshima wanapotoa habari yenye maneno ya misemo ya vibaka mitaani kwa lugha za matusi, dharau na uchochezi ikiwa ni taarifa rasmi ya Ikulu, ni aibu tupu kwa nchi yetu. Pamoja na kusomea na kupata ujuzi wa mawasiliano ya habari na kubobea katika kusomea elimu ya rhytorics unashangaa mtu kama huyo leo anatoa hadharani lugha iliyo chini ya kiwango hata mtu asiye na taaluma ya uandishi anabaki kushangaa usanii wa vyombo vya habari vya Ikulu yetu.

  Nilisema vyombo vya habari Tanzania tunahitaji kupiga hatua moja mbele zaidi kwa kutumia taaluma yetu, leo alichoongea mwakilishi wa Rweyemamu na wakati Rweyemanu ametilia sahihi nakala hiyo kama mkuu wa mawasiliano Ikulu kujibu kauli ya Dr. Slaa kuhusiana na Richmond na Dowens ni nje ya kiwango kabisa kwa watu wanaojua na wenye taaluma ya uanahabari (lack all depth). Na huwezi amini kama huyu amewahi kuwa mhariri wa gazeti nchini.

  Wengi wa watumishi wa serikali hufanya kazi na wajibu zao zaidi kwa dalili ya kulinda maslahi binafsi kwa wakubwa wao hali inayojenga udhaifu wa kutokuwa na hali ya kujenga hoja za kujiamini ila kuwapamba wakubwa kwa mazuri tu ingawa ndani ya mioyo yao wanajua madhaifu yao.

  Kauli alizosema Mheshimiwa Rais Kikwete za kiungwana na kiustaarabu na kuheshimiana katika salamu za mwaka mpya ziko wapo wakati wanahabari wa Ikulu yake kabla hatujameza mate wameanza na kashfa za lugha chafu chafu za dharau, matusi, kejeli na uchochezi?
  Jungu kuu halikosi ukoko
   
 2. S

  S.M.P2503 JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 463
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hao wanaoitwa wanahabari IKULU kwa ufupi wanataka kupachafua mahali patakatifu na labda walikwisha pachafua siku nyingi tu maana mambo hayaanzi hivihivi...kila jambo lina mwanzo wake...
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ikulu hakuna kitu pale kuanzia wahabari hadi wafagiaji wa ofisi. Siju jk ameleta mkosi gani pale!
   
 4. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #4
  Dec 29, 2011
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  you sound so surprised
   
 5. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #5
  Dec 29, 2011
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,606
  Likes Received: 6,181
  Trophy Points: 280
  rhytorics is not an english word, perhaps you meant "rhetorics" ?
   
Loading...