Wanahabari acheni kuwa mahakimu wa ufisadi-KKKT | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanahabari acheni kuwa mahakimu wa ufisadi-KKKT

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kite Munganga, Jul 17, 2008.

 1. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2008
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Askofu: Wanahabari acheni kuwa mahakimu wa ufisadi  Na Mwandishi Maalumu, Tanga

  VYOMBO vya habari nchini vimetakiwa kutokuwa mahakama au mahakimu katika vita dhidi ya rushwa na ufisadi.

  Rai hiyo ilitolewa juzi mjini hapa na Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dayosisi ya Kaskazini Mashariki, Askofu Stephen Munga.

  Askofu Munga pia aliipongeza Serikali kwa kuendesha vita dhidi ya ufisadi kwa mujibu wa sheria na utawala wa sheria, badala ya kuongozwa na hisia na shinikizo la vyombo vya habari.

  Kiongozi huyo wa KKKT alisema hayo wakati akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa hospitali teule ya wilaya mpya ya Kilindi, katika siku ya kwanza ya ziara ya siku tisa ya Rais mkoani Tanga.

  “Naipongeza Serikali yako, kwa kuiendesha nchi kwa mujibu wa Utawala wa Sheria na hasa katika vita dhidi ya ufisadi. Endeleeni hivyo hivyo nasi tutaendelea kuwaungeni mkono.

  “Jambo moja msifanye; msiviruhusu vyombo vya habari kuwa mahakimu katika suala hili,” alisema bila kufafanua.

  Kuhusu ujenzi wa hospitali hiyo, Dk Munga alisema wazo la kujenga hospitali hiyo lilibuniwa mwaka 2003 lakini ujenzi ukaanza Januari mwaka huu kwa ushirikiano kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP).

  Dkt. Munga alisema chini ya ushirikiano huo, KKKT itajenga hospitali hiyo na Serikali itaajiri na kulipa wafanyakazi na wataalamu wa hospitali hiyo iliyopangwa kuanza kutoa huduma Februari mwakani.

  Hukumu ndio hiyo
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Jul 17, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,189
  Trophy Points: 280
  Msanii mwingine huyu hana jipya. Sasa anampongeza Kikwete kwa kupambana na mafisadi kwa lipi alilolifanya linaonyesha anapambana na mafisadi? :confused:
  Mafisadi wote bado wanapeta uraiani na utajiri wao walioupata kiharamu.
   
 3. Kiungani

  Kiungani JF-Expert Member

  #3
  Jul 17, 2008
  Joined: Feb 2, 2007
  Messages: 274
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Hawa ndiyo wale aliowasema Mzee Ruksa kuwa wamesoma lakini hawakuelimika. How sad......
   
 4. Pundit

  Pundit JF-Expert Member

  #4
  Jul 17, 2008
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 3,741
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Huyu naye Almeida nini? Inawezekana wasanii wa Almeida wameanza kuingia mpaka katika uongozi makanisani sasa.
   
Loading...