DOKEZO Wanafunzi zaidi ya 100 Mkoani Mbeya walazimishwa kushika kinyesi cha Binadamu kwa mikono na walimu wao

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Sijaona sehemu iiyohusisha dini ya walimu ila angefanya mwarabu kwa giza mgeona balaa lake humu
 
Tukio la kikatili limeripotiwa kutokea Septemba 7, 2022 majira ya asubuhi Shule ya Sekondari Songwe, Kata ya Bonde la Songwe kwa wanafunzi wa kidato cha pili na cha nne waliopo shuleni hapo kwa maandalizi ya mitihani ya Taifa.

Inadaiwa kuwa walimu wa shule hiyo ambao kwa majina ni Lugongo, Kasambala, Jengela na Geazi walikuta kinyesi cha binadamu kwenye mojawapo ya madarasa ya shule. Baada ya wanafunzi wote kuulizwa na kukana kufanya kitendo hicho, walimu hao waliamuru wanafunzi wajipange mstari kwa lazima, kisha kuwalazimisha kila mmoja kushika kinyesi kile kwa mikono kama sehemu ya adhabu.

Wanafunzi walio kataa kufanya kitendo hiki walikuwa wanapigwa hadi wakubali, na walimu hao walitoa onyo kali kuwa ikitokea siku nyingine kitendo kama hiki kitatokea tena, siku hiyo wote hawatalala na kinyesi hicho kitapakwa usoni kwa kila mmoja wao kama mafuta.
Ipo haja walimu wa huko kupimwa akili kwa dharura maana kuna upepo unaashiria hali ya hatari baada ya tukio la mauaji yaliyofanywa na Mwalimu majuzi kwa familia yake mwenyewe
 
Ni jambo la kawaida sana Sema Mizazi ya kipindi hiki inajisahaulisha maisha ya shule ya msingi miaka ya 2000 kurudi nyuma. Tunavunja maadili wenyewe tukiwa na watoto wetu nyumbani, wao nao wakivunja huko shuleni wakipewa adhabu, Tunapiga kelele as if walimu kazi yao ni mona tu kuwafundisha watoto wajue kuandika na kusoma,na si kufundisha nidhamu.


Wazazi na watz tuache kipigapiga kelele, waache walimu wafanye kazi yao kama sisi tumeshindwa kifanya.




PERIOD
 
Imenikumbusha zamani kuna walim walifanya hivi kisa watu wamejisaidia bafuni walifukuzwa
 
Back
Top Bottom