Wanafunzi zaidi waachiwa huru Nigeria baada ya kikombozi kulipwa

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,005
9,872
Wanafunzi zaidi waliokua wametekwa kaskazini mwa Nigeria wameachiwa huru baada ya kikombozi kilipwa.

Wafunzi 10 waliachiliwa siku ya Jumapili, kulingana na chama kimoja cha Kikristo katika eneo hilo,11 bado wako mikononi mwa watekaji.

Mkuu wa chama hicho Joseph Hayab, amesema wanashughulikia mpango wa kuhakikisha wanafuzi walisalia wanaachiliwa huru.

Hili ni kundi la nne la wanafunzi kuachiliwa na watekaji. Jumla ya wanafunzi 110 aidha wameachiliwa au wametoroka kufikia sasa.

Wanafunzi 121 kutoka shule ya upili ya Bethel walitekwa Tarehe 5 Julai katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria.
Watekaji nyara watatu walikamatwa na polisi na kuoneshwa hadharani wiki iliyopita.

Utekaji nyara wa shule umekuwa ukiongezeka nchini Nigeria, huku watekaji nyara wakidai mamilioni ya pesa za Nigeria katika malipo ya fidia.

BBC Swahili
 
Back
Top Bottom