wanafunzi wetu wa siku hizi wana nn?

Mtu wa Pwani

JF-Expert Member
Dec 26, 2006
4,184
671
huku tunakoelekea ni wapi? mbona kila uchao wanafunzi wanakuwa mbogo


Serikali yaifunga shule kwa mwaka mmoja



na Joseph Ishengoma



SERIKALI imewarudisha nyumbani wanafunzi wote na kuifunga Shule ya Sekondari ya wavulana Kibiti kwa kipindi cha mwaka mmoja, baada ya wanafunzi kufanya vurugu kubwa na kuharibu miundombinu ya shule hiyo ikiwemo umeme, maji, kuchoma mabweni na kuchoma vitabu vyote vya kiada na ziada vilivyokuwa katika maktaba ya shule hiyo.

Katika vurugu hizo zilizotokea usiku wa kuamkia Aprili 23, mwaka huu, wanafunzi hao walichoma vyakula vyote vilivyokuwa katika stoo ya shule hiyo yakiwemo maharage, sukari na unga.

Uamuzi huo wa kuifunga shule hiyo yenye jumla ya wanafunzi 890 ulitangazwa jana jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Mwantumu Bakari Mahiza.

“Baada ya serikali kukaa chini na kutafakari vurugu hizo, imeamua kuifunga shule hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja, na wanafunzi wote wanatakiwa kuwa wameondoka shuleni hapo ifikapo saa sita mchana wa leo,” alisema Mahiza.

Kwa mujibu wa Naibu Waziri huyo, hatua hiyo ya serikali itatoa mwanya kwa serikali kuifanyia shule hiyo matengenezo yanayohitajika na kufanya tathmini ya kina kuhusu hasara iliyotokea ambayo hadi sasa bado haijajulikana.

Chanzo cha vurugu hizo zilizosababisha pia kutishiwa maisha kwa walimu wa shule hiyo na kupigwa kwa Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Kibiti, ni malalamiko ya wanafunzi kuhusu ufundishaji usioridhisha wa baadhi ya walimu, akiwemo mwalimu wa fizikia, anayefundisha kidato cha tatu, ukosefu wa maji safi na salama kwa muda mrefu na kutokuwepo kwa uhakika wa umeme shuleni hapo.

Hadi jana moto ulikuwa unaendelea kuteketeza majengo ya shule hiyo kutokana na ukosefu wa maji ya kuuzima.

“Yako matatizo ya msingi katika shule zetu na madai ya wanafunzi wa Kibiti yalikuwa ya msingi, lakini walikosa uvumilivu. Matatizo hayo hayakuanza leo, lakini yanatatuliwa kwa njia ya majadiliano, si kuchukua hatua na kuharibu mali za serikali,” alisema Mahiza.

Kufuatia hali hiyo, serikali imeiagiza bodi ya shule hiyo kukutana haraka na kubaini chanzo cha vurugu hizo pamoja na wanafunzi wote waliohusika.

“Watakaobainika kuhusika sheria itachukua mkondo wake na watakaobainika kutohusika katika vurugu hizo, watatawanywa katika shule nyingine,” alifafanua.

Shule hiyo iliyounganishiwa umeme wa jua mwaka jana kutokana na jenereta yake kuharibika, ilihitaji kufanyiwa ukarabati mkubwa uliohitaji zaidi ya sh milioni 170, lakini serikali ilijipanga kuufanya ukarabati huo katika mwaka ujao wa fedha. Kutokana na uharibufu huu gharama hizo zinakadiliwa kuongezeka zaidi.


freemedia/tanzania daima
 
Hii ni shule ya nne katika kipindi kifupi - zingine ni Lyamungo, Chidya, Bagamoyo.

Hii ni dalili ya matatizo yaliyopo katika sekta ya elimu kwa ujumla. Lakini, zaidi ni kwa watoto wa walalahoi - kwani zote hizo ni za serikali (na ziko meant kwa wale wasioweza kwenda kwenye Academies)
 
Back
Top Bottom