chitambikwa
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 3,941
- 900
Jamani tukipigwa lebel wote situtakimbiana
Mungi & MODs ningeomba hii post ibakie hapa ili ijadiliwe na wengi. Ni muhimu sana kwa watu wengi kuona huu unyama unaofanywa huko Kibaha.
Hii ni aibu kwa Taifa zima, na ni kinyume kabisa na haki za binadamu. Lakini linalonisikitisha zaidi ni majibu aliyotoa waziri wa afya kwamba hawezi kusemam chochote mpaka uchunguzi ufanyike! Hivi waziri hajui kwamba hili ni kosa? Na inakuje BBC wawe wa kwanza kujua hii habari ni sio vyombo vyetu vya habari hapa Tanzania?
Hii si sawa! Tumesoma na watoto wenye allergies, asthma, disabilities mbalimbali! Kwani hao watoto wako wangapi hadi walimu wasiwajue? By the way, walimu wanapaswa kuwajua wanafunzi wote wanaohitaji special attention ili wawasaidie! Kama ni kwa ajili ya kuwatambua, ina maana wenye malaria na kuhara wanapewa label?
Isitoshe ukimwi sio ugonjwa jamani! Kwani mtoto mwenye hiv akichota maji atakuwaje? Mbona tuko na watu makazini na wanafanya kazi kama kawa na kusafiri pia? Na hao wazazi wanawafundisha watoto kujinyanyapaa!
Uko sahihi,,well sishangai,,wazee wenyewe wa Pwani! uelewa wao nao mdogo wengi shule teee! haf uvivu ndo asili ya watu wa pwani. Shule za siku hizi hazina kazi sana kama enzi zetu tunalima mashamba,tunasomba matofali,kuni,ambazo ndo kazi ngumu. so wanawakinga na kazi zipi leo hii? Nonsense!
Hujaelewa ulichokisoma, rudia tena kusoma kwa utulivu, kisha ndo ucomment.Hii itasaidia kupunguza maambukizo zaidi manake ni ngumu sana ukamvae mtu mwenye label
Acha longolongo, wengi wa wanaowekewa ni HIV positive. Mwalimu Mkuu amekiri hilo wewe hutaki!What a misconception!! Huo ni upotoshaji.
Hii taratibu si kuhusu HIV. Ni utaratibu upo muda mrefu tangu tunakua wengine. Mi nakumbuka sie primary watu walikuwa wanawekewa label ili wasipewe adhabu ama shughuli ambazo kiafya wameshauriwa wasifanye na madaktari. And it was quite okay.
Mi kwa mfano,nlikua na allergy,yani nkinusa vumbi tu ujue ntaumwa hadi kulazwa.so nikawekewa label kwa hiari ya mzazi wangu na hivyo nkawa sifagii wala kudeki shule hata aje mke wa rais kututembelea.
Kwa hivyo huyo anayesema ni ukimwi anapotosha sababu usually ugonjwa hauwekwi hadharani na ni mwalimu husika tu anayeidhinisha ndo anajua,tena si kwa kuambiwa ugonjwa bali kwa note ya daktari inayoeleza hivyo.