Wanafunzi wengine 1,775 wa mwaka wa kwanza wapata mikopo

HOMBOY

JF-Expert Member
May 16, 2016
1,432
924
WANAFUNZI WENGINE 1,775 WA MWAKA WA KWANZA WAPATA MIKOPO
Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) leo imetangaza orodha ya Awamu ya Nne yenye wanafunzi 1,775 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 31,353. Katika Awamu ya Kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo, Awamu ya Pili (11,481) na Awamu ya Tatu (7,901).

Orodha hiyo ya Awamu ya Nne inapatikana hapa. Aidha, orodha hii inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz) na imeshatumwa kwa vyuo husika ili kuwawezesha wanafunzi kufanya usajili na kuendelea na masomo.

Kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na kati ya fedha hizo shilingi 108.8 bilioni ni kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Tayari Serikali imeshatoa shilingi 147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.
 
Majina elfu moja.!!??? Hivi bodi manatuchukulia poa ee!!
 
Majina elfu moja.!!??? Hivi bodi manatuchukulia poa ee!!
ahahhaaaa watakuambia lengo letu ilikuwa elfu 30 tu kwa mwaka wa kwanza hivyo serikali ya raisi wa wanyonge imewahurumia watoto wakimasikini 1,353
 
Jamani mbona loan breakdown sijaelewa hakuna vya tuition fees wala meal and accommodation au bado wanapakia mambo ...mungu asante nilikuwa nisha kataa tamaa vbaya
 
Wengine tunaendelea na vilio vyetu tu. Naona TSSF inatuita vinginevyo chuo bye bye.
 
Jamani mbona loan breakdown sijaelewa hakuna vya tuition fees wala meal and accommodation au bado wanapakia mambo ...mungu asante nilikuwa nisha kataa tamaa vbaya
Hahahahaha hadi Mimi ila now namshukur mungu nimepata lord have mercy.....
 
IMG_20171112_175044_614.jpg

Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jana imetangaza orodha ya Awamu ya Nne yenye wanafunzi 1,775 wa Mwaka wa Kwanza waliofanikiwa kupata mikopo na hivyo kufanya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa kufikia 31,353. Katika Awamu ya Kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo, Awamu ya Pili (11,481) na Awamu ya Tatu (7,901).
Orodha hiyo ya Awamu ya Nne inapatikana HAPA==> BOFYA HAYA MANENO KUONA MAJINA

Aidha, orodha hii inapatikana katika tovuti ya Bodi (www.heslb.go.tz) na imeshatumwa kwa vyuo husika ili kuwawezesha wanafunzi kufanya usajili na kuendelea na masomo.
Kiasi cha shilingi 427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/2018 na kati ya fedha hizo shilingi 108.8 bilioni ni kwa ajili ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza. Tayari Serikali imeshatoa shilingi 147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/2018.
 
Hivi means tested kwenye mikopo bado inatumika au mwaka huu wameifuta?
 
Kuna dogo alikuwa analalamika wamempa 97,000/= katika ada ya 1,200,000/= sijui huu nao ni mkopo au nauli ya daladala

Inategemeana na taarifa alizojaza kwenye form zake za maombi.

Japo pia inaweza ikawa ni makosa ya kibinadamu hasa " typing error "

Kwa hesabu za harakaharaka inaonekana alipewa mkopo wa asilimia themanini (80%) yaani 80/100×1.2m = 960,000/= hivyo inawezekana kabisa ni human typing error.

Hapaswi kulialia mitaani na vijiweni anatakiwa kuwasiliana na board au aende kabisa ofisi za board atapata ufafanuzi.
 
Back
Top Bottom