Wanafunzi wengi jijini Dar wanaosoma mbali na wanapoishi wanateseka sana. Tunawezaje kuwasaidia?

mr vata

JF-Expert Member
Jan 30, 2017
465
616
Hili suala linawahusu sana Wanafunzi wa shule za msingi na kama tujuavyo siku hizi Mwanafunzi wa kiwango hiki cha elimu anakua na umri mdogo sana hasa akiwa madarasa ya chini...

Unatoka kazini jioni na kukutana na watoto wengi wakiwa wanagombania usafiri, kitu ambacho ni hatari kutokana na umri wao. Kama hilo la kugombania usafiri halitoshi pia wanakutana na kadhia ya foleni...

Mtoto anaishi Gongolamboto lakini anasoma sinza. Mtoto huyu anachelewa kurudi nyumbani na akirudi anakua amechoka sana, anajisomea saa ngapi?

Hivi haiwezekani kuweka utaratibu wa kusoma maeneo wanaoishi hasa kwa hawa wa shule za msingi?

Tuwaangalie watoto hawa.
 
Acha wajifunze maisha, Wakomae ... ANKO MAGUGU hafugi mayai

Ukiona hafai kupitia hayo yote IST na ISM ziko wazi nahic hazjajaa
 
Hilo suala huwa linanisononesha sana.

Yaani unaweza ukaona katoto kadogo kweli halafu kako peke yake tu kanasubiri kupanda daladala.

Hii jamii yetu ina dosari nyingi mno kwa kweli.

Mimi siwezi kabisa kumwacha mtoto wangu ahangaike na madaladala peke yake.
 
Yani inasikitisha sn. Mtu unaamka saa kumi up najiona umewahi, ukifika kituoni unakutana na kitoto alafu baadhi ya daladala huwakataa. Mi sidhani km ni busara mtoto kumuacha asome mbali aise.
 
Tatizo ni nyumba zenu za kupanga.

Mnahamahama sana January upo Tegeta, Mwezi march umehamia Mbagara August upo Sinza.

Kwa jinsi mnavyohamahama mnawatesa watoto wenu
 
Nimependa Utaratibu walioutumia shule ya Msingi Mlimani (Udsm).Baada ya shule yao kutofanya vizuri Kwa muda mrefu wameamua kuja na mikakati mipya na kuifanya kuwa miongoni mwa shule Bora.Kwanza wameijenga upya.Pili hawasajiri mwanafunzi yeyote anayetoka mbali.Hata anayetoka Kimara au Makongo juu hawamkubali.
Tatu,madarasa yao ni standard na idadi ya wanafunzi Kwa Kila Darasa ni wanafunzi 45 tu ( Hawatazidi hapo).
Miaka ya karibuni shule hii itafanya vizuri kushinda shule nyingi za binafsi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
IMG_20190103_105822.jpg
IMG_20190103_105707.jpg

Shule ya Msingi Mlimani (Udsm)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hili suala linawahusu sana wanafunzi wa shule za msingi, na kama tujuavyo siku hizi mwanafunzi wa kiwango hiki cha elimu anakua na umri mdogo sana hasa akiwa madarasa ya chini...
Unatoka kazini jioni na kukutana na watoto wengi wakiwa wanagombania usafiri, kitu ambacho ni hatari kutokana na umri wao. Kama hilo la kugombania usafiri halitoshi pia wanakutana na kadhia ya foleni...
Mtoto anaishi gongolamboto lkn anasoma sinza. Mtoto huyu anachelewa kurudi nyumbani na akirudi anakua amechoka sana, anajisomea saa ngapi?
Hivi haiwezekani kuweka utaratibu wa kusoma maeneo wanaoishi hasa kwa hawa wa shule za msingi?
Tuwaangalie watoto hawa.
Hilo tatizo kwa dsm ni kubwa,bahati mbaya wanafunzi wa msingi hubeba madtari yote kila siku,umbali ukiongeza lundo la madfari mateso matupu,hapa wazazi wenyewe chanzo cha yote,wazazi wengi wapo bize na majukumu mengine hawana muda wa kubaini,nakushukuru kwa mtoa uzi angalau umeliona hili.
 
Nadhani tatizo linatokana na maeneo yenye wakazi wengi kutokuwa na shule nyingi.Sasa hivi ukienda pembezoni mwa mji makazi ya watu yanakuwa Kwa Kasi lakini huoni maeneo ya shule yakitengwa.Baada ya muda unakuja kuta Eneo limeshakuwa na wakazi wengi lkn shule hazipo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo suala huwa linanisononesha sana.

Yaani unaweza ukaona katoto kadogo kweli halafu kako peke yake tu kanasubiri kupanda daladala.

Hii jamii yetu ina dosari nyingi mno kwa kweli.

Mimi siwezi kabisa kumwacha mtoto wangu ahangaike na madaladala peke yake.
Sijui wazazi wanajisikiaje,upo zako kwenye mishe zako halafu unamuacha mtoto mdogo aende umbali mrefu hivyo tena apambane kwenye daladala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MUHIMU Ni kuangalia usalama wao ilo la umbali siyo tija.

Jambo lingine, hata hizo shule wakisema waandikishe watoto wa jirani na shule hiyo hawawezi kutosheleza hata madarasa mawili.
 
MUHIMU Ni kuangalia usalama wao ilo la umbali siyo tija.

Jambo lingine, hata hizo shule wakisema waandikishe watoto wa jirani na shule hiyo hawawezi kutosheleza hata madarasa mawili.
Yap kitu cha kwanza ni Usalama.Lakini hata umbali ni tatizo kubwa.Kuna mtoto alikuwa anaishi na wazazi wake Kivule na alikuwa anasoma Kivule (Kitunda Kwa mbele).Wazazi wake wakatengana ikabidi mtoto akaishi Kwa Mzazi mmoja Mbezi Tangi Bovu.Just Imagine hii route ya Kivule to Tangi bovu tena Kwa daladala ni mateso makubwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom