Wanafunzi 2 Juma Ahmed (9) na Ayoub Ahmed (12) wa shule ya msingi Shangazi iliyopo Tarafa ya Mlalo wilayani Lushoto wamefariki dunia kwa madai ya kula Muhogo unaodaiwa kuwa na sumu.
Akielezea tukio hilo Kamanda wa Polisi mkoani Tanga Kamishna Msaidizi wa Polisi Leonard Paul amesema siku ya tukio mama wa watoto hao Ashura Mohamed alikwenda shambani kwake yeye na watoto wake wanne kuchimba mihogo huku baadhi ya watoto wake wakianza kuila ikiwa mibichi na walipofika nyumbani mama aliichemsha mihogo hiyo na kuanza kuila ikiwa ni mlo wa mchana.
Amesema ilipofika nyakati za jioni mama alipika tena chakula aina ya ugali na dagaa kisha kula mlo wa jioni na watoto wake,lakini ilipofika nyakati za usiku wa manane watoto walianza kulalamikia kuumwa na tumbo ndipo walipowahishwa hospitali na kulazwa kisha baadae walifariki watoto wawili kati ya wanne.
katika hatua nyingine Kamanda Paul amewataka wamiliki wa silaha kwenda katika vituo vya Polisi kwa ajili ya ukaguzi ikiwa ni sehemu ya zoezi la kukabiliana na vitendo vya ujambazi kufuatia kukamata silaha ya kivita aina ya Shot Gun iliyokuwa imehifadhiwa na mtuhumiwa mmoja ambaye hivi sasa anashikiliwa na jeshi la Polisi.