Wanafunzi watano wa shule nyingine walipewa lifti katika basi la shule lililopata ajali Mtwara

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,458
GARI ya Shule ya King David lililopata ajali jana eneo la Mjimwema, manispaa ya Mtwara Mikindani, mkoani Mtwara na kuua watu 13, lilikuwa pia likiwapa lifti wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mikindani.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Shule ya Mikindani, Jacob Godfrey, aliyeeleza kuwa katika ajali hiyo kulikuwa na wanafunzi wa shule yake watano ambao walijeruhiwa na walipewa lifti na dereva wa gari hilo aitwaye Hassan, ambaye ni miongoni mwa waliofariki.

"Wanafunzi wetu walikuwa watano kwenye gari hilo na wote ni wa kike, wote ni majeruhi," amesema na kuongeza kuwa wanafunzi hao ni miongoni mwa majeruhi 15, ambao walipelekwa hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara, Ligula.

Amesema mwanafunzi mmoja kati ya hao watano amepewa rufaa kwende Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dar es Salaam na wengine wawili wanapelekwa hospital ya Rufaa, Ndanda.

Jacob amesema baadhi ya wanafunzi wake wamekuwa wakiomba lifti kwa dereva wa gari hilo au magari ya watu binafsi kwa ajili ya kuwasaidia kufika shuleni haraka.

"Kutokana na changamoto za usafiri wanafunzi wetu wanakuwa njia rahisi ya kupata usafiri na ikitokea gari kama hilo huwa wanaomba na kupewa lifti na wamekuwa wakipewa," amesema.

Wanafunzi hao watano walikuwa kwenye gari la shule ya Msingi ya King David, ambayo ilipata ajali jana eneo la Mjimwema baada ya kukatika breki, ikiwa kwenye mteremko na kuanguka kwenye mtaro na watu 13, wakiwemo wanafunzi 11 walifariki na wengine 15 kujeruhiwa.
 
Key word, Wanafunzi wote watano walipoe2a Lift na Marehemu Hassan walikuwa ni WA Kike
 
Back
Top Bottom