Wanafunzi wasistishwa kufanya mitihani ya mwisho wa mwaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wasistishwa kufanya mitihani ya mwisho wa mwaka

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by kcmc students, Aug 9, 2011.

 1. k

  kcmc students New Member

  #1
  Aug 9, 2011
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  [h=2][/h]
  Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Tiba kishiriki cha Tumaini (KCMC) wamekuwa katika kipindi kigumu cha masomo yao, hasa wakati huu wanapokaribia kufanya mitihani kutokana na kushindwa kumaliza kiasi kikubwa cha fedha kama sehemu ya ada.
  Kwa kipindi kirefu Serikali imekuwa mstari wa mbele katika kuongeza idadi ya madaktari ili kupunguza ule uhaba wa usawa wa daktari mmoja kwa wagonjwa 50,000 wanaomtegemea kuhudumia katika jamii.

  Pamoja na kuwa Serikali imekuwa na tija katika kutimiza hii dhamira lakini kuna kundi kubwa la watu/Wakuu wa vyuo waliohodhi Nafasi hizo kwa maslahi yao binafsi na kupelekea kudidimia kwa nia njema ya serikali ya jamuhuri ya watu walalahoi wa Tanzania.

  Wanafunzi wamekuwa ni wa kusumbuliwa na kuwekewa mikingamo juu ya chochote wanachodadisi ilihali yakiwahusu wao na kuishia kuambiwa ni siri na hawatakiwi kujua na wanaposimamia kujua kwa nguvu basi chuo hichi huchukua mabavu ya kuwatishia kuwafukuza chuo,bila kuangalia uzito wa hoja na maslahi ya wanafunzi wategemewao kuhudumia Jamii hiyo kesho.

  Yanayojiri hapa KCMC.

  • Chuo hiki kipo chini ya bodi inayoongozwa na askofu Martin shao,ambaye amekuwa mstari wa mbele kushirikiano bege kwa bega na mkuu wa chuo hiki (Provost) Prof.Egbert Kessi katika kuwanyanyasa na kuwatesa wanafunzi.
  Waheshimiwa hawa kwa sasa wamefananishwa na nduli wasiojali watanzania wenzao na hata ile dhamira ya ukristo kwenye vitabu vitakatifu {Biblia}.wamekuwa Waonevu wasio na upendowala hekima na wasiopenda kusikiliza ,kurekebishwa na kuendelea na kufuja pesa za Kanisa na wizara(Serikali) na wahisani mbali mbali.
  • Serikali imekuwa ikitoa udhamini kwa wanafunzi kupitia bodi ya mikopo kwa asilimia 100% na wale wa udhamini wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi (WEMU).Chuo hiki ni moja ya kati ya vyuo vya binafsi vinavyoongeza ada bila kujali madhara yanayoweza kuwakabili wanafunzi na kipato cha wazazi wao ambao ni wakulima wenye kipato cha chini.

  • Kuanzia Mwaka 2008/2011 chuo kimeshaongeza ada mara tatu ndani ya kipindi cha muda mfupi kitu ambacho hakikubaliwi kisheria na kinaonesha misingi mibovu ya uongozi ya chuo na kutokuwa na Dira katika Mipango yake.
  Hali hii imepelekea wanafunzi kuamuriwa na chuo kulipa kwa Nguvu ada bila ya wadhamini wao ambao ni bodi ya mikopo(Wizara ya Sayansi na elimu ya Juu) na Wizara ya Elimu na mafunzo ya ufundi(WEMU),kufahamishwa na kutoa maamuzi.

  Pamoja na Serikali kutoa agizo kupitia bodi ya mikopo mapema mwaka juzi mwezi wa pili kuonya tasisi za elimu za juu kutoongeza mpaka TCU itakapofanikisha mchakato rasimu utakaokuwa mwongozo rejea kwa kila chuo.

  Pia mnapo tarehe 26 julai 2009 wakuu wa chuo walipewa maagizo ya kutoongeza gharama kwa wanafunzi waliopo chini ya wizara ya elimu ya na mafunzo ya ufundi(WEMU).

  Maelekezo hayo yamekuwa ni bure na kutofutwa kitu ambacho kinatishia Uadilifu na Utekelezwaji wa Maagizo ya serikali kuu na Taasisi hizi za mashirika ya Dini (KKKT).
  • Wanafunzi hawa ni watu wa kati tu baina ya mfadhili na Chuo ,Wanapohojiwa uhalali wa wao kuongezea ada bila ya wizara husika kuafahamishwa,wamekuwa kupewa kauli za kejeli na masikhara na mkuu huyu wa chuo,mfano:nyie ni masikini na mnajua chuo ni ghali mnategemea nani awalipie,na wakati wengine akisema serikali yenu haina pesa,wakati mwingine huhoji hadi mavazi yetu ni chakavu na ya kimasikini (Duni) hatustahili kuongea naye.
  • Katika hali ya kumnyenyekea tumekuwa tukimwomba mara nyingi apitishe barua zetu zipate Baraka za chuo kwenda kwa wadhamini na amediriki kutuambia hawezi kufanya hivyo na hawezi kufundishwa kazi na sisi,yeye yupo ofisini kutumikia Bodi ya menejimenti ya chuo na si wanafunzi.Hivyo wanafunzi hawa wamekuwa katika wakati mgumu Juu ya Muamala wa Maisha yao kielimu.
  • Wanafunzi wamekuwa wakiambiwa kiasi wanachodaiwa bila ya kupewa written notification na vile vile wanafunzi waliopo chini ya wizara ya elimu na mafunzo wamekuwa wakisoma mpaka kumaliza chuo bila kupewa risiti ya kiasi walicholipiwa kitu amacho mkataba wa serikali umeagiza chuo kumpatia mwanafunzi annual statement.
  • Chuo hiki kimekuwa ni cha kisanii zaidi na kutokutoa huduma ambayo serikali na umma ikitegemea,kwani kimekuwa na wakufunzi waajiriwa wachache na wasionekanana kwenye vipindi na wengi wakiwa ni wanafunzi wa uzamili( master's degree programme) wakilazimishwa kufundisha chuoni na kulipwa 5,000 kwa kipindi,na kimekuwa mstari wa mbele kuajiri watu wengi kada za kubeba mafaili na kupeleka chai maofisi ambao nao hulipwa kiasi kidogo cha ujira 150,000/=,
  • Utegemezi wa chuo kwa madaktari waliopo hospitalini kuja kufundisha chuoni kimekuwa cha kutotabirika kwani si sawa kuacha wagonjwa na kuja kufundisha na pia uhaba wa nguvu kazi ya hospitali ni kubwa na ukipitia Prospectus mpya ya chuo utaona majina mengi za maprofesa ambao hawapao na wengine hawajulikani hata kwa wanafunzi wa idara husika(usanii).

  • Pia kumekuwa na udanganyifu kwa tasisi za kifedha kama HELBS na WEMU juu ya mafunzo wapatiwayo wanafunzi katika maeneyo yajumuishayo safari za mafunzo vijijini na pia pesa za kiada na ziada kwa mwanafunzi.

  • Chuo kimekuwa kikijipatia pesa ndani ya vipengele hivyo bila ya mwanafunzi kutumikia ilihali wanafunzi wamekuwa wakienda field mwaka wa tatu na Nne ila chuo inapokea fedha hizo tokea mwaka wa kwanza mpaka wa Tano.

  • Fedha za wanafunzi maalumu chini ya WEMU zimekuwa zikitumwa nyingi kuliko kiasi mwanafunzi anachoambiwa na baada ya kupitiwa na idara ya fedha hapa chuoni kuponekana kuna ubadhirifu mkubwa,kitu ambacho mkuu huyu wa chuo akiulizwa husema hataki kujibu nay eye hayupo chuoni kujibu maswala ya wanafunzi isipokuwa anatumikia bodi ya menejimenti ya chuo ambayo yeye ni katibu mkuu.

  • Pia kumekuwa na harufu ubadhirifu pamoja na ushirikianaji wa karibu na coordinator wa wizara kwa hapa chuoni aitwaye Bwana Rajabu Abdullah ambaye ni mjumbe katika bodi na mwakilishi wa vyuo kutokea wizarani.

  • Wanafunzi wa Udaktari wa vyuo vya Tiba Dar es salaam HKMU na IMTU wamekuwa wakilipiwa 3.6M na hapa Chuoni 3.245M,na ukipitia nyaraka za malipo katika mtirirko wa mahesabu utakuta kuna zaidi ya milioni kumi kwa kila darasa ambazo hazionekani zimetumikaje,na endapo zingegawanywa kwa wanafunzi hao zingetosha.kitu ambacho kinaonesha wizara imepotoshwa na mkuu huyu na bwana Rajabu na kufuja Fedha za serikali.

  • Wahisani wengi wamekuwa wakikitembela chuo na kutoa misaada mingi kifedha na kitaaluma lakini chuo imekuwa ikatufa misaada hiyo bila kumfikia mfaidikaji(mwanafunzi muhitaji),hakuna mpaka sasa ajuaye wakati nani na vipi hizo fedha zinatumika.

  • Mpaka sasa ni mwaka wa saba kwa chuo hiki kukaa bila ya kufanyiwa auditing,kutokana na malengo binafsi ya walaji. Kitu ambacho ni hatari kwa taasisi yeyote inayopokea fedha za serikali na wahisani.
  • Tunaomba Waziri wa Elimu na Mafunzo Ya Ufundi Mh.Kawambwa asikie kilio chetu na kuvalia njuga swala hili kuu lenye maslahi ya watumishi watarajiwa wa nchi yetu, na ikiwezekana waajibishwe wahusika
   
 2. Salanga

  Salanga JF-Expert Member

  #2
  Aug 10, 2011
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 375
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hizi ni tuhuma ambazo CDM wanatakiwa wavalie nyuga
   
 3. Perry

  Perry JF-Expert Member

  #3
  Aug 10, 2011
  Joined: Feb 24, 2011
  Messages: 10,028
  Likes Received: 853
  Trophy Points: 280
  Dah!poleni sana wakuu!!
   
Loading...