Wanafunzi wasiotoa michango kufukuzwa ni hujuma kwa Serikali?

Sumba-Wanga

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
5,349
1,226
Wanajamvi,

Nimekutana na kitendo ambacho kimenifanya nijiulize kwma zana na serikali ya awamu ya Tano ya Elimu bure msingi na sekondari ni ya kweli. Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Mbabala, iliyopo katoka Manispaa ya Dodoma, Bwana Gaitani Mwatenga amewafukuza wanafunzi ambao hawajalipa michango, na wale waliolipa michango amewabakiza shule.

Kwa madai yake, elimu bure ni kwenye ada peke yake, na sio kwenye michango ya wanafunzi wanaokaa hostel ambayo inafikia Tshs 500,000. Nimejiuliza, hivi hili ndio agizo la serikali? Kwani sekondari haipeleki pesa za wanafunzi wanaokaa Hostel kwa shule kama Mzumbe, Bihawana na Msalato? Kama ni kweli, kumbe slogan ya ELIMU BURE ni kiini macho?

Nimeenda mbali hadi kujiuliza kama Municipal Director is aware of all these!

Naomba msaada wa kuelimishwa zaidi. Pia, naomba kama kwenye jamvi hili kuna namba za Prof Ndalichako na Mheshimiwa Simbachawene ili tuongee nao na kupata ufumbuzi zaidi.

Nina wasi wasi kwamba watu kama bwana Mwatenga wanatumiwa ili kumhujumua JPM.
 
Kwahiyo unamchomea mkuu wa shule. Nadhani ungefatilia kwanza je hela zimepelekwa hapo shuleni? Na kama hazijapelekwa wanafunzi wanakula nini asipowafukuza?
 
Ipo hizi serikali imefanya mchanganuo wakutosha kuhusiana na gharama za kila shule na kila mtoto,awe anakaaa bweni au day.Ada,michango na gharama zote zinazomuhusu mwanafunzi serikali inagharimia mfano Ada,Michango ya Madawati,karatasi,Hostel nk zote hizo serikali inagharamia.Kwahiyo kama kuna hizo gharama hapo shuleni na watoto wanadaiwa basi hilo litakua jipu linalohitaji kupasuliwa haraka iwezekanavyo.Pia kuna gharama zinazomuhusu mzazi au mlezi moja kwa moja kama Daftari ,vyatu,sale , nauli kwa wale wa day pamoja na kuhakikisha mtoto anapata chakula kwa wale wa day.
 
Mkuu basikia tetesi kuwa pesa azitoshi na wanafunzi ni wengi so najiuliza kweli hii dhana itafanikiwa
 
Kama pesa hazitoshi basi hiyo in Kesi nyingine,na mzigo wasibebeshwa walezi au wazazi.
 
Pesa inatosha kama haita pigwa,cha msingi wakuu washule inatakiwa wazoee na hii hali.
 
Kuna mwalimu amesema wana wanafunzi 500 wamepewa 500000 kweli unaona hizo pesa zinaweza fanya nn labda watakuja na majibu hpa
 
Wanajamvi,

Nimekutana na kitendo ambacho kimenifanya nijiulize kwma zana na serikali ya awamu ya Tano ya Elimu bure msingi na sekondari ni ya kweli. Mwalimu Mkuu wa Shule ya sekondari ya Mbabala, iliyopo katoka Manispaa ya Dodoma, Bwana Gaitani Mwatenga amewafukuza wanafunzi ambao hawajalipa michango, na wale waliolipa michango amewabakiza shule.

Kwa madai yake, elimu bure ni kwenye ada peke yake, na sio kwenye michango ya wanafunzi wanaokaa hostel ambayo inafikia Tshs 500,000. Nimejiuliza, hivi hili ndio agizo la serikali? Kwani sekondari haipeleki pesa za wanafunzi wanaokaa Hostel kwa shule kama Mzumbe, Bihawana na Msalato? Kama ni kweli, kumbe slogan ya ELIMU BURE ni kiini macho?

Nimeenda mbali hadi kujiuliza kama Municipal Director is aware of all these!

Naomba msaada wa kuelimishwa zaidi. Pia, naomba kama kwenye jamvi hili kuna namba za Prof Ndalichako na Mheshimiwa Simbachawene ili tuongee nao na kupata ufumbuzi zaidi.

Nina wasi wasi kwamba watu kama bwana Mwatenga wanatumiwa ili kumhujumua JPM.
Hostel na boarding ni tofauti, Mzumbe na msalato ni boarding schools zinalipiwa na serikali hostel ni mpango wa shule husika na mzazi lazima walipe michango ya chakula na kulala. Ukiangalia utaona hostel wanalipa ada sawa na wale wa kutwa , lakini boarding wanalipa ada tofauti. Hostel zipo kuwasaidia watoto wa eneo huska wanaokaa mbali na shule katika mmji mmoja. lakini boarding wanachukuliwa hata kutoka mikoa mingine au wilalaya za mbali. Fuatilia hiyo shule ni day school au boarding school?
 
Asante sana kwa taarifa, nitafuatilia.

Kwa maana hiyo, kama ni kitu tiofauti, kwa nini wanafunzi wanadaiwa pay in slip za malipo ya Hostel?
Hiyo pesa inakwenda wapi?

Hostel na boarding ni tofauti, Mzumbe na msalato ni boarding schools zinalipiwa na serikali hostel ni mpango wa shule husika na mzazi lazima walipe michango ya chakula na kulala. Ukiangalia utaona hostel wanalipa ada sawa na wale wa kutwa , lakini boarding wanalipa ada tofauti. Hostel zipo kuwasaidia watoto wa eneo huska wanaokaa mbali na shule katika mmji mmoja. lakini boarding wanachukuliwa hata kutoka mikoa mingine au wilalaya za mbali. Fuatilia hiyo shule ni day school au boarding school?
 
Kwahiyo unamchomea mkuu wa shule. Nadhani ungefatilia kwanza je hela zimepelekwa hapo shuleni? Na kama hazijapelekwa wanafunzi wanakula nini asipowafukuza?

Kwani kuna haja ya kusema kwamba namchongea? yeye hadi afanye hivyo si anajiamini?
How come wanafunzi wanadaiwa pay in slip kwa malipo hayo?
Mbona haya yote hatukuambiwa na serikali?
maelezo haya ameyapata wapi?
 
Ipo hizi serikali imefanya mchanganuo wakutosha kuhusiana na gharama za kila shule na kila mtoto,awe anakaaa bweni au day.Ada,michango na gharama zote zinazomuhusu mwanafunzi serikali inagharimia mfano Ada,Michango ya Madawati,karatasi,Hostel nk zote hizo serikali inagharamia.Kwahiyo kama kuna hizo gharama hapo shuleni na watoto wanadaiwa basi hilo litakua jipu linalohitaji kupasuliwa haraka iwezekanavyo.Pia kuna gharama zinazomuhusu mzazi au mlezi moja kwa moja kama Daftari ,vyatu,sale , nauli kwa wale wa day pamoja na kuhakikisha mtoto anapata chakula kwa wale wa day.

Kweli hili ni jipu na leo ndio mwisho wake.
Kama alikuwa anangangania awamu ya 4 basi ngoja prof Ndalichako ampasue jipu
 
Ipo hizi serikali imefanya mchanganuo wakutosha kuhusiana na gharama za kila shule na kila mtoto,awe anakaaa bweni au day.Ada,michango na gharama zote zinazomuhusu mwanafunzi serikali inagharimia mfano Ada,Michango ya Madawati,karatasi,Hostel nk zote hizo serikali inagharamia.Kwahiyo kama kuna hizo gharama hapo shuleni na watoto wanadaiwa basi hilo litakua jipu linalohitaji kupasuliwa haraka iwezekanavyo.Pia kuna gharama zinazomuhusu mzazi au mlezi moja kwa moja kama Daftari ,vyatu,sale , nauli kwa wale wa day pamoja na kuhakikisha mtoto anapata chakula kwa wale wa day.

Kweli hili ni jipu na leo ndio mwisho wake.
Kama alikuwa anangangania awamu ya 4 basi ngoja Prof Ndalichako na Sembachawene wampasue jipu
 
Kwani kuna haja ya kusema kwamba namchongea? yeye hadi afanye hivyo si anajiamini?
How come wanafunzi wanadaiwa pay in slip kwa malipo hayo?
Mbona haya yote hatukuambiwa na serikali?
maelezo haya ameyapata wapi?
Hapo Hostel kuishi ni HIARI Au ni LAZIMA???????????????Na kama ni LAZIMA Hiyo shule inafahamika serikalini kama SHULE Ya BWENI au DAY?????????????Maana inaweza kuwa shule ni DAY na mambo ya HOSTELI ni biashara zenu binafsi halafu mnakuja KULAUMU SERIKALI.
 
Mkuu basikia tetesi kuwa pesa azitoshi na wanafunzi ni wengi so najiuliza kweli hii dhana itafanikiwa

Inawezekana ni kweli. Kama pesa hazitoshi si watoe taarifa? Inakuwaje wao nao wanakuwa na serikali yao?
Hawa wakuuu wa sekondari ni majipu yaliyoshindikana.
Huu sasa ndio mwisho wao
 
Hapo Hostel kuishi ni HIARI Au ni LAZIMA???????????????Na kama ni LAZIMA Hiyo shule inafahamika serikalini kama SHULE Ya BWENI au DAY?????????????Maana inaweza kuwa shule ni DAY na mambo ya HOSTELI ni biashara zenu binafsi halafu mnakuja KULAUMU SERIKALI.

Mkuu Maswali hayo yote atayajibu Prof Ndalichako au Afisa elimu wa Manispaa ya Dodoma.
 
Back
Top Bottom