Wanafunzi Wasagana Mabwenini, Shule Yafungwa

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,720
21,779
Wanafunzi Wasagana Mabwenini, Shule Yafungwa


Monday, March 01, 2010 3:08 AM
Shule moja ya wasichana nchini Afrika Kusini imeyafunga mabweni yake na kuwalazimisha wanafunzi wote waondoke baada ya wanafunzi 27 wa shule hiyo kugundulika wanaendeleza tabia ya usagaji shuleni hapo.
Maafisa wa elimu wa nchini Afrika Kusini wanafanyia uchunguzi ripoti ya kufungwa kwa mabweni ya shule ya sekondari ya wasichana kutokana na tabia ya wanafunzi wa kike kusagana.

Wanafunzi wawili wa kike walikamatwa wakibusiana na wanafunzi wengine kadhaa inasemekana wako kwenye mahusiano ya jinsia moja.

Jumla ya wanafunzi 27 wamefukuzwa shule kutokana na tabia hiyo ya usagaji.

Watetezi wa haki za binadamu nchini Afrika Kusini wamekuja juu wakipinga uamuzi wa shule hiyo kwakuwa mahusiano ya jinsia moja yanaruhusiwa kisheria nchini Afrika Kusini.

Afrika Kusini ndio nchi pekee barani Afrika iliyoruhusu wasagaji na mashoga kujitawala kama katika nchi za barani ulaya na Amerika.

Wanafunzi waliofukuzwa shule katika shule hiyo iliyopo KwaZulu-Natal hawakutajwa majina yao kwa vyombo vya habari na jina la shule hiyo nalo liliwekwa kapuni.

Gazeti la The Star la nchini humo lilisema kwamba wanafunzi ambao walishindwa kurudi majumbani mwao walipewa hifadhi kwenye nyumba zilizo karibu na shule hiyo.

Msemaji wa kitengo cha elimu cha Afrika Kusini, Sihle Mlotshwa alinukuliwa na gazeti hilo pia akisema kuwa shule hiyo haina haki ya kuwafukuza au kuwasimamisha shule wanafunzi kwasababu ya masuala yao ya kijinsia.
 
kuwa na shule ya wasichana watupu ndo madhara yake...
wangekuwa na wavulana,wangejifaidia mihogo ya jang'ombe.
sasa wavulana hakuna wafanyaje??????
 
kuwa na shule ya wasichana watupu ndo madhara yake...
wangekuwa na wavulana,wangejifaidia mihogo ya jang'ombe.
sasa wavulana hakuna wafanyaje??????

dawa ni kuileta mijianaume mitupu sijui nayo ingeleta kasheshe??
 
Binadamu sasa tunakuwa viumbe wa ajabu kuliko hata wanyama, maana sijaona Beberu likimega beberu mwenzie hata siku moja
 
Binadamu sasa tunakuwa viumbe wa ajabu kuliko hata wanyama, maana sijaona Beberu likimega beberu mwenzie hata siku moja

Uliza uambiwe, kuna beberu moja lilikuwa linajua kazi ni kumega tu! lilimega jike mpaka akafa halafu likawa linamega hata vidume wenzake. We acha dunia tambara bovu!
 
Binafsi sikubaliani kabisa na hizi shule za jinsia moja. Iwe ya dei au ya bweni. Ni sawa na kufuga nyoka mwenye sumu ktk chumba unacholala.
 
Hizo ni rasha rasha tu, kama hatua mathubuti hazitachukuliwa na Zuma kutengua sheria hiyo, itafikia mpaka majumbani mwao mada kusagana. Tuombe neema zake tu zitunusuru na haya yote.
 
Haya ndiyo matokeo ya maendeleo ya science and technology. Vyakula watoto wanakula siku hizi and the like. Mbona zamani wengi wetu tulisoma shule za wasichana/wavulana pekee na co-education zilikuwa chache (nikizungumzia wakati wa public schools and a very few private). Huko kulikuwa hakuna usagaji wala ushoga (kama ulikuwepo ni maajabu mno) . Ninachofahamu mambo yakiwa magumu, sabuni ilikuwa inatake charge!! Kwa wanawake sina ujuzi sana. Hata zile za Co-education masuala ya zinaa shuleni ilikuwa ni marufuku na nidahmu ilikuwapo. Mabinti walikuwa wanamaliza shule hadi high level na vyuo virgin!!! Leo hii primary school wengine hawana kitu kabisa, kwisha!!! Tafadhali usije ukaenda kuchukua torch leo usiku ukammulike yule binti yako under 15 years akiwa usingizini. Utaweza kupayuka kilio usiku!!! usije kunilaumu!!!

Je sasa, kama watu wazima hapa over 18 years tunaojadili hapa. Je hayo ndiyo maendeleo au ni nini? Unapofikiria kufanya ngono na mtoto wa umri wa mtoto wako, au mdogo wako ambaye unajua fika ni mdogo anasoma, tena primary school and secondary (at 16-18 watoto wako form six) unaonaje kama angekuwa ni mtoto wako au ni ndugu yako? Halafu wakati mwingine unataka umuingilie kinyume na maumbile?? Je angekuwa wa kwako ungefanya hivyo?? Dhambi hii itakunyemelea wewe na kizazi chako, hadi cha nne!! Halafu mnaanza kulalamika, ohh mwanangu/mjukuu/kitukuu/kilembwe/kilembwekeze kawa shoga/msagaji/malaya/mzinzi/ etc wakati alirithi madhambi yako. Tutubu na Tumrudie Mungu vinginevyo Sodoma na Gomora nyingine yaja!
 
Back
Top Bottom