Wanafunzi Wasagana Mabwenini, Shule Yafungwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi Wasagana Mabwenini, Shule Yafungwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 1, 2010.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 1, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,005
  Likes Received: 6,823
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi Wasagana Mabwenini, Shule Yafungwa


  Monday, March 01, 2010 3:08 AM
  Shule moja ya wasichana nchini Afrika Kusini imeyafunga mabweni yake na kuwalazimisha wanafunzi wote waondoke baada ya wanafunzi 27 wa shule hiyo kugundulika wanaendeleza tabia ya usagaji shuleni hapo.
  Maafisa wa elimu wa nchini Afrika Kusini wanafanyia uchunguzi ripoti ya kufungwa kwa mabweni ya shule ya sekondari ya wasichana kutokana na tabia ya wanafunzi wa kike kusagana.

  Wanafunzi wawili wa kike walikamatwa wakibusiana na wanafunzi wengine kadhaa inasemekana wako kwenye mahusiano ya jinsia moja.

  Jumla ya wanafunzi 27 wamefukuzwa shule kutokana na tabia hiyo ya usagaji.

  Watetezi wa haki za binadamu nchini Afrika Kusini wamekuja juu wakipinga uamuzi wa shule hiyo kwakuwa mahusiano ya jinsia moja yanaruhusiwa kisheria nchini Afrika Kusini.

  Afrika Kusini ndio nchi pekee barani Afrika iliyoruhusu wasagaji na mashoga kujitawala kama katika nchi za barani ulaya na Amerika.

  Wanafunzi waliofukuzwa shule katika shule hiyo iliyopo KwaZulu-Natal hawakutajwa majina yao kwa vyombo vya habari na jina la shule hiyo nalo liliwekwa kapuni.

  Gazeti la The Star la nchini humo lilisema kwamba wanafunzi ambao walishindwa kurudi majumbani mwao walipewa hifadhi kwenye nyumba zilizo karibu na shule hiyo.

  Msemaji wa kitengo cha elimu cha Afrika Kusini, Sihle Mlotshwa alinukuliwa na gazeti hilo pia akisema kuwa shule hiyo haina haki ya kuwafukuza au kuwasimamisha shule wanafunzi kwasababu ya masuala yao ya kijinsia.
   
 2. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2010
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,852
  Likes Received: 22,943
  Trophy Points: 280
  kuwa na shule ya wasichana watupu ndo madhara yake...
  wangekuwa na wavulana,wangejifaidia mihogo ya jang'ombe.
  sasa wavulana hakuna wafanyaje??????
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 36,005
  Likes Received: 6,823
  Trophy Points: 280
  dawa ni kuileta mijianaume mitupu sijui nayo ingeleta kasheshe??
   
 4. Mtoto wa Kishua

  Mtoto wa Kishua JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 15, 2009
  Messages: 827
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 45
  Hata ungeweka madume, hao mademu ni lesbians tuu
   
 5. Dreamliner

  Dreamliner JF-Expert Member

  #5
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 17, 2010
  Messages: 2,033
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ni dalili za mwisho wa dunia.
   
 6. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 368
  Trophy Points: 180
  Aisee tuombe kuendelea kuyasikia tu haya!
   
 7. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Jamani haya mambo yapo tangu enzi za Lutu, hata hapa kwetu yapo ila sema kama kawa waTZ ni wanafiki tu. Uliza shule kama Ashira na Kilakala utapata habari zake, ila ukimchunguza bata huwezi kumla!

  Ndio maisha kuweni na moyo wa ujasiri.
   
 8. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #8
  Mar 2, 2010
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,934
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Binadamu sasa tunakuwa viumbe wa ajabu kuliko hata wanyama, maana sijaona Beberu likimega beberu mwenzie hata siku moja
   
 9. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 655
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Uliza uambiwe, kuna beberu moja lilikuwa linajua kazi ni kumega tu! lilimega jike mpaka akafa halafu likawa linamega hata vidume wenzake. We acha dunia tambara bovu!
   
 10. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #10
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Kumbe SA,mi nilifikiri hapa Bongo.Afadhali kama sio hapa kwetu.
   
 11. Emanuel Makofia

  Emanuel Makofia JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 3,851
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145

  Hakuna cha afadhali GS ile shule ina watanzania wanaosoma pale...
   
 12. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #12
  Mar 3, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,561
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  yani ni balaa ata a wanaume kwa wanaume mchezo ni huo huo
   
 13. m

  mchajikobe JF-Expert Member

  #13
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 2,515
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Hii ndio ingekoboana kabisa,bora hao wanao sagana!!
   
 14. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #14
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Binafsi sikubaliani kabisa na hizi shule za jinsia moja. Iwe ya dei au ya bweni. Ni sawa na kufuga nyoka mwenye sumu ktk chumba unacholala.
   
 15. j

  jikis Member

  #15
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  Hizo ni rasha rasha tu, kama hatua mathubuti hazitachukuliwa na Zuma kutengua sheria hiyo, itafikia mpaka majumbani mwao mada kusagana. Tuombe neema zake tu zitunusuru na haya yote.
   
 16. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #16
  Mar 3, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,902
  Likes Received: 1,133
  Trophy Points: 280
  Haya ndiyo matokeo ya maendeleo ya science and technology. Vyakula watoto wanakula siku hizi and the like. Mbona zamani wengi wetu tulisoma shule za wasichana/wavulana pekee na co-education zilikuwa chache (nikizungumzia wakati wa public schools and a very few private). Huko kulikuwa hakuna usagaji wala ushoga (kama ulikuwepo ni maajabu mno) . Ninachofahamu mambo yakiwa magumu, sabuni ilikuwa inatake charge!! Kwa wanawake sina ujuzi sana. Hata zile za Co-education masuala ya zinaa shuleni ilikuwa ni marufuku na nidahmu ilikuwapo. Mabinti walikuwa wanamaliza shule hadi high level na vyuo virgin!!! Leo hii primary school wengine hawana kitu kabisa, kwisha!!! Tafadhali usije ukaenda kuchukua torch leo usiku ukammulike yule binti yako under 15 years akiwa usingizini. Utaweza kupayuka kilio usiku!!! usije kunilaumu!!!

  Je sasa, kama watu wazima hapa over 18 years tunaojadili hapa. Je hayo ndiyo maendeleo au ni nini? Unapofikiria kufanya ngono na mtoto wa umri wa mtoto wako, au mdogo wako ambaye unajua fika ni mdogo anasoma, tena primary school and secondary (at 16-18 watoto wako form six) unaonaje kama angekuwa ni mtoto wako au ni ndugu yako? Halafu wakati mwingine unataka umuingilie kinyume na maumbile?? Je angekuwa wa kwako ungefanya hivyo?? Dhambi hii itakunyemelea wewe na kizazi chako, hadi cha nne!! Halafu mnaanza kulalamika, ohh mwanangu/mjukuu/kitukuu/kilembwe/kilembwekeze kawa shoga/msagaji/malaya/mzinzi/ etc wakati alirithi madhambi yako. Tutubu na Tumrudie Mungu vinginevyo Sodoma na Gomora nyingine yaja!
   
 17. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #17
  Mar 3, 2010
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 12,074
  Likes Received: 4,450
  Trophy Points: 280

  Nani aliyewaambia bongo hakuna hii tabia?? ipo na inakua kwa kasi sana.

  tuombe Mungu
   
 18. S

  S. S. Phares JF-Expert Member

  #18
  Mar 3, 2010
  Joined: Nov 27, 2006
  Messages: 2,141
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0


  Mkuu Huu mfano wako...umeniacha kwenye mataa kabisa...fafanua kidogo tafadhali.
   
 19. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #19
  Mar 4, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,484
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Ya kweli haya? Mbona mfano upo straightforward?
   
 20. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #20
  Mar 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  kwani kwetu hayapo? sema hayatangazwi tuu.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...