Wanafunzi wanywa sumu kupinga kuzuiwa ngono | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wanywa sumu kupinga kuzuiwa ngono

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by charger, Jul 13, 2011.

 1. charger

  charger JF-Expert Member

  #1
  Jul 13, 2011
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 2,327
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 145
  Habari zenu wakuu,naamini mpo salama popote mlipo.

  Jana niliwaletea kituko cha vitoto vya shule kutelekezwa guest nikawa na maswali mengi ambayo hata ninyi pia mlionekana kuwa nayo kwa jinsi mlivyo changia.Leo tena nimekutana na kituko kingine cha hawa watoto/wadogo zetu.Nakuendelea kujiuliza mustakabali wa hiki kizazi.


  WANAFUNZI wawili wa Shule ya Sekondari Zimanimoto, mkoani Ruvuma wamenusurika kufa baada ya kunywa sumu ya panya na vidonge saba vya panadol, kwa
  kile kinachodaiwa walionywa na wazazi wao kuacha tabia ya kujihusisha na vitendo vya ngono.

  Inadaiwa wazazi walitoa onyo kwa wanafunzi hao, baada ya kugundulika wana uhusiano wa kimapenzi, huku mmoja wao akifukuzwa nyumbani na mama yake mzazi.

  Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Bw. Michael Kamuhanda alisema tukio hilo lilitokea juzi saa 5 asubuhi eneo la Msamala, ambapo binti mhusika alifukuzwa nyumbani na mama yake mzazi baada ya kushindwa kuelewana mara kwa mara.

  Alisema hali hiyo ilitokana na mama huyo kutoridhishwa na tabia ya mwanawe na siku ya tukio alishikwa na hasira baada ya kumuonya mara kwa mara kuhusu tabia ya kujihusisha na vitendo viovu, lakini ilishindikana, hivyo kuamua kumfukuza nyumbani.

  Alisema kuwa baada ya binti huyo kufukuzwa alienda kwa mpenzi wake
  ambaye ni mwanafunzi mwenzake.

  Alisema wakiwa Msamala, binti huyo alikunywa sumu ya panya kwa lengo la kujiua, na mpenzi wake kuona hivyo naye aliamua kunywa sumu hiyo na vidonge saba aina ya panadol kwa lengo la kutaka wafe wote.

  Hata hivyo, alisema baada ya muda mfupi wasamalia wema walifanikiwa kuwaona na kuwakimbiza katika Hospitali ya Mkoa kwa ajili ya matibabu.

  Kwa upande wake, Kaimu Mganga Mkuu Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa Songea (HOMSO) Dkt. Gideon Njowoka alikiri kupokea wagonjwa hao na kuongeza kuwa hali za wanafunzi hao zinaendelea vizuri.

  Alisema baada ya kupatiwa matibabu mwanafunzi wa kiume alitoroka na kwenda kusiko julikana.

  Source:Majira 12th JULY 2011

  KAZI NI KWAKO
   
 2. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #2
  Jul 13, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Wana umri gani hao watoto jamani wanaharaka nayo ya nini haiondoki hiyo kukicha zinakuja mpyaaaaaaaaa.Mungu atunusuru na vizazi vyetu.
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Jul 13, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 159,018
  Likes Received: 420,655
  Trophy Points: 280
  wangewaacha wajifie tu kwa nini iko nini?......si wengine huzaliwa kila siku......................
   
 4. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #4
  Jul 13, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  nimetikisa kichwa tu basi........
   
Loading...