Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Hong Kong wakamatwa kwa madai ya kuunga mkono ugaidi

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
Wanafunzi wanne wa Chuo Kikuu cha Hong Kong wamekamatwa leo kwa madai ya kuunga mkono ugaidi. Polisi wa Hong Kong wamesema waliokamatwa ni wanafunzi wa kiume wenye umri wa kati ya miaka 18 na 20, waliokuwa wanachama wa kamati ya baraza la wanafunzi.

Afisa wa polisi Li Kwai-wah, amesema wanafunzi hao wamekamatwa wakihusishwa na mkutano wa baraza hilo ambalo linaunga mkono ugaidi.

Waliokamatwa ni pamoja na rais wa baraza la wanafunzi, ambao walikuwa miongoni mwa zaidi ya wanafunzi 30 waliohudhuria mkutano uliopitisha azimio la kuomboleza kifo cha mtu mwenye umri wa miaka 50 aliyeuawa kwa kuchomwa kisu na polisi mwezi uliopita.

Ukamataji huo umefanyika chini ya sheria yenye utata ya usalama wa taifa na huenda ikazusha wasiwasi mpya kuhusu uhuru wa kujieleza mjini Hong Kong
 
Binafc Wanaouwa civilians ndiyo magaidi wengine cyajui.

Mfano; marekani na washirika wake, na vikundi vyao vya kigaidi ndio magaidi wenyewe.
 
Back
Top Bottom