Wanafunzi wanaswa wakifanyiana mitihani IFM | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wanaswa wakifanyiana mitihani IFM

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Che Kalizozele, Sep 15, 2009.

 1. Che Kalizozele

  Che Kalizozele JF-Expert Member

  #1
  Sep 15, 2009
  Joined: Jul 20, 2008
  Messages: 778
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  na Sauli Giliard


  WATU watatu, akiwamo mwanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam wamekamatwa wakiwafanyia mitihani wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wanaosoma ngazi ya stashahada ya juu pamoja na shahada.

  Mwanafunzi huyo, Frank Kaduma, aliyekuwa anamfanyia mtihani mwanafunzi aliyemtaja kwa jina moja la Tina, alikuwa ameahidiwa na mtu aliyemuunganisha na mtahiniwa huyo kuwa baada ya kutoka kwenye mtihani huo angelipwa sh 150,000.

  Tanzania Daima ilimshuhudia mtuhumiwa huyo akihojiwa na Michael Andekisye, ambaye ni Msajili wa Wanafunzi chuoni hapo.

  Msajili huyo alisema kuwa kitambulisho alichokuwa akikitumia kumfanyia Tina mtihani kilikuwa na jina la Christian Mbago, mwanafunzi wa mwaka wa tatu.

  Kaduma alifafanua mbele ya ofisi hiyo kuwa aliitwa na rafiki yake ambaye hata hivyo hakutaka kumtaja jina, na baadaye alimuunganisha na mtahiniwa na kukubaliana kiasi hicho cha fedha baada ya kazi hiyo kumalizika.

  “Mimi ninasoma Azania, nachukua PCM (Fizikia, Kemia na Hisabati), rafiki yangu anasoma masomo ya biashara na mtihani wa leo una hisabati, hivyo juzi nilikuja naye ili anionyeshe darasa na leo ndiyo nimekuja kumfanyia mtihani,” alisema Kaduma.

  Wakati mwanafunzi huyo akihojiwa, mwanafunzi mwingine, John Kapinga, alikamatwa na kupelekwa katika ofisi ya msajili baada ya kukutwa akimfanyia mtihani mwanafunzi wa mwaka wa tatu chuoni hapo, Joel Mlengule, anayesoma Stashahada ya Juu ya Hifadhi ya Jamii (Advanced Diploma in Social Protection).

  Kapinga, alikiri kuwa alihitimu kidato cha sita mwaka 2003, akisoma masomo ya PCM, pamoja na kuahidi kwamba angetoa ushirikiano ili kumkamata mtahiniwa halisi.

  “Sikutaka kufanya, ila nilishawishiwa mara nne sikutaka, hata ikafikia hatua ndugu yake kunishawishi, nikakubali, ila dhamiri ikinisuta. kwani hakuna malipo yoyote tuliyoahidiana na ndugu yangu huyo,” alisema Kapinga huku akijiinamia.

  Tanzania Daima ilishuhudia kitambulisho chake kikiwa na jina la Joel Mlengule, kikiwa na namba ya usajili ADSP/16492/2007 na kinamalizika muda wake mwaka huu.

  Kwa upande wake, Joel Mlengule, aliyefanyiwa mtihani na kukamatwa akiwa nje ya eneo la IFM akimsubiri Kapinga, alinaswa na walinzi wa chuo na kuhojiwa, ambapo alikiri kufanyiwa mtihani na Kapinga.

  Mlengule ambaye ni mkazi wa Upanga, jijini Dar es Salaam, alikiri kuwapo mtu aliyemuunganisha na Kapinga, baada ya kufeli somo lake la hesabu mara mbili mfululizo, hivyo hakutaka hali hiyo imrudie, hasa ikizingatiwa kuwa huo ulikuwa mtihani wa mwisho chuoni hapo.

  “Ni kweli alikuwa ananifanyia mtihani baada ya kufeli somo hili mara mbili. Niliona mwaka huu, na huu ni mtihani wangu wa mwisho, mimi sijui hesabu, ndiyo maana hata aliponiambia anifundishe nilikataa na kumwomba anisaidie kunifanyia,” alisema Mlengule.

  Kwa mujibu wa Msajili wa Wanafunzi chuoni hapo, tukio jingine la namna hiyo lilitokea jana, ambapo msichana mmoja alikimbia na kuacha viatu vyake, baada ya kubainika kuwa alikuwa akimfanyia mtihani mwanafunzi ambaye jina lake halikupatikana mara moja.

  Aliongeza kuwa, mwaka jana matukio hayo yalitokea na imebainika kuwa kuna wakala anayewaunganisha wanafunzi wa chuo na watu wa nje kuwafanyia mitihani hiyo kinyume cha taratibu.

  Akizungumzia udhibiti wa wanafunzi hao, Andekisye alisema chuo hicho kiko katika mchakato wa kubadili vitambulisho kwa wanafunzi na kuongeza nguvu katika usimamizi.

  Alisema wanafunzi waliobainika kufanyiwa mitihani watafikishwa kwenye bodi ya chuo na waliowafanyia watapelekwa polisi, kwani tukio hilo ni la kughushi.

  Sina hakika kama tutafika kwa mwendo huu.
   
 2. s

  saikon nokoren Member

  #2
  Sep 15, 2009
  Joined: Jun 30, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WATU watatu, akiwamo mwanafunzi wa kidato cha sita katika Shule ya Sekondari ya Azania, jijini Dar es Salaam wamekamatwa wakiwafanyia mitihani wanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), wanaosoma ngazi ya stashahada ya juu pamoja na shahada.
  Hii ni aibu kubwa kwa wanafunzi wetu wa vyuo vyikuu,hata siamini mwanafunzi wa kidato cha sitta kumfanyia mtihani mwanachuo wa stashahada ya juu na shahada,hii ni kweli wandugu?
   
 3. GP

  GP JF-Expert Member

  #3
  Sep 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  unabisha nini sasa?, mtihani wa hesabu wa adv diploma wa mtu anayesoma biashara unadhani utamshinda mtu anayesoma PCM???, simple calculus, algebra etc!!. simple, very possible.
   
 4. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #4
  Sep 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Hahahaha dah hesabu ni ugonjwa kweli wa taifa....
   
 5. GP

  GP JF-Expert Member

  #5
  Sep 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  aah sana mkuu!,
  tatizo msingi mzuri kwa wanafunzi hasa wa shule za msingi haujengwi, hivyo watoto wanakua na akili ya jumla kwamba hesabu ni somo gumu!, but amini usiamini mathematics is one of the easiest subjects, just playing around with logics!!.
  ukiweza hesabu then hakuna somo lolote la sayansi litakuzingua.
   
  Last edited: Sep 15, 2009
 6. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #6
  Sep 15, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Utajengwa vp wkt hao walimu wanao wafundisha mnawalipa mishahara kiduchu 150000/= kwa mwezi wkt nyie vibopa hiyo ni pesa ya vocha kwa siku wao wanapiga miayo tu. Acheni iendelee kufeli mpaka muwakumbuke walimu kwanza ndo wanao watoa matongo tongo lakini mnawasahau kana kwamba wao hawastahili kula vizuri, kulala pazuri, kunywa vinono vinono, kuendesha escudo n.k
   
 7. GP

  GP JF-Expert Member

  #7
  Sep 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  mkuu
  tatizo sio mshahara mdogo kwa walimu!, bali uwezo wa walimu wenyewe sio mzuri sana.
  hebu nambie mwalimu wa vodafasta anifundishie mwanangu kweli hesabu ataelewa??.
  ujue waliosemaga ualimu ni wito ndio kile kipindi amabcho tulikua na walimu wa uhakika mtu unapigwa shule kweli unasema hesabu zimeingia kichwani sawa sawia, siku hizi twisheni nyingi uswazi na watoto hawaelewi wala hawana misingi mizuri ya hesabu.
   
 8. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #8
  Sep 15, 2009
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Tatizo lingine ni uongo tunaoimbiwa tukiwa bado wadogo.Ukiingia shule utasikia kila mtu anasema hesabu ngumu! hesabu ngumu! sasa unaweka hilo akilini na unaamini hesabu ngumu bila hata kuzijaribu kama ngumu kweli ,unafeli kabla hujaanza kuzifanya.Kumbe mawazo yangebadilika na kuamini inawezekana hakuna ambaye angefeli hesabu sababu ukweli ni kuwa hesabu ni rahisi sana tu.
   
 9. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Tatizo ni rushwa wakati wa kufanya admission ya wanafunzi wa IFM, so baadhi yao hawakuwa na sifa hata za kuwawezesha kujiunga, sasa ndo unakuta mitihani hata ya hesabu rahisi tu inawasumbua.
   
 10. GP

  GP JF-Expert Member

  #10
  Sep 15, 2009
  Joined: Feb 5, 2009
  Messages: 2,073
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  uko sawa kabisa,
  kula gwala!!.[​IMG]
   
 11. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #11
  Sep 15, 2009
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  Wasichana wa ifm kazi yao kubwa ni kuchuna mabuzi
  no wonder inaiitwa institute of female management.
   
 12. P

  Patrick Nyemela JF-Expert Member

  #12
  Sep 15, 2009
  Joined: Nov 25, 2008
  Messages: 330
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Wanafunzi wengine wa IFM ni "viwango duni", sasa hii ni aibu kubwa sana. Vile vile nasikia IFM inaongoza kwa wanachuo kununua mitihani. AIBU
   
 13. j

  josephkibena Member

  #13
  Sep 15, 2009
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 16
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Duuh huu sasa kweli upumbavu,kuanzia Frank Kaduma pamoja na washiriki wake,vimini vitawaponza watoto,mabinti wengi wa IFM wanachanganya watoto,baba zao n.k.

  Mtu mwenye akili zako huwezi kukubali kumfanyia mtu ona sasa mnavyodhalilika.Frank kimemponza kimini,IFM wanatega saaaaaaaaaana,shauri zenu.
   
 14. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #14
  Sep 15, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Noma tupu , Majirani zetu kenya, uganda rwanda ,zaire malawi n.k sijui kama watatupa kazi aibu tupu....
   
 15. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,007
  Trophy Points: 280
  Hesabu sio ugonjwa wa Taifa tu bali ni wa dunia, kila nchi inalalamikia wanafunzi wake kukimbia masomo yanayokuwa na hisabati, nilikuwa Zambia, Malawi, BOtsw na hata SA kilio ni hichohicho tu
   
 16. b

  bnhai JF-Expert Member

  #16
  Sep 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Wawapi hawachuni?
   
 17. b

  bnhai JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hawa wanafunzi wa IFM hawakutoka kwenye sayari tofauti na wengine. Kugeneralise hao na kuwaexclude wengine si sahihi
   
 18. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #18
  Sep 17, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  tutafika tu mjomba kwani hii ilianza long time
  wewe unafikiri yanayotokea BOT chanzo ni nini????
  hawa bahati mbaya tu wamekamatwa kabla ya kuingia ofisini
   
 19. O

  ODILI SAMALU JF-Expert Member

  #19
  Apr 20, 2014
  Joined: Dec 13, 2013
  Messages: 1,261
  Likes Received: 209
  Trophy Points: 160
  Siamini kama tumefikia huku
   
 20. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #20
  Apr 20, 2014
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,788
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  Chezea Namba weye!!!
   
Loading...