Wanafunzi wanasoma kwa kugeuziana migongo Ruvuma | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wanasoma kwa kugeuziana migongo Ruvuma

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by armanisankara, Aug 8, 2012.

 1. a

  armanisankara JF-Expert Member

  #1
  Aug 8, 2012
  Joined: Jul 15, 2011
  Messages: 283
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  WANAFUNZI 201 kuanzia darasa la tatu hadi la sita katika shule ya msingi Kidugalo kata ya Rwinga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma wanasoma katika vyumba viwili vya madarasa kwa kugeuziana migongo hali ambayo inachangia kushusha taaluma katika shule hiyo.

  [​IMG]
  Wanafunzi wa darasa la tatu na la nne katika shule ya msingi Kidugalo kata ya Rwinga Namtumbo mjini mkoani Ruvuma wakisoma katika chumba kimoja kwa kugeuziana migongo.


  Mwalimu mkuu wa shule hiyo Owini Mpangala alibainisha kuwa wanafunzi 51 wa darasa la tatu na wanafunzi 56 wa darasa la nne wanasoma katika chumba kimoja kwa kugeuziana migongo na wanafunzi 62 wa darasa la tano na wanafunzi 32 wa darasa la sita wanasoma katika chumba kimoja kwa kugeuziana migongo.

  "Madarasa mawili kusomea katika chumba kimoja kunasababisha kila darasa kufundishwa vipindi vinne tu kati ya vipindi nane vinavyotakiwa kufundishwa kwa siku,walimu wawili hawawezi kuingia kwa wakati mmoja kufundisha kwenye chumba kimoja,vipindi vinne vinapotea darasa halifundishiki'',alisisitiza.

  Kwa mujibu wa mwalimu Mpangala shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 yenye wanafunzi 453 ina vyumba vinne tu vya madarasa kati ya mahitaji ya vyumba nane na kwamba shule hiyo haina ofisi ya walimu hali ambayo inasababisha mwalimu mkuu na walimu kutumia ofisi moja ambayo hata hivyo haitoshi kutokana na idadi ya walimu 13 waliopo katika shule hiyo. Kutokana na hali hiyo baadhi ya walimu wanakaa nje ya ofisi wakati wa kiangazi huku wakiendelea kufanyakazi za kusahihisha madaftari ya wanafunzi wakipigwa na jua hali ambayo inaleta kero kubwa kwa walimu na wanafunzi.

  Mkuu wa shule hiyo alisema amechukua hatua mbalimbali za kukabiliana na matatizo hayo ikiwa ni pamoja na kuyapeleka katika kamati ya shule na Baraza la madiwani ambayo wameahidi katika msimu ujao wa fedha wanatarajia kulipatia kipaumbele hasa kero ya upungufu wa vyumba vya madarasa,samani na ofisi ya walimu.

  "Hapa kwangu uongozi wa serikali ya kijiji umekataa kujenga vibanda vya nyasi kama ilivyo katika shule nyingine kwa madai kuwa hapa ni mjini hawawezi kujenga vibanda vya nyasi ni aibu,wamefyatua tofali zipo kwenye tanuri'',alisema. Baadhi ya walimu wanaofundisha katika shule hiyo wamesema wanatamani kuacha kazi au kuhama katika shule hiyo kutokana na changamoto nyingi ambazo hazijapatiwa ufumbuzi kwa muda mrefu na kuchangia kushusha elimu katika shule hiyo ambayo ipo mjini.

  Mratibu elimu kata ya Rwinga Thomas Komba amekiri shule za msingi katika kata yake inakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo shule ya msingi Kidugalo ambapo hivi sasa uhamasishaji unafanyika ili kumaliza kero ya upungufu mkubwa wa vyumba vya madarasa.

  [​IMG]

  Baadhi ya walimu katika shule ya msingi Kidugalo wakisahihisha madaftari ya wanafunzi nje baada ya shule hiyo iliyoanzishwa mwaka 2007 kukosa ofisi ya walimu.


  Aliongeza kuwa wananchi wa eneo la Kidugalo mwaka jana wamefyatua na kuchoma tofali kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na kwamba hivi sasa kinachosubiriwa ni nguvu toka serikalini kutoa vifaa vya kiwandani ili kuweza kufanikisha kupunguza kero hiyo ya muda mrefu.

  Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo ina shule za msingi 107 kati ya hizo shule 105 zinamilikiwa na serikali na shule mbili ni za watu binafsi na mashirika ya dini.
   
 2. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2012
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  bongo hali ya madarasa mjengwablog 8-3-12.jpg

  haya madai hayatekelezeki!!
   
 3. b

  baajun JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tusiende kwenye ufunguzi wa ccm washington dc,serikali ya ccm imeleta pesa kwa ajili ya kukusanya watu kutoka kwenye state nyingine ,na sio kuelekeza pesa kwenye sehemu muhimu kama hii hapo juu inasikitisha sana.naomba watanzania tunaoishi washington dc,kutoiunga mkono ccm hapa.tuonyeshe mfano kwa kuwakataa,mwambie rafiki yako ,dada yako ,mjomba wako kuwa hatuendi kwenye ufunguzi hata kama wangemleta 50 cent kupiga muziki.sasa tunatakiwa kushikamana na kuonyesha msimamo.mungu ibariki tanzania
   
 4. b

  baajun JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ewe mtanzania unaishi usa,naomba angalia hizi picha alafu tushirikiana kutokuja kwenye ufunguzi wa tawi la ccm washington dc.sote twaweza
   
 5. m

  magohe JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2012
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Hivi naomba kujua kama eneo hilo lina mwakilishi wa wananchi ktk serikali hii na kama yupo kazi yake ni ipi? Ama kweli hii ni serikali sikivu. Ee bwana eee naomba nikutume kwa mwl.mkuu wa shule hiyo abadili moto ya shule na isome hivi "UJINGA NI URITHI WETU"
   
 6. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  thubutu...nania asiende ?labda sio watanzania..wanavyoipenda ccm chama lao sio rahisi ila jitahidi nawe kwenda ukatuwekee mipicha ya jinsi ukumbi utakavyokuwa umefurikaaa
   
 7. JOYCE PAUL

  JOYCE PAUL JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2012
  Joined: Jan 8, 2010
  Messages: 1,007
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  hii ni hali ya kawaida kabisa kwa nchi za africa tatizo sio kwa sisiem ,na mimi hapa nilipo nilitokea huko huko tena bora yao wanakaa kwenye dawati me nilikaa chini nakuandikia kwenye tofali amablo nalo tulikuwa tunagombania...but mungu tumuombe airehemu tanzania kwani tulichopitia sisi watoto wetu wasikipitie....nasisitiza shida sio ccm its a problem all over africa
   
 8. Mamndenyi

  Mamndenyi JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 29,081
  Likes Received: 6,545
  Trophy Points: 280
  Nambari wani ni ccm
   
 9. Bushbaby

  Bushbaby JF-Expert Member

  #9
  Aug 9, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 1,577
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Hivi mbunge wao anafanya nini Bungeni??
   
 10. m

  magohe JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2012
  Joined: May 21, 2011
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  karne hii na rasilimali zote zilizopo ikiwemo misitu ya kutosha unahalalisha mambo hayo? nchi hizo za africa unazozisema zimeshaanzisha mpango wa kugawia wanafunzi laptops za kujifunzia kwa kila mtoto mathalani Rwanda jirani zetu bado tu wewe unasapoti uji.... kama huo wa kukaa chini!!! Ama kweli kupenda ni ugonjwa ,la kama si ugonjwa ni upungufu wa akili.Hujaona tu kuwa kwa kukaa kwako chini tayari umeshaathirika kwa kuzalisha mtu eti anajiita kapita shule kutoa point za hovyo kiasi hicho!!! laaa ajabu na kweli na hii ni ikabu kwa wana jf wote kuwa na mtazamo kama huu humu ndani.
   
 11. B

  Bobuk JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 5,876
  Likes Received: 481
  Trophy Points: 180
  Jamani mimi ninafahamu ili SHULE ifunguliwe na kuanza kupokea wanafunzi lazima iwe imetimiza VIGEZO vifuatavyo
  1. Vyumba vya kutosha vya madarasa
  2. Ofisi ya walimu/mwalimu
  3. Matundu ya kutosha ya vyoo
  4. etc etc

  Hivi siku hizi hivyo VIGEZO havifuatwi tena na Wizara ya Elimu kabla ya shule kuruhusiwa ku operate?
   
 12. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  naona pameandikwa elimu ni urithi wetu, kwani elimu ni bia ya safari? Msinichanganye kabisa; mie najua urithi wetu ni bia ya safari.
   
 13. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Jamani nyie majambazi ccm hamyaoni hayaaaaaaaaaaaaa!!!!!!!! mpaka tuwaambiejeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!! za rada mmpeleka wapi tena wakati mlisema zitatumika kuboresha mashuleeeeeeeeeee!!!!!!!!! nyie vipi bhanaaaaaaaaaa!!!!!!!!!

  Arrrrrrrrrrrrrrrrrggggggggggggggggggggghhhhhhhhhhhhhhhhh!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!

  hakyanani nitaandamana peke yangu sasa!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
Loading...