Wanafunzi wamechana karatasi kwenye daftari zao ili kujibia mitihani. Nikigoma kusahihisha nitapata madhara gani?

Habuba

JF-Expert Member
Oct 11, 2015
918
1,201
Wadau jukwaa la elimu na walimu wenzangu mkuje tuelezane kwenye vituo vyenu vya kazi hali ikoje?

Kipi kinachotakiwa kufanyika kwenye ufanyaji wa hii mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza shule za sekondari?

Mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza (Terminal examination June 2018)

Iko hivi Mimi ni mwalimu shule ya sekondari X. Leo wanafunzi wameanza mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza.

Cha ajabu ambacho sijawahi kuona/kusikia/kuota ni wanafunzi kuambiwa KILA MWANAFUNZI AJE NA KARATASI ZAKE ZA KUJIBIA KILA MTIHANI ATAKAOFANYA.

Shule haina hela na HELA ZA ELIMU BURE HAZIGAWANYIKI KUFANIKISHA MITIHANI HIYO.

Kilichofanyika Leo na kitachofanyika kesho wanafunzi kuchana karatasi kwenye daftari zao. Kumbuka wanafunzi wana daftari tofauti tofauti, kuna za shilingi 300, 500, 1000, na kuna wenye makaunta. Kumbuka karatasi zinapishana rangi, urefu na upana (dimensions) kulingana na bei na aina ya daftari/kaunta husika karatasi ilipochanwa.

Mitihani ikikusanywa inaonekana kama uchafu umekusanywa kiasi kwamba huwezi kuibeba upelekee MKE WAKO akusaidie kusahihisha Yale maswali ya kuchagua hapo utaonekana fala umepeleka upupu gani?

Mimi binafsi sisahihishi upuuzi huo (nagoma pekeangu) ila najua kuna waalimu pale iyo kwao wala sio tatizo na hakika wataisahihisha. Einstein alisema "if you move naked around the tree at a speed of light the probability of fucking yourself is one" wao sio shida kwao.

Wadau wa Elimu na waalimu mkuje tujadili hili, point ipanguliwe kwa point mseme na madhara ntayopata kwenye huo mgomo wangu.

Karibuni.
 
Poleni na elimu bure. Mwambie mwalimu mkuu atoe tamko kila mtoto alete karatasi za kufanyia mitihani. Nchi za Afrika huwa hatuna vipaumbele. Mara nyingi tunadonoadonoa tu.
 
We wa lini?
Sisi tumefanya hizo..
It's not about the dimensions of the paper. It's about the answers.
 
Poleni na elimu bure. Mwambie mwalimu mkuu atoe tamko kila mtoto alete karatasi za kufanyia mitihani. Nchi za Afrika huwa hatuna vipaumbele. Mara nyingi tunadonoadonoa tu.

Mkuu hujui lile tamko la haitakiwi mwanafunzi kuchangishwa chochote shuleni
 
We wa lini?
Sisi tumefanya hizo..
It's not about the dimensions of the paper. It's about the answers.

Unazibebaje karatasi dimensions tofauti tofauti? labda kama unawekaga kwenye gunia kama mihogo

Mkuu hujui kwanini necta wanatoa booklets?
Its okay lakini maana najua kuna waalimu wanatokea sengerema.
 
Poleni na elimu bure. Mwambie mwalimu mkuu atoe tamko kila mtoto alete karatasi za kufanyia mitihani. Nchi za Afrika huwa hatuna vipaumbele. Mara nyingi tunadonoadonoa tu.
Nchi hii wakati mwingine tunabaki kujishangaa tu...

Elimu bure kwa maoni yangu ilipaswa ianze kwa phase au pilot study ambapo Serikali na Wazazi wangekuwa na Cost Sharing Scheme.

Mfano, Serikali ikafuta ada na mzazi akachangia kwenye maendeleo ya mtoto.

Tungeanza mfano pilot study kwa mikoa au Kanda..etc

Serikali inapaswa iwekeze kwanza kwenye Elimu, Afya na Miundombinu...kwa mfuatano uliotoa value chain kwa kingine..

Tukitaka kuyafanya yote kwa pamoja tutakuwa tunadonoa donoa tu hadi 2025...na hatutaweza kufikia Nchi ya Uchumi wa Kati.
 
Wadau jukwaa la elimu na walimu wenzangu mkuje tuelezane kwenye vituo vyenu vya kazi hali ikoje?

Kipi kinachotakiwa kufanyika kwenye ufanyaji wa hii mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza shule za sekondari?

Mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza (Terminal examination June 2018)

Iko hivi Mimi ni mwalimu shule ya sekondari X. Leo wanafunzi wameanza mitihani ya kumaliza muhula wa kwanza.

Cha ajabu ambacho sijawahi kuona/kusikia/kuota ni wanafunzi kuambiwa KILA MWANAFUNZI AJE NA KARATASI ZAKE ZA KUJIBIA KILA MTIHANI ATAKAOFANYA.

Shule haina hela na HELA ZA ELIMU BURE HAZIGAWANYIKI KUFANIKISHA MITIHANI HIYO.

Kilichofanyika Leo na kitachofanyika kesho wanafunzi kuchana karatasi kwenye daftari zao. Kumbuka wanafunzi wana daftari tofauti tofauti, kuna za shilingi 300, 500, 1000, na kuna wenye makaunta. Kumbuka karatasi zinapishana rangi, urefu na upana (dimensions) kulingana na bei na aina ya daftari/kaunta husika karatasi ilipochanwa.

Mitihani ikikusanywa inaonekana kama uchafu umekusanywa kiasi kwamba huwezi kuibeba upelekee MKE WAKO akusaidie kusahihisha Yale maswali ya kuchagua hapo utaonekana fala umepeleka upupu gani?

Mimi binafsi sisahihishi upuuzi huo (nagoma pekeangu) ila najua kuna waalimu pale iyo kwao wala sio tatizo na hakika wataisahihisha. Einstein alisema "if you move naked around the tree at a speed of light the probability of fucking yourself is one" wao sio shida kwao.

Wadau wa Elimu na waalimu mkuje tujadili hili, point ipanguliwe kwa point mseme na madhara ntayopata kwenye huo mgomo wangu.

Karibuni.
Usishangae Mwl nchi yetu hapo ndo tumefikia, usikatae kusahihisha kazi za wanafunzi kisa karatasi maana hilo si geni hapa nchini. Jana kuna Halmashauri nimeona form four wanafanya mock ya mkoa lakini kila mwanafunzi alitakiwa ajitegemee kwenye karatasi za kujibia. Ila waliotufikisha hapo nafikiri watoto wao hawana hali hiyo. Tufanye kazi hamna namna ya kulikwepa hilo wenye mpini ni sisi kumbe wao wameshika makali.
 
Sasa unagomea mtihani au unagomea karatasi?kama ni karatasi basi usiwape mtihani mpaka karatasi zitolewe kama ni mtihani basi usisahihishe
 
Wasaidie watoto hawajakukosea wao, hasira za malimbikizo yako, kuchelewa kwa mshahara na manyanyaso mengine ya serikali hii dhidi yenu walimu hayakuanza leo na hayasababishwi na wanafunzi.
 
Mitihani ikikusanywa inaonekana kama uchafu umekusanywa kiasi kwamba huwezi kuibeba upelekee MKE WAKO akusaidie kusahihisha Yale maswali ya kuchagua hapo utaonekana fala umepeleka upupu gani?

Mimi binafsi sisahihishi upuuzi huo (nagoma pekeangu) ila najua kuna waalimu pale iyo kwao wala sio tatizo na hakika wataisahihisha. Einstein alisema "if you move naked around the tree at a speed of light the probability of fucking yourself is one" wao sio shida kwao.
Mhhhhhh haya maajabu. Mwenye jukumu la kusahihisha ni wewe na si mkeo, ukifanya hivyo huwatendei haki wanafunzi na bibie pia. Hata kwenye MCQ mambo yanaweza kwenda arijojo.
Haipendezi kwa wanafunzi kufanyia mtihani kwenye mikaratasi ya ajabu ajabu-lakini tujiulize kama hiyo ndiyo hali halisi basi kwa msimamo wako uamuzi uwe kufunga shule hiyo au kujiongeza (improvise) na watoto wasome na tathmini ya mitihani ifanyike. Kama wanaleta vitabu vyao na kuchana karatasi je hakuna uwezekano wa kuwa ambia waje na karatasi za aina fulani ili zifanane? What ever the case kugoma kusahihisha mtihani ni njia ya uhakika kujitafutia makubwa.
 
Wensahihisha hivyo hivyo wazazi wao si wanafurahia hasara kwao bora liende .

Kila mtu atabeba msalaba wake
 
Una hamu ya kuhamishiwa Nursery school !

Wewe sahihisha mitihani Acha Mbwembwe Na Ujuaji

Cha msingi unapokea ki TGS D chako mengine hayakuhusu
 
Unaona ajabu kubeba karatasi ambazo hazina size moja!

Kwani ukizibeba utachekwa!

Nakumbuka Zamani, tulikuwa tunaambiwa tuje na makaratasi ya kufanyia Mitihani, Tulikuwa tunaenda Dukani, tunanunua Katasi fulani ndefu....Tunapeleka shule.
 
Elimu bure ni mzigo kwa walimu! Vipi hiyo mitihani yenyewe imechapwa au inaandikwa ubaoni?
 
Shule binafsi (private) huwa wazazi tunatakiwa kupeleka rim za karatasi za A4 sio chini ya mbili kila muhula kwani huwa wanazifanyia nini kama sio kuchapisha mitihani?
Huko serikalini kama wanashindwa kutamka mahitaji kama hayo ya rim walau moja kwa mwaka wataepuka hili tatizo kabisa . Mambo ya kudai watoto waje na karatasi kwa kweli ni changamoto karatasi linafikaje shuleni likiwa limenyooka mtoto anayetembea umbali mrefu.

Wizara ya Elimu inatetemeka tangu waambiwe bure basi nao wamekaa kiburebure tu wajiongeze kwenye vitu kama hivi . Kama ilivyo lazima kwa uniforms na madaftari basi kwa mwaka mtoto apeleke rim moja shuleni. Hii bure bure hii inaharibu watoto wetu physiologically. Kubebana na makaratasi tena wapi na wapi
 
Nakumbuka shuleni kwetu kila mwaka tulikua tunapeleleka ream moja A4 na ream moja aina zile ndefu ya mistari ambazo tulikua tunagawiwa siku za mtihani kwa ajili ya kujibia. Hiki kichaa cha elimu bure aliekileta alikua anafikiri elimu ni ada tu
 
Back
Top Bottom