Wanafunzi Waliohitimu kidato cha sita Mwaka 2022 waitwa JKT

Nali aliwahi kukwama popote kwa kutokwenda JKT kwa mujibu wa Sheria?
Hii nikwaajili ya manufaa ya muendaji mwenyewe sidhani kama muhusika hataki kwenda atalazimishwa.
Kwa Dunia ya Sasa yenye ushindan na ajira chache na kisomo cheti Cha white collar jobs ni bora uende Ili uongeze nafasi Yako ya kuajiriwa hyko mbeleni.. kuanzia kwwnye majeshi na zipo ajira zingne wanatoa kipaumbele Kwa waliopita jeshini.
Kumbuka ajira za majeshi mwaka huu walitoa kigezo Cha kupitia JKT, ambao hawakupita waliachwa pemben.
 
Mkuu wa Tawi la Utawala wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), Brigedia Jenerali Hassan Mabena amewaita vijana wote waliohitimu kidato cha sita 2022 kutoka shule zote za Tanzania Bara kujiunga na mafunzo ya jeshi hilo kwa mujibu wa sheria.

Brigedia Jenerali Mabena ametoa wito huo leo Jumanne Mei 31, 2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mafunzo hayo kwa mwaka huu, akiwataka kuanza kuripoti kuanzia Juni 3 hadi 17 katika makambi waliopangiwa.

Kwa mujibu Brigedia Mabena, vijana hao wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma, Msange, Ruvu, Mpwapwa, Makutupora, Mafinga, Makuyuni, Kanembwa, Itaka, Mlale, Mgambo, Oljoro, Milundikwa, Nachingwea, Kibiti Bulombwa na Maramba.

"Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho waripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani. Kambi hii ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hii.

"Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajab Mabele awakaribisha vijana wote walioitwa ili kujiungna katika kujifunza uzalendo, umoja wa kitaifa, stadi za kazi na maisha, utayari kulijenga na kulitumikia Taifa,"amesema Brigedia Jenerali Mabena.
Mbona karibu mno siku ya kureport!
 
Back
Top Bottom