usininukuu
JF-Expert Member
- Aug 8, 2011
- 380
- 44
Inauma sana kumharibia mtu maisha yake kisa anadai haki.
Kuna tetesi zilizoenea huku mtaani na pale UDSM kwamba hii fukuza fukuza ya wanafunzi ni malipizi ya JK baada ya kuzomea alivyoenda kupewa degree ya heshima. Inasemekana Museven alimuuliza JK "hawa wanaokuzomea unawalipia ada?" JK alijibu "ndiyo" Museven aliendelea "ingekuwa Uganda ningewafukuza wote hawa na kudahili wengine"...Je inawezekana JK alifuata ushauri wa Museven? Maana wanaomjua wanadai ni mtu wa visasi sana. Nawasilisha.
Na BUKOBA kuna wafunzi 5 wamefukuzwa shule walihudhuria kongamano liliandaliwa na CDM wamefukuzwa hii serikali ni nuksi
Jamani huku sasa ni kwenda mbali sana. Pamoja na kwamba tumepewa uhuru wa habari, lakini ni hekima kuutumia uhuru huo kwa mambo ya maana na mambo ya kweli. Jakaya si mtu wa kufanya mambo kama haya hata kidogo. Andikeni vitu vya maana na vyenye kufundisha jamii, acheni kuandika uzandiki, umbea na uwongo wenye nia na lengo la kupotosha umma. Ningekuwa na uwezo wa kumshauri Raisi kikwete ningemwambia aondoe uhuru wa habari haraka sana ili kuokoa jamii kudanganywa kwa habari mbovumbovu kama hizi.