Wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi waliofaulu mtihani wa darasa la saba bila kujua kusoma na kuandika

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Idimulwa, Dec 16, 2011.

 1. Idimulwa

  Idimulwa JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2011
  Joined: May 27, 2011
  Messages: 3,384
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Philipo Mulugo nw wa elimu na mafunzo ya ufundi stad kasema wasiripoti shuleni na watakaoripoti wapewe mtihani wa kusoma kwanza

  Hivi inakuwaje mwanafunzi afaulu kwenda sekondari pasipo kujua kusoma?Kwa maelezo ya Mulugo ni wazi serikali inakiri inawezekana sasa kwanini udhibiti usifanyike kule wanakotoka badala yake wadhibitiwe kule waendako?

  Source taarifa ya habari TBC1 inayoendelea sasa hivi.

  Nawasilisha
   
 2. Mama Mdogo

  Mama Mdogo JF-Expert Member

  #2
  Dec 17, 2011
  Joined: Nov 21, 2007
  Messages: 2,866
  Likes Received: 437
  Trophy Points: 180
  Mwaka huu wizara ya elimu imetunga mtihani wa darasa la saba wa mtindo wa multiple choice kwa masomo yote ikiwemo hisabati/hesabu, na hivyo kurahisisha kuibia majibu, kukisia majibu na kuweza kushinda hata kwa bahati tu za kudra ya mtu. Kwenye mtihani wa multiple choices yenye majibu manne kwa kila swali likiwemo jibu moja sahihi kila mtoto ana 25 % chance ya kupata jibu sahihi hata kwa kukisia tu. Kama wizara inabisha basi ifanye jaribio uitoe nakala za mitihani hii kwa machinga, wapiga debe, etc pale ubungo stend na wawachague wale ambao hawakuweza kuvuka darasa la nne wawape huo mtihani, si ajabu ukapata pass rate ya 75 % au zaidi just by sheer lukcy. Tanzania ni zaidi ya uijuavyo!!!
   
 3. Ndumbayeye

  Ndumbayeye JF-Expert Member

  #3
  Dec 17, 2011
  Joined: Jan 31, 2009
  Messages: 4,806
  Likes Received: 1,053
  Trophy Points: 280
  we mama we! Hata vyuo vikuu kuna multiple choices.
   
 4. s

  sugi JF-Expert Member

  #4
  Dec 18, 2011
  Joined: Feb 12, 2011
  Messages: 1,367
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 160
  aaah bwna we hayo masihala,multiple choice kwenye hisabati?Hebu sema ni chuo gani na ni course gani ya hesabu ina multiple choice!
   
 5. C Programming

  C Programming JF-Expert Member

  #5
  Dec 18, 2011
  Joined: Nov 11, 2011
  Messages: 2,749
  Likes Received: 1,782
  Trophy Points: 280
  ww sio darasa la saba-----hata kuna wanafunzi wanamaliza vyuo vikuuuu tena degree na masters
  1.hawajui kuongea na kuandika kiingeleza kwa ufasahaaa

  2.wakiandika waanandika miandiko mibaya kuliko mtoto wa darasa la tatu

  3.hawawezi kujieleza mbele ya hadhira


  hivi.......hili swala ulioni
   
 6. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #6
  Dec 18, 2011
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Mkuu, kutokujua kiingereza si kigezo cha kuwa mtu hajasoma au hajui kuandika/kusoma. Na mwandiko mzuri kama ilivyo kwa uwezo wa kujieleza mostly ni kipaji.

  Naweza nikawa na hati mbaya kupita maelezo na nikashindwa kujieleza hadharani lakini bado nikawa kipanga.

   
 7. K

  Konya JF-Expert Member

  #7
  Dec 18, 2011
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 920
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Hivi ni ipi dhamira ya siri kali kuwapa tena mtihani hao waliofaulu? na ikitokea wakapatikana watakaofeli nini hatma yao? wataendelea na masomo ya secondari au itakuwaje?this is politics than a real situation
   
Loading...