Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na vyuo vya umma vya afya na sayansi shirikishi kwa mwaka wa masomo 2020/2021

Ndugu zangu, kuna mtoto wa dada yangu nimemfanyia application ndoto zake kubwa ni kusoma udaktari hasa hasa anapenda sana MUHAS akilala akiamka ananiuliza mjomba ntapata kweli chuo namuambia asijali, ufaulu wake ni kama ifuatavyo

O LEVEL
Civics..........B
History.......D
Geograph..B
Kiswahili....B+
English.......B+
Physics.......C
Chemistry...C
Biology.......B
Basic Mathematics....C

Amesoma Diploma ya Clinical Medicine amepata GPA ya 4.1/5.0

Na vyuo nilivyomfanyia application mpaka sasa ni vyuo 5, (UDOM (MD), UDSM(MD), MUHAS (MD), KCMC (MD), NA ST FRSNCIS CHA MOROGORO (MD) ),

Naombeni kujua kwa ufaulu huo je anaweza kuchaguliwa kusoma Udaktari kwa mwaka huu wa masomo 2020/21 Katika vyuo vya selikali kati ya UDOM, MUHAS AU UDSM?

karibuni.
Anapata, Mapema sana.
 
kwa mtu yoyote anayetaka kusoma excellent collage of health iliyopo dar es salama kwa ngazi ya cetfcat au diplom ani pm kwa muongozo...
 
Wakiosubiria kwa hamu selection za NACTE tayari wameshatoa post ila naomba kushauri kitu.

1. Kwa wale waliobahatika kuchaguliwa katika chuo fulani hongereni sana kwa kupata nafasi hiyo nyeti; munatakiwa kupambana sana kwani kozi za afya siyo za kulia bata.

2. Kwa ambao hawakubahatika kuchaguliwa na vyuo vya serikali pia musikate tamaa kwani bado muda na nafasi ipo sana japo wengine watashindwa kumudu gharama za kusoma private ila nakushauri unaweza ukafanya mpango ukaenda private then baada ya semester ya kwanza kuisha au mwaka kuisha unaweza kuhamia chuo cha serikali.

Mwisho, kwa wale waliochaguliwa Mtwara COHAS hongereni sana na kama watawepo basi wanaweza nitafuta DM.

AHSANTE

========

Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) ni chombo kilichoanzishwa kwa Sheria ya Bunge Sura 129, ili kusimamia na kuratibu utoaji wa mafunzo ya elimu ya ufundi nchini.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) waliratibu udahili wa waombaji wa Mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi Ngazi ya Astashahada na Stashahada kwa mwaka wa masomo 2020/2021. Dirisha la udahili lilifunguliwa tarehe 15 Juni, 2020 na kufungwa rasmi tarehe 15 Agosti, 2020.

Jumla ya nafasi za udahili 3,586 katika vyuo vya umma vya Afya na Sayansi Shirikishi kwa kozi za Astashahada ya Msingi, Astashahada na Stashahada zilitangazwa. Kufuatia mchakato mzima wa udahili na uchaguzi imebainika kwamba walioomba na kuwa na sifa za kuwawezesha kujiunga na Mafunzo ya Afya na Sayansi Shirikishi kwa mwaka wa masomo 2020/2021 walikuwa 14,074. Idadi ya waombaji waliochaguliwa katika programu za Astashahada na Stashahada ni 3, 354. Idadi ya waombaji wenye sifa ambao hawakuchaguliwa kwa kukosa nafasi ni 10,720.

Hivyo, Baraza linapenda kuwafahamisha waombaji na umma kwa ujumla kwamba matokeo ya uchaguzi yametoka rasmi leo tarehe 3 Septemba, 2020 na yanapatikana akaunti (profiles) za waombaji na tovuti ya NACTE (www.nacte.go.tz).

Baraza linawashauri waombaji ambao hawakuchaguliwa kutuma maombi kwenye vyuo vingine vinavyoendelea kufanya udahili hadi tarehe 15 Septemba, 2020 dirisha la udahili litakapofungwa.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA KATIBU MTENDAJI
BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)
3 Septemba, 2020
Mkuu, habari yako! Angalia PM yako.
 
Naombeni list ya vyuo vya private vya uhakika vinavyotoa Clinical Medicine sehemu yoyote Tanzania lakini visiwe vya bei ghali sana, isizidi 1.8M
Ikitokea akaweza kumudu 2.9M aende Tanzanian Training Centre For International Health Ifakara.Ni chuo kizuri mno kwa clinical medicine
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom