Wanafunzi wakifaulu wanasifia miundombinu, wakifeli wanalaumu walimu

CK Allan

JF-Expert Member
Aug 14, 2013
2,729
5,923
Tumeona baada ya matokeo ya form six kutangazwa na shule nyingi za Serikali kuingia kwenye 10 bora, sasa wameibuka wanasiasa, wakijinasibu namna matokeo hayo yalivyopatikana, wengi wanasifia majengo waliyojenga, madawati waliyonunua, na baadhi husifia jitihada za wazazi kusimamia watoto wao haswa kipindi hiki cha Corona.

Hata hivyo sioni kiongozi anayesimama hadharani na kuwapongeza walimu, hususani walimu wa shule za serikali ambao wamefanya kazi katika mazingira magumu, miaka 6 bila nyongeza ya mshahara, bila kupanda madaraja, lakini wameona potelea pote bora punda afe mzigo ufike, na umefika.

Tumeshindwa hili la maslahi ya walimu je hata kuwapongeza tu? sipati picha matokeo haya ynagetoka na wanafunzi wamefeli tungeona vioja kama sio 'viroja' walimu wangelaumiwa asubuhi mchana na jioni, sasa wanafunzi wamefaulu yanasifiwa MAJENGO! mwee!
 
Huo ndio ukweli, viko vitu vingi vinavyopelekea kufeli vilevile viko vinavyopelekea kufaulu. Wakifeli ndivyo vitakavyo orodheshwa likewise wakifaulu.
 
Back
Top Bottom