Wanafunzi wakamata wajumbe wa bodi hadi kituo cha polisi

Status
Not open for further replies.

mkama

Member
Oct 19, 2007
67
10
Sasa naanza kuamini wakati wowote wananchi wanaweza kuanza kuwashughulikia mafisad.

Hebu angalia vijana hawa shupavu wealivyowashughulikia mafisad wao.

Ama kweli Tanzania bila mafisad inawezekana


Source Mwnanchi 31.10.07

Na Lilian Lugakingira, Bukoba

WAJUMBE watano wa bodi ya Shule ya Sekondari Domilia iliyoko Wilaya ya Muleba, Kagera hivi karibuni walikamatwa, wakafungwa kamba na wanafunzi na kisha kufikishwa kituo cha Polisi Kamachumu na wanafunzi 37 wa Kidato cha Pili.


Kamanda wa polisi mkoani hapa Abdalah Mssika alisema watu hao ambao ni wajumbe wanne wa bodi akiwamo padri ambaye ni miongomi mwa wamiliki wa shule hiyo, walikamatwa Oktoba 20 mwaka huu saa saba mchana.


Kufuatia tukio hilo Jeshi la Polisi mkoani Kagera linawashikilia watu hao kwa tuhuma za kuwatapeli wanafunzi na kuwakosesha kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili ambao unatarajiwa kufanyika hivi karibuni.


Alisema sababu kubwa ya kuwapandisha hasira wanafunzi hao na kuamua kuwafunga kamba wajumbe hao wa bodi ya shule ni kutokana na kuwachangisha fedha ambazo ni karo ya shule fedha za mtihani wa taifa wa Kidato cha Pili na fedha ya usafiri wakati wakijua wanawapotezea muda kutokana na shule hiyo kutosajiliwa.


Jumla ya fedha iliyobainika kuchangwa na wanafunzi hao ni Sh 3.9 milioni kwa mategemeo ya kusoma na kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha pili katika shule hiyo hali ambayo imekuwa kinyume na matarajio yao.


Baada ya wanafunzi kugundua kuwa shule hiyo haina usajili ndipo walianzisha vurugu shuleni hapo na kutaka kujua hatima yao ya kufanya mtihani huo na kisha kuwakamata na kuwafunga kamba wajumbe hao wa bodi na kuwapeleka polisi.


Kamanda huyo alisema kuwa baada ya kufikishwa polisi walihojiwa kama shule hiyo imesajiliwa na iwapo wanafunzi hao wangefanya mtihani huo, wajumbe hao walikiri kuwa haijapata usajili na kudai kuwa walikuwa na mpango wa kuwapeleka wanafunzi hao kufanya mtihani huo katika shule za sekondari Humura na Kagondo zilizoko wilayani humo.


Alisema kutokana na uchunguzi ilibanika kweli wanafunzi hao wamelipa fedha hizo hasa kutokana na kuwa na stakabadhi zinazoonyesha kuwa shule hiyo imepokea kiasi fulani cha fedha kutoka kwa wanafunzi hao.


Alisema fedha hizo zimekuwa zikipokelewa na mkuu wa shule hiyo Mathusela Joel ambaye alidai kuwa baada ya kupokelewa zimekuwa zikichukuliwa na familia ya wamiliki wa shule.


Alisema watu hao wanatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika ili kujibu shtaka lililoko mbele yao la kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu.
 
Ni mda nzuri, sema ingeenda pale kwenye jukwaa la elimu
 
Vuguvugu za mapinduzi huanzia ngazi za chini na baadaye kuenea sehemu kubwa ya jamii.

Hizi ni dalili za mawingu, mvua yenyewe iko karibu, pale wananchi watakapoamua wenyewe kwa misuli yao, mawe yao, pinde zao na umoja wao kuwashughulikia mafisadi/wezi mmoja baada ya mwingine.

Imekuwa bahati vijana wale hawakuwafanyia madhara hao wanabodi. wametumia Busara kuwapeleka mahali pa usalama. hatari ni kama hao waliokabidhiwa watuhumiwa watakapotoa hukumu kinyume na matarajio ya wanafunzi hao. Moto utakaotokea sitaki kutabiri maana wanafunzi wanajulikana kwa kutoa adhabu mbadala.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom