Wanafunzi wajifungua saa chache kabLa ya mtihani wa darasa la 8 kuanza

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,498
9,279
VISA kadhaa vilishuhudiwa Jumatatu Mtihani wa Darasa la Nane (KCPE), ulipoanza, huku baadhi ya watahiniwa wakilazimika kufanyia mitihani yao hospitalini baada ya kujifungua watoto na mwingine akiufanyia kwenye seli.

Wanafunzi watano katika kaunti za Nakuru, Samburu na Nyandarua walifanyia mitihani yao hospitalini baada ya kujifungua watoto Jumatatu.

Katika Kaunti ya Nakuru, wanafunzi watatu walijifungua saa chache kabla ya mtihani huo kuanza.

Mmoja wa watahiniwa hao, 15, anafanyia mtihani wake katika Hospitali ya Nakuru Level Five, baada ya kujifungua mtoto wa kiume Jumatatu asubuhi.

Mtahiniwa huyo kutoka Shule ya Msingi ya Kuresoi, iliyo katika Kaunti Ndogo ya Kuresoi Kaskazini, alikimbizwa hospitalini baada ya kuanza kulalamikia maumivu.

Mkurugenzi wa Elimu katika Kaunti ya Nakuru, Bw Fredrick Osewe alisema msichana huyo alipata maumivu ya uzazi mara tu baada ya kufika shuleni.

Watahiniwa wengine ni mmoja kutoka Nakuru, aliyejifungulia katika Hospitali ya Rufaa ya Kericho na mwingine kutoka Kaunti ya Narok, aliyejifungulia katika hospitali moja mjini Nakuru.

Katika eneo la Elburgon, msichana wa miaka 17 anafanyia mtihani wake katika Kituo cha Afya cha Murinduko, Kuresoi Kaskazini baada ya kujifungua mnamo Jumapili.

Katika Kaunti ya Samburu, mtahiniwa kutoka Shule ya Msingi ya Amayian anafanyia mtihani wake katika Hospitali ya Rufaa ya Samburu.

Alipata maumivu ya kujifungua, ambapo alisaidiwa na wazazi kwa kupelekwa katika hospitali hiyo. Alijifungua kwa njia ya upasuaji. Hata hivyo, mtoto wake alifariki muda mfupi baada ya kujifungua.

Katika Kaunti ya Nyandarua, watahiniwa 11 wanafanya mtihani huo wakiwa wajawazito.

Mkurugenzi wa Elimu katika kaunti hiyo Bw Philip Wambua aliiambia Taifa Leo kwamba jumla ya watahiniwa 18 walipata mimba wakati wanafunzi walikuwa majumbani mwao kutokana na janga la virusi vya corona mwaka uliopita.

Katika kaunti iyo hiyo, mtahiniwa, 17, kutoka eneo la Njoro anafanyia mtihani wake katika seli ya polisi kwa tuhuma za kumdhulumu kimapenzi mtoto wiki moja iliyopita.

Mshukiwa huyo, aliyekamatwa wiki iliyopita, alishtakiwa kwa kumdhulumu msichana wa miaka 11 katika kijiji cha Sigotik, eneo la Nessuit, Kaunti Ndogo ya Njoro.

Alifikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Nakuru, Bi Eunice Kelley, ambapo aliachiliwa kwa dhamana ya Sh400,000 na mdhamini wa kiasi kama hicho au bondi Sh300,000 pesa taslimu.

Hakimu aliagiza mshukiwa aruhusiwe kufanyia mtihani wake katika Kituo cha Polisi cha Njoro.

Katika Kaunti ya Homa Bay, hali ilikuwa vivyo hivyo, baada ya watahiniwa wanne kufanyia mitihani yao hospitalini.

Wanne hao wanajumuisha wasichana watatu wajawazito na mvulana aliyeanza kuugua wiki mbili zilizopita.

Katika Kaunti ya Nairobi, Afisa Mkuu Mtendaji wa Baraza la Kitaifa la Mitihani (KNEC), Dkt Mercy Karogo, alitoa onyo kali dhidi ya wale ambao watajihusisha kwenye wizi wa mitihani.
 
Hongera kwa serikali yetu kutilia maanani mitihani na elimu kwa wananfunzi wa jinsia ya kike, kwamba hata ukiwa unajifungua utaletewa hapo ulipo ufanyie kwenye wodi.
Ifahamike kuteleza mara moja kimaisha haipaswi ndio iwe mwisho, huyo binti hapo anaweza akajifungua, kisha abadilishe mienendo atie bidii na hatimaye aibuke kuwa mtu muhimu sana kwa jamii.
Wengi sisi wa kiume tulikengeuka mara 1,000 lakini tukarudi njia kuu na kukomaa tu darasani mpaka mwisho... Hivyo haipaswi kuwahukumu mabinti na kuwaharibia maisha.
 
Hivi watoto wa darasa la nane huwa wana umri gani huko Kenya mpaka wanazaa watoto?
 
Nafikiri ni 14,
Ila wanawake wanabadika kibaiolojia zaidi kuliko kurefuka au umri,
Mtoto wa kike anaweza balehe hata na miaka 10 au eleven

Kama ni hivyo wanachelewa sana shule.
Miaka 10 ni abnormal kwa binti kuvunja ungo.
 
Anyway Kama wananchi(wakenya) MK254 wameridhia ni sawa lakini sioni kama ni vema kulifanya jambo hili la watoto kufanya ngono kuwa jambo la kawaida. Naishukuru serikali yetu kupinga hili jambo maana kuna maumivu makubwa sana kisaikolojia kwa mama mzazi kukaa darasani na vitoto. Vema kama ni elimu aipate kwenye mifumo mingine kama QT na vyuo lakini sio kwenye huu mfumo wa kawaida athari ni nyingi kuliko faida.
 
Hamna serikali yoyote inayoweza kuruhusu ngono baina ya wanafunzi, hapa Kenya ni hatia kwa kufanya ngono na yeyote chini ya umri, wanafunzi duniani kote wanafanya ngono kwa kwenda mbele, hamuwezi kuzuia kwa kuwatesa mabinti, tofauti yetu ni kwamba binti akiteleza na kupata uja uzito, tumeamua kutokumuongeza msongo kwa kumtupia nje nje, tunampa fursa aendelee na mapambano ya kutimiza ndoto yake hivyo akamilishe mtihani wake tu.
Jameni msichana amesomea elimu ya msingi miaka minane kisha akateleza na kupata uja uzito, halafu umnyime haki ya kufanya mtihani kwamba tumvuruge kabisa aage elimu. Huyo hapo siku ya kesho anaweza kuibuka kuwa hakimu, wakili, mhandisi n.k.
 
Hongera kwa serikali yetu kutilia maanani mitihani na elimu kwa wananfunzi wa jinsia ya kike, kwamba hata ukiwa unajifungua utaletewa hapo ulipo ufanyie kwenye wodi.
Ifahamike kuteleza mara moja kimaisha haipaswi ndio iwe mwisho, huyo binti hapo anaweza akajifungua, kisha abadilishe mienendo atie bidii na hatimaye aibuke kuwa mtu muhimu sana kwa jamii.
Wengi sisi wa kiume tulikengeuka mara 1,000 lakini tukarudi njia kuu na kukomaa tu darasani mpaka mwisho... Hivyo haipaswi kuwahukumu mabinti na kuwaharibia maisha.
Watanzania tuna Jambo la kujifunza na kuiga. Kila mtoto ana haki ya kupata elimu bila ya kujalisha makosa aliyoyafanya
 
Hamna serikali yoyote inayoweza kuruhusu ngono baina ya wanafunzi, hapa Kenya ni hatia kwa kufanya ngono na yeyote chini ya umri, wanafunzi duniani kote wanafanya ngono kwa kwenda mbele, hamuwezi kuzuia kwa kuwatesa mabinti, tofauti yetu ni kwamba binti akiteleza na kupata uja uzito, tumeamua kutokumuongeza msongo kwa kumtupia nje nje, tunampa fursa aendelee na mapambano ya kutimiza ndoto yake hivyo akamilishe mtihani wake tu.
Jameni msichana amesomea elimu ya msingi miaka minane kisha akateleza na kupata uja uzito, halafu umnyime haki ya kufanya mtihani kwamba tumvuruge kabisa aage elimu. Huyo hapo siku ya kesho anaweza kuibuka kuwa hakimu, wakili, mhandisi n.k.
Hata Tanzania hatumzuii kupata elimu kwani wote twatambua manufaa ya elimu kwake na kwa mtoto anayezaliwa.
Kinachofanyika ni kuzuiliwa kuendelea na mfumo rasmi ili kukemea na kumlinda mama pamoja na kumpa nafasi ya kumlea mtoto wake vema, kwa kufanya hivyo tumeweka mifumo mingine ambayo ni mizuri kabisa isiyo rasmi lakini yaweza kumfikisha popote atakapo kwani hata Raisi wetu Samia Suluhu amepitia kwenye mifumo hiyo mbadala.
Ujumbe unapelekwa ni kwamba mimba chini ya umri sio sahihi hivyo vijana lazima wasijihusishe. Ni Kama kusema kwa kuwa wizi ni mzuri unaongeza matajiri basi turuhusu hapana lazima ionekane dhahiri kwamba ni jambo ovu na matokeo yake ni mabaya
 
Narudia tena, mimba za wanafunzi haziruhusiwi Kenya, kile tunafanya ni kuhakikisha mwanafunzi anakamilisha mtihani wake aliojindaa, sio kumtupia nje na kumvuruga kama mnavyofanya eti mnamtuma akafuate mfumo mbadala sijui wapi huko. Hatua kama hizo huchangia sana ndoa za utotoni maana hapo binti akili zishavurugika, ndoto yake imeharibiwa.
Nakumbuka hilo liliibua sana mjadala kwenu huko, na kulijadili hutegemea unayejadili naye ni Mtanzania wa mlengo upi, nyuzi zilifunguliwa JF za kukemea hatua ya serikali yenu, lakini mlio wa mlengo wa serikali mkakomaa sana kutetea.
Changamoto la mimba za wanafunzi ni donda sugu na hauwezi kulitatua kwa kutumia ubabe, tunalo sana huku Kenya kwanza kipindi cha corona, na naona kwa Tanzania pia bado ni balaa, nacheck hapa mkoa mmoja tu wasichana 101 walitiwa mimba, na 16 wakaishia kwenye ndoa za utotoni Katika kipindi cha likizo ya COVID 19 Wanafunzi 101 Shinyanga wapata mimba
 
Kenyans have never been smart kwenye mambo yao. Utofauti wa Kenya na Kisarawe ni Jokate tu.
 
Faida ya mifumo isiyo rasmi ni mingi kuliko iliyo rasmi (kwenye muktadha huu) kwa sababu inamsaidia mama kumlea mtoto wake huku akishughulikia elimu yake. Tambua ni ngumu sana kufundishwa peke yako darasani ati kwa sababu Jana ulishindwa kufika shule sababu mtoto alikuwa anaumwa. Pamoja na mambo mengi ikiwa ni pamoja na maadili ni vema mwanafunzi (mama) mwenye mtoto atumie mifumo mingine.
Kuna vitu havihitaji degree kung'amua madhara yake. Hizi NGO ni nzuri na zinasaidia sana jamii lakini kuna nyingine lazima tuzisimamie na tuangalie mustakabali wake kwa vizazi vijavyo vya nchi yetu. Masuala yanayopiganiwa lazima yachambuliwe kwa undani kutambua dhima yake kwa miaka 50 ijayo ya nchi yetu.
No new normal in Tanzania
 
Nimeelewa tatizo lako nini, ulikurupuka kujibu bila kusoma nini kinazungumzwa kuhusu na ndio tatizo kubwa sana kwenu huko, hapa tunaongea kuhusu wanafunzi kuruhusiwa kufanya mtihani wa kitaifa licha ya changamoto za uja uzito, hawajatupwa nje, kwetu hapa hata ukiwa hospitali utaletewa mtihani ukamilishe ulichojiandaa miaka yote hiyo.
 
Anyway Kama wananchi(wakenya) MK254 wameridhia ni sawa lakini sioni kama ni vema kulifanya jambo hili la watoto kufanya ngono kuwa jambo la kawaida. Naishukuru serikali yetu kupinga hili jambo maana kuna maumivu makubwa sana kisaikolojia kwa mama mzazi kukaa darasani na vitoto. Vema kama ni elimu aipate kwenye mifumo mingine kama QT na vyuo lakini sio kwenye huu mfumo wa kawaida athari ni nyingi kuliko faida.

Tatizo ni Kufanya ngono au Kupata mimba? Kwani ukiwafukuza wenye mimba utabaki na mabikra shuleni?
 
Back
Top Bottom