Wanafunzi wajiandae na Maisha halisi baada ya kutoka vyuoni

think3r91

JF-Expert Member
May 7, 2013
469
209
Hebu vuta picha,namna ulivyosota kuipata hiyo degree yako. Miaka isiyopungua 16 imeteketea darasani! Umebeba vidumu na ufagio kama wafagiaji wa jiji ukiwa shule msingi. Umepiga jaramba maili kadhaa kuifata shule.Umekumbana na kashkashi za walimu "wanoko",ukiwaona tu bandama zilikuwa zinacheza "ndombolo" na tumbo liliunguruma kama jenereta la kiwanda.
Kasheshe ni pale ulipochaguliwa high school shule ya bweni! Enzi zile za ugali na maharage kama Segerea, wadudu ni wengi kuliko maharage! Hukukata tamaa ulivumilia kwa kuamini ipo siku tochi ya mafanikio itakumulika.
Ukupigao ndio ukufunzao,ila hukujifunza pale ulipochaguliwa chuo!

Masikini akipata....Boom lote liliyeyuka kwenye nguo! ulitaka na wewe ufanane na "watoto wa jiji"! Ulihudhuria disco zaidi kuliko lecture. Flat screen, "dance floor" vikahamia chumbani kwako! Suplimentary zikakukosa kosa, tia maji tia maji MUNGU si Athumani ukamaliza chuo na gamba lako!
Wazazi wakawa na matumaini sasa ndio muda wa kula "pensheni" mana msomi umeshavaa joho! Umerudi chuo na rundo la makaratasi tu kama gari la magazeti!Yote hayo ukawaambia wazazi yanaitwa "madesa" na uliyasoma sana kumbe ulikuwa bingwa wa kuzima moto na "vizenga"(vibomu).Ulijulikana kama mzee wa "kujilipua".

Mtaa ukakukaribisha kwa shangwe na vifijo.Haikupita wiki zile "Bata" za chuo ukaanza kuzimiss, daah! ulifulia hasa hata kifurushi uligongea cha bi mkubwa! Hizo zilikuwa salamu za rasharasha tu za kukukaribisha mtaani!
Uliowacha ambao hawakuendelea na masomo, wapo mtaani, baadhi wamepauka kama kopa la mtwara, wengine "ngoma inogile" wanang'aa kama kikalio cha stova-wamewekeza kwenye biashara zao!

Enzi zile uko chuo ulikuwa unawavalia miwani ya mbao na kujifaragua kama joka la mdimu kuwa si class yako utaongea nao nini? Sasa ndio wamekuwa wenyeji wako mtaani! Aibuuu!Umeshikwa na haya,sura imekushuka kama viraka ya nyongeza vilivyoisaliti suruali!

Kila kazi unayoomba unaambulia usaili tu!Nyingine hata usaili hutii pua! kazi moja mnaitwa alfu tano! khaa! Ulidhani mlisoma "Survival for the fittest " ili mfaulu mtihani tu?ndiyo uko maabara sasa.
Unazikumbuka pesa ulizozitumia "kula bata" chuoni,lol leo "bata" anakula wewe! "umeanza kuisoma namba" !Umepauka kama koti la mtunguo Tandika!

Mungu si athumani ukabahatika ajira mpya huko kwetu "Nanjilinji". Mshahara laki 3,huna jinsi inabidi tu uende! Miaka mitatu sasa imepita huna tofauti na uliowakuta hapo "kijijini". Zile ndoto na hekaya za chuoni za kuwa na kazi ya 1.5M, ununue gari, ujenge nyumba, uwe na "demu" mkali,zoote zimeyeyuka kama samli kikaangoni! Magari unayaona mjini tu,"mademu" wakali unaendelea tu kuwaita "shemeji"! ndio hivyo, amtunzae mpiga zumari ndie anaechagua wimbo! Utatunza nini na wewe pangu pakavu tia mchuzi!sasa umekuwa mzee wa kaunda suti za kupauka kama inzi wa chooni. Gucci unaziona kwenye filamu tu ,wewe ni magauni ya chirimeni tu!

Mjini unakuja mara moja kwa mwezi kufuata mshahara! Mwanzoni ulikuwa unaona taabu kukaa kijijini, kila weekend uko mjini, unajifanya alwatani "vascoda Gama", baada ya shida kukutandika vibao,sasa huna jeuri ya kupanda gari kila wiki! Hivi si ulisema ukimaliza chuo na kupata kazi utaunga kusoma masters?Vipi kwani vyuo vimefungwa?

Haya ndio maisha ya vijana wengi! Hudhani mtaani kuna asali na maziwa wakishamaliza degree zao! Mtaani kuna hitaji zaidi ya hiyo degree!Kuna wakati degree inabidi uiweke pembeni ili ufunike kombe "mwanaharamu "apite!Lakini pia mtaa unakupokea kama ulivyojiandaa nao! kama kwa kutumia bumu lako ulijibana na kuhifadhi kidogo basi mtani utaziona fursa za kuwekeza hicho kidogo ulichonacho.Kama ulikula bata tu na mtaani umerudi na mawigi,kucha feki na "modo" za kuvaa mlegezo basi mtaa hautakuonea aibu, utakupa swaga zake.Nguo ya ijumaa hufuliwa Alhamisi #JIPANGE jombaaaaaaaaaa

Source: thebridge tz
 
Dah! Mshikaji una majungu wewe? Kwani elimu yako ni gani?
Huyo darasa la saba sasa anajisafisha ujinga wake uonekane wa maana na degree kuonekana haina mpango

Sasa nikwambie tu mtoa mada kua elimu itabaki kua na umuhimu hadi dunia iishe kwa nini usijiulize serikali kuchonga madawati na siyo hizo benchi mnazokalia kuchezea draft na kuandikia mikeka??
 
Msiogope vijana kama upo chuo na wewe kijana usiogope tumia ujana wako uwezavyo cha msingi ujue tu upo chuo kusoma pia tambua Kuna maradhi ukijua hayo basi jiachie kadri uwezavyo

Kwani maisha ya chuo ndio unamalizia ujana wako na ujinga wako wewe kama furaha yako mziki nenda
Kama furaha yako mitungi itandike kisawa sawa ukiwa na mda
Kama vaaa nguo nzuri nzuri nunua tu
Fanya unalohisi linakupa furaha

Kwanini nasema jiachie maisha ya chuo ni mafupi pia hiyo ndio hatua yako ya mwisho kufanya upuuzi jamii ikakuchukulia pouwa na ukasaidiwa kisa tu mwana chuo utoto unakusumbua

Pia Ukimaliza chuo unaanza maisha mapya maisha yakuonekana wewe msomi ukiwa mtu wa kujiachia sana jamii itakushangaa pia utapata stress kwani uku katika maisha ya mtaa watu wanatimiza malengo ili badae wafurahie maisha upya

Mfano kujenga kutunza familia, kama vile kusomesha nk hivyo basi maisha ya mtaa yanaitaji nizamu ya pesa ya hali ya juu kwani jamii itakutegemea so mchezo mchezo wa kijinga club pamba ukiendekeza tu unakuwa wa mwisho

Hivyo basi mda wa kufanya upuuzi huo ni chuo cha msingi tu jua chuo umeenda kusoma so Piga shule ukipata mda jiachie uwezavyo kwani tuna ushahidi waliojibana kujiachia vyuoni leo hii ni shida katika familia zao

Mtu msomi ana mke na watoto analala bar anakesha club ofisi nzima wanawake katongoza yani full matatizo si kwa wanaume hata wanawake wengi ambao chuo hawakujiachia wakija mtaani endapo mungu akawasaidia kupata ajira basi wanamini ule upuuzi walioukwepa chuoni wa bata sana basi mda huo wao wanajira ndio mda sahihi kumbe wapi ndio maana ndoa nyingi zinavunjikq single mother wamekuwa wengi sababu waliluka stage

Endapo wangejiachia vyuoni wangepata some kuwa pesa inaitaji heshima kwani zile pasi ndefu mda boom umechezea limeisha au ile pesa toka home imekata unavyosota unakuwa katika somo tosha
 
Mi bana hela yangu situmii ki f*la f*la hata siku moja....tokea naanza chuo hivi....kila nikiaangalia maisha ya kitaa huwa nlikua nashikwa na hofu sanaa....and that i was fearing to be a failure/looser hyo pekee ilinifanya niweze kufanya maamuzi ya msingi sanaa in my life na shule sikufanya mchezo kabisaa..unapiga msuli mpaka we mwenyewe unaji appreciate.

Asikwambie mtu mwanamme miaka hii usipokua na hela...dharau kejeli zote kwako. Inabidi ufanikiwe to tha point watu wasikuchukulie poa kabisaa. Always tufanye kazi kwa nguvu na akili zote na usimtegemee binadam yeyote yule (Ur always gana be happy).
 
Msiogope vijana kama upo chuo na wewe kijana usiogope tumia ujana wako uwezavyo cha msingi ujue tu upo chuo kusoma pia tambua Kuna maradhi ukijua hayo basi jiachie kadri uwezavyo

Kwani maisha ya chuo ndio unamalizia ujana wako na ujinga wako wewe kama furaha yako mziki nenda
Kama furaha yako mitungi itandike kisawa sawa ukiwa na mda
Kama vaaa nguo nzuri nzuri nunua tu
Fanya unalohisi linakupa furaha

Kwanini nasema jiachie maisha ya chuo ni mafupi pia hiyo ndio hatua yako ya mwisho kufanya upuuzi jamii ikakuchukulia pouwa na ukasaidiwa kisa tu mwana chuo utoto unakusumbua

Pia Ukimaliza chuo unaanza maisha mapya maisha yakuonekana wewe msomi ukiwa mtu wa kujiachia sana jamii itakushangaa pia utapata stress kwani uku katika maisha ya mtaa watu wanatimiza malengo ili badae wafurahie maisha upya

Mfano kujenga kutunza familia, kama vile kusomesha nk hivyo basi maisha ya mtaa yanaitaji nizamu ya pesa ya hali ya juu kwani jamii itakutegemea so mchezo mchezo wa kijinga club pamba ukiendekeza tu unakuwa wa mwisho

Hivyo basi mda wa kufanya upuuzi huo ni chuo cha msingi tu jua chuo umeenda kusoma so Piga shule ukipata mda jiachie uwezavyo kwani tuna ushahidi waliojibana kujiachia vyuoni leo hii ni shida katika familia zao

Mtu msomi ana mke na watoto analala bar anakesha club ofisi nzima wanawake katongoza yani full matatizo si kwa wanaume hata wanawake wengi ambao chuo hawakujiachia wakija mtaani endapo mungu akawasaidia kupata ajira basi wanamini ule upuuzi walioukwepa chuoni wa bata sana basi mda huo wao wanajira ndio mda sahihi kumbe wapi ndio maana ndoa nyingi zinavunjikq single mother wamekuwa wengi sababu waliluka stage

Endapo wangejiachia vyuoni wangepata some kuwa pesa inaitaji heshima kwani zile pasi ndefu mda boom umechezea limeisha au ile pesa toka home imekata unavyosota unakuwa katika somo tosha
huo ndio ushauri wa kipuuzi sana
 
Huyo darasa la saba sasa anajisafisha ujinga wake uonekane wa maana na degree kuonekana haina mpango

Sasa nikwambie tu mtoa mada kua elimu itabaki kua na umuhimu hadi dunia iishe kwa nini usijiulize serikali kuchonga madawati na siyo hizo benchi mnazokalia kuchezea draft na kuandikia mikeka??
Dah... chief elimu si lazima kukaa darasani. Hata kwenye bao au draft unaweza kupata elimu yenye manufaa kuliko hiyo ya kukaa darasani. Ukiwa na PhD halafu haikusaidii wewe wala wengine kufanya maisha yawe rahisi basi ni sawa kabisa na yule asiye na KKK
 
Back
Top Bottom