Wanafunzi wagoma wakidai kudhalilishwa kingono na walimu, polisi wawatawanya kwa mabomu

NGolo Kante

Member
Feb 28, 2017
80
131
Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro limelazimika kutumia mabomu kuwatawanya wanafunzi wa shule ya sekondari Majengo baada ya kugoma kuingia madarasani kwa kile walichodai ni kudhalilishwa kingono na kuchaniwa nguo na walimu wao.

Hatua hiyo imekuja mara baada ya wanafunzi hao kugoma kuingia darasani, kukataa kula chakula na kukusanyika mbele ya ofisi ya Mkuu wa shule hiyo huku wakitaka uongozi wa shule kufanya utatuzi wa sakata hilo.

Wakizungumza na Mtanzania Digital leo Ijumaa Februari 8, baadhi ya wanafunzi hao wamesema wamechoshwa na vitendo hivyo vya kikatili na udhalilishwaji wa kingono huko wakilitaka jimbo Katoliki la Moshi na Waziri wa Elimu Joyce Ndalichako kuingilia kati.

Kiongozi wa serikali ya wanafunzi wa shule hiyo Gasto Lucas, amesema kuwa vitendo hivyo wanavyofanyiwa ni vya kudhalilisha utu wao kinyume na taratibu za nchi na wanapoulizia inakuwaje vitendo hivyo vinafanyika wanapigwa.

Kwa upande wake mwanafunzi Anithe Asenga amesema walimu wamekuwa wakiwanyanyasa wanafunzi wa kike na kuwadhalilisha huku wakichawachania sketi zao mbele na sehemu za kwenye mapaja.

“Tangu tumefungua shule hii ni sketi ya tatu nachaniwa tu jamani na sketi nimeshoneshewa hapa hapa shuleni nimelipia sh.20000 kwa kila sketi, “amesema.

Aidha akizungumza kwa niaba ya uongozi wa shule ya sekondari Majengo Mwalimu Mukindia Stephen amesema kuandamana siyo suluhisho hivyo aliwataka wanafunzi hao watawanyike warudi majumbani na uongozi wa shule utakaa na uongozi wa serikali ya wanafunzi kuzungumzia suala hilo.

Chanzo: Mtanzania
 
ningekuwa mie Rais ningepiga fimbo 50 hadharani mwalimu anayedhalilisha mwanafunzi ki ngono!

halafu ningeagiza kila siku mwalimu huyo achapwe viboko 5 mbele ya wanafunzi kwa sku 20
akibaki kufundisha bas atakuwa amekiri kosa
bila ya kujua sababu ni nini?

shida mimi nimehisi "ni sketi fupi" lakini kama zinashonwa hapo na vipimo wanafahamu kwa nini uichane

kama zinashonwa hapo wana haki 100% kulalamika, ila kama zashonwa mtaani wajirekebishe washone zinazo endana na taratibu za shule.
 
S
Mfano mwanafunzi kavaa sketi Fupi, kumchania nguo kwenye mapaja ni kuongeza tatizo au kupunguza? Au wakishawachania wanawapa na khanga za kujifunga?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimesoma hapo form one mpaka A level miaka ya nyuma kdg, Sina mfano mkuu (picha) na walichokifanya ni udhalilishaji mkubwa sana sana na sheria inabidi ichukue mkondo wake hapo wangetafuta adhabu nyingine
 
Ni bora wangewasimamisha masomo kwa Kosa la kuvaa sketi Fupi kuliko kuwadhalilisha kwa kuwachania.

Sent using Jamii Forums mobile app
hahaahha mkuu acha utani basi, kuvaa sketi fupi ni mwanzo wa kujidharilisha ni mwanzo wa kuidharilisha shule pia

umeshonewa sketi ndefu unaikata unataka fupi yenye kukuweka wazi wazi ukiwekwa wazi et umedharilishwa duuuh
 
Hakuna excuse yoyote ya kumchania mtoto nguo..huo ni udhalilishaji.
Kama haifai mwambie atoe harafu mpatie adhabu inayostahili hata ikibidi afukuzwe shule.
Lakini kuchana nguo mbele ya wenzake sio poa hata kidogo.
Mi Africa sijui tukoje..tunakuwa na mambo ya kiajabu ajabu.
 
Sometimes Wanafunzi Huchukuliwa Kama Watoto Wadogo Na Hutumiwa Kuchafua Walimu Wenye Mitazamo Fulani Kinzani Hasa Ya Kisiasa Au Namna Fulani Ya Chuki Ili Kuwakomoa. Issue Za Wanafunzi Ni Very Sensitive Wanasikilizwa Hata Katika Upuuzi Wao. Ufanyike Uchunguzi Wa Kina Kabaini Ukweli Wa Malalamiko Yao Isije Ikawa Wamekosa Nidhamu Na Adabu Kuchafua Walimu Wao
 
shida ya Watanzania ni uongo, mwalimu hawezi kukuchania sketi/suruali bila sababu lazima kuna sababu.
Na hii umesema kweli mie kipindi nikiwa A level kuna migomo mingine tulikuwa tunaifanya kw makusudi kabsa na aliwahi kuja mkuu wa wilaya tukaanza kuwasingizia walimu kwa mambo ambayo hawafanyi... Wanafunzi pia huwa wanalazimisha uhuru fulani wanasahau kuwa wao ni wanafunzi!! Na hakika wakifanya uchunguzi yawezekana ikawa kweli ama uongo.... Mwanafunzi nae siku zote ni mwanafunzi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom