wanafunzi wafukuzwa kwa kukataa kula mavi ya watu

TAIKUBWA

Senior Member
Jan 20, 2008
115
1
Wanafunzi 1,200 wafukuzwa Shule

2008-05-06 10:35:51
Na Patrick Chambo, PST Mwanga


Wanafunzi zaidi ya 1,200 wa Shule ya Sekondari ya Kifaru iliyopo wilayani Mwanga wamefukuzwa baada ya kupinga adhabu ya kushika kinyesi cha binadamu kilichokuwa kimehifadhiwa kwenye ndoo ya maji.

Habari zimesema kwamba kitendo chao cha kukataa adhabu, kilisababisha wenzao wachapwe, hali ambayo ililipusha vurugu zilizosababisha uongozi wa shule kutimua wanafunzi karibu wote.

Mkuu wa wilaya ya Mwanga, Bw. Gordan Lugimbana aliithibitishia PST jana kuwapo kwa tukio hilo na kuongeza kuwa Kamati ya Ulinzi na Usalama imeunda tume kuchunguza madai ya wanafunzi kufukuzwa.

Mwandishi wa habari hizi alipofika shuleni hapo ili kuonana na uongozi wa shule hakufanikiwa kutokana na wanamgambo kutanda na kutoruhusu mtu kukaribia eneo hilo.

Wanafunzi hao walifukuzwa katika shule hiyo ambayo ni ya serikali, Jumamosi iliyopita, lakini Mkuu wa Wilaya amewataka wazazi kuwarejesha shuleni mara moja kwa kuwa uamuzi wa kuwafukuza shule haukuzingatia sheria.

Hata hivyo, alisema amesikitishwa na taarifa kuwa baadhi ya wanafunzi walilala porini, wengine nyumba za kulala wageni wakibangaiza nauli za kurudi nyumbani baada ya kufukuzwa, hali ambayo alisema ni hatari.

`Hata sisi tumeelezwa kuwa walilazimishwa kushika kinyesi cha binadamu katika ndoo` Kama ukweli utabainika, walimu waliotoa adhabu hiyo watachukuliwa hatua za kisheria kwa kuwa ni kinyume cha haki za binadamu,`` alisema mkuu huyo wa wilaya.

Hatua hiyo ya walimu imeelezwa kuwa imetokana na mwanafunzi mmoja kujisaidia haja kubwa katika `korido`.

Hatua hiyo inadaiwa iliwafanya walimu wawalazimishe wanafunzi kuweka kinyesi hicho katika ndoo, kisha wakatoa adhabu hiyo ya kukishika kama njia ya kukomesha kitendo hicho kisirudiwe tena.

Ilidaiwa kuwa wanafunzi walijipanga kwenye mstari na kila mmoja akatakiwa kuweka mkono ndani ya ndoo iliyokuwa na kinyesi hicho na majimaji.

Kutokana na adhabu hiyo, habari zimedai kwamba wanafunzi hao waligoma, wakaanzisha vurugu ikiwa ni pamoja na kuvunja samani za shule ikiwemo kompyuta, na hivyo kusababisha hasara ya zaidi ya Sh. milioni nane.

PST ilipotembelea maeneo hayo ya kijiji cha Kifaru ilishuhudia wanafunzi wengi wakihaha kutafuta sehemu za kulala na wengine nauli kwa wale wanaoishi mikoa ya Tanga, Arusha, Manyara na Kilimanjaro.

Inadaiwa kuwa baadhi ya wanaume `wapuuzi` walifanikiwa kuwarubuni watoto wa kike kwa kulala nao katika nyumba zao na wengine nyumba za kulala wageni wakiwaahidi kuwapatia nauli na chakula siku ya Jumapili.

PST ilishuhudia baadhi ya watoto hao wakizagaa katika nyumba za kulala wageni eneo la Mwanga.

Hili ni tukio la pili kufanyika katika shule za serikali mkoani Kilimanjaro ambapo tukio jingine lilitokea katika shule ya sekondari ya Lyamungo ambapo viranja wa shule hiyo waliokuwa wakivuta bangi walikuwa wakiwaamsha wanafunzi wenzao usiku na kuanza kuwacharaza viboko kutokana na uongozi mbovu wa shule, hali iliyopelekea machafuku na wanafunzi kufukuzwa shule.

SOURCE: Nipashe
 
Back
Top Bottom