wanafunzi waandamana | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

wanafunzi waandamana

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Faith, Aug 1, 2008.

 1. Faith

  Faith Member

  #1
  Aug 1, 2008
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 52
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  niko hapa jirani na jengo la mkuu wa mkoa, naona na kusikia wanafunzi wakiandama kupinga nauli ya mia
  wanaimba nyimbo za kumpondea kandolo
  naona na wengine wamechukuliwa na defender ya polisi
  mpo wana habari?
   
 2. BadoNipo

  BadoNipo Senior Member

  #2
  Aug 1, 2008
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 175
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  hata me nimeona hawa wadogo zetu, bora watafute haki yao,
   
 3. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #3
  Aug 1, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Hakika ila bila kibali wataumizwa
   
 4. Faith

  Faith Member

  #4
  Aug 1, 2008
  Joined: Jul 9, 2008
  Messages: 52
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hofu yangu ni kua HAWANA KIBALI KWANI WALINYIMWA!, sasa hii inaweza kuwaletea tatizo, na wanafunzi wenyewe wengi ni wa msingi na sekondari (lkn ni km o'level) mana wadogonaona na mabomu yanatupwa hapa, watoto wanakimbizwa
  nitajuza baadae
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Aug 1, 2008
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Hivi, hao wanafunzi wana haki gani, kwa taarifa yenu sheria za nchi zinasema walipe nusu ya nauli ya mtu mzima... kwa maana kuanzia sasa walipe 200/- per normal route...

  Lakini hata hivyo SUMATRA wamepunguza to 100/- Tsh. nani asiyejua kwamba mafuta yamepanda?

  Hao wenye dala dala ambao wanalipa kodi etc. kwa nini wabebeshwe mzigo wao...

  Ndio muda muafaka wa kujua kwamba kuzaa si tabu... bali kazi kulea na tujiandae kuwalipa watoto wetu.
   
 6. Mzee wa Gumzo

  Mzee wa Gumzo Senior Member

  #6
  Aug 1, 2008
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni haki ya kiraia but i think lazima serikali itafute njia ya kukabiliana na kupanda kwa bei ya mafuta.

  Am sorry kwa wanetu na wadogo zetu but i think they should'nt.Things are worse on both sides.
   
 7. H

  HKiboka Member

  #7
  Aug 1, 2008
  Joined: Feb 6, 2007
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mabomu ya nini kwa watoto wadogo? mbona hata Ulaya watu wakiandamana huzuiwa tu na si kuwapiga mabomu ya machozi! Lakini ndio njia inayotumika sana hapa Afrika, kupiga na kujeruhi. Na hao askari watoto wao hawamo kwenye maandamano?
   
 8. M

  Malila JF-Expert Member

  #8
  Aug 1, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Kweli kila mtu ana haki ya kumsomesha mtoto ktk shule anayoipenda,au yenye sifa nzuri(kulingana na anavyoona yeye),au anayomudu. Sasa kuna Watz wenzetu hasa Dar; mtoto wa darasa la kwanza(umri 6/7yrs) anatoka Tabata kisukulu anakwenda kusoma s/msingi Kawe Ukwamani, au mtoto(7yrs) anatoka Gongo la Mboto anakwenda kusoma s/msingi Mbagala rangi tatu.Wakati unajua kuwa mtoti/kijana wako hatamudu ngalambe za mabasi unategemea nini? Ni kweli shule nyingi za serikali zinaktisha tamaa sana.

  Kwa sekondari ni vigumu kidogo kwa sababu shule ni chache ktk maeneo yetu,itabidi tupambane hivyo hivyo.
   
 9. NaimaOmari

  NaimaOmari JF-Expert Member

  #9
  Aug 1, 2008
  Joined: Sep 25, 2007
  Messages: 807
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Asubuhi one of the students was talking kwenye TBC ... he said kwamba theres someone who wanted to start up a company ya transport for students ... i've forgotten the abbreaviation and the details ... ameomba kibali siku nyingi but has not received any response

  If someone watched please help me out ...

  I really wonder kama kweli mtu kajitolea to save the situation na the same govt inamnyima kibali .. what do you expect

  Kasheshe hao watoto wameshapigwa mabomu tayari wengine wamefungwa
   
 10. Kevo

  Kevo JF-Expert Member

  #10
  Aug 1, 2008
  Joined: Jun 12, 2008
  Messages: 1,332
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nilishasikia siku nyingi ila sijui kama alipatiwa ruksa.
   
 11. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #11
  Aug 1, 2008
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Hiyo issue ya huyo muhindi aliotaka kuleta mabasi ya wanafunzi aliomba kusamehewa kodi zote kuanzia import,duty, mpaka income tax sasa serikali ikaona labda ni ujanja flani ikagoma
   
 12. Ibrah

  Ibrah JF-Expert Member

  #12
  Aug 1, 2008
  Joined: Mar 22, 2007
  Messages: 2,721
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145

  Sasa kama watoto wa shule nao wameanza kuandamana bila kuogopa vitisho vya Polisi basi tunaelekea kubaya kabisa! Huko tunakokwenda Watoto wa Chekechea nao wataanza kuandamana, sijui Polisi watawapiga virungu nao?

  Naona Polisi wetu wamekosa cha kufanya kabisa na sasa wanashindana na watoto wa shule; ni upotevu wa raslimali za taifa, au stock ya mabomu ya machozi inakaribia ku-expire? Kwani RPC angruhusu maandamano ingekuwaje? Wangeandamana na baadaye kutawanyika wenyewe baada ya kufikisha ujumbe wao.

  Yaani mambo mengine yanazuilika kirahisi sana lakini kwa kuwa polisi wetu wamezoeshwa kutumia nguvu hata mahali pasipohitaji nguvu; Busara ndogo sana wanakosa! Ni vema serikali ijue hao ndo wapiga kura wa Uchaguzi wa 2010.
   
 13. H

  Haika JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2008
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,318
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  mimi naona wazazi walipe tu hizo nauli. kama tumekubali school fees kupanda katika shule za serikali bila kulalamika kuwa wanafunzi watashindwa inakuwaje haya mabasi ya wafanyabiashara, wajasiriamali inawezekanaje?
   
Loading...