Wanafunzi wa Vyuoni na madesa/vibomu, tutafika kweli?

nipeukweli

JF-Expert Member
Jul 16, 2012
656
348
habari zenu wadau wa Jukwaa hili la Elimu.

leo maoni yangu yanaelekea kwa wanafunzi wa elimu ya juu na suala zima la matumizi ya madesa yanayojulikana vilevile kama vibomu.
madesa hutumika sana na wanafunzi katika nyakati tofauti tofauti, mfano kuandika assignments na reports (za field work au research)...hili sitoligusia leo
aina ya madesa ninayotaka kuigusia leo ni vile videsa vinavyotumika na wanafunzi in the course of an exam. katika utaratibu wa elimu ya juu, ikithibitika kuwa mwanafunzi aliingia katika chumba cha mtihani na kidesa, anakuwa discontinued almaarufu kama kupigwa DISCO.

pamoja na kuwepo kwa adhabu hiyo, wanafunzi bado wanatumia vibomu, tena sana tu. mtu anadiriki kujiandika terial kwenye mapaja, anaandika kwenye handkerchief, kwenye vikaratasi n.k ili waweze kuvitumia wakati wa mtihani. wengine huviweka toilet ili akiomba ruhusa ya msimamizi wa mtihani kwenda msalani, akaperuz.

hivi hali hii itakwisha lini? je utegemezi kwa madesa unatengeneza wahitimu wa namna gani? sadly, kadiri miaka inavyosonga hali inazidi kuwa mbaya... kwa hali hii ya kutegemea videsa kwenye exams tutafika kweli? ni kizazi gani cha graduates tunachotengeneza?

karibuni kujadili...
 
Huu mchezo upo udsm cass na law, coet hawana. Ila kiukweli watu wanauwezo lakini cha kushangaza wakishafika chuo uwezo unapotea na wanaishia kudesa, mi nadesa sana katika ripoti yani nabadili jina reg.no
 
Back
Top Bottom