Wanafunzi wa Vyuo wapewa likizo ya mapema ikiwa ni njia ya kudhohofisha maandamano yao

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Wizara ya elimu ya juu nchini Algeria imeamuru likizo ya mapema kwa wanafunzi wa vyuo vikuu katika hatua ya kujaribu kuyadhoofisha maandamano yanayoendelea.

Wanafunzi hao wamekuwa wakiandamana kwa zaidi ya wiki mbili sasa kupinga hatua ya Rais Abdelaziz Bouteflika ya kutaka kugombea muhula wa tano.

Wizara ya elimu ya juu imetangaza kwamba likizo hiyo ya mapema itaanza leo Jumapili na kuendelea hadi Aprili 4.

Kwa kawaida likizo hiyo huwa ya wiki mbili na huanza tarehe 21 mwezi Machi hadi Aprili 5 kila mwaka. Walimu na wanafunzi kutoka kwenye vyuo vikuu kadhaa wameanza mgomo, huku wengine wakiahidi kuanza mgomo leo hii Jumapili.

Rais Bouteflika ambaye ni nadra kuonekana hadharani tangu augue kiharusi mnamo mwaka 2013 ameahidi kutokamilisha muhula wake iwapo atchaguliwa tena katika uchaguzi wa Aprili 18, lakini wanafunzi wa vyuo vikuu wanaipinga hatua hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom