Wanafunzi wa Vyuo Wafundishe kwa muda! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wa Vyuo Wafundishe kwa muda!

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Kamundu, Oct 26, 2009.

 1. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Tanzania kwa sasa inatatizo la walimu na kitu cha kushangaza serikali inasomesha wanafunzi wengi kwenye vyuo vikuu ambao hawatalipa mikopo yao. Mimi ningeshauri serikali kwa wakati huu wa uhaba wa walimu wange weka ulazima wa wanafunzi wa vyuo wa mwaka wa mwisho kufundisha kwa miezi sita tu kabla ya kupewa vyeti vyao. Inashangaza watanzania tunafikiria kila kitu serikali ifanye, lakini serikali inatakiwa kuweka sera kwa Watanzania kusaidiana wenyewe sioni sababu ya wanafunzi wa vyuo vikuu ni kwanini wasifundishe kwa sasa wakati serikali inafanya mikakati ya kusomesha walimu.

  Tutapiga siasa lakini kama kizazi kijacho hakina elimu Tanzania itatawaliwa na vijana wa nje.
   
 2. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #2
  Oct 26, 2009
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,606
  Likes Received: 3,905
  Trophy Points: 280
  Mkuu, uamuzi na mawazo mazuri sana.
  Ila kufundisha kwa 'emergency' sitation kama hii, haihitaji walimu tu.
  Mtu yeyote mwenye elimu anaweza kujitolea kwenda shule yoyote ile na akafundisha bure, na hii inabidi tuanze na wewe.

  Huwa sipati picha ya nini wasomi tunaifanyia nchi hii, ila Kamundu, ujue ubnafsi wetu na roho za umimi ndio zinatufikisha hapa. Ubinafsi huu unaweza kutokana na matabaka tuliyo nayo na aina ya siasa tunayoipitia.

  Ukisemacho kingeweza kutekelezeka kirahisi kama nchi ingekuwa ya kijamaa.Ubepari hauruhusu hivyo, maana ubepari unaanzia ndani ya moyo (no free lunch)

  Nchi ina system mbili za elimu International school-matajiri
  English academ-kipato cha kati
  Kiswahili(kayumba)- maskini
  Kila mtu anawaza kuwa group la pili au la kwanza, watu wanapigana na kuhsindana hili wawe na maisha mazuri, ya kushindana na kuhodhi mali na utajiri.

  Ikifikia hapo, hakuna atakayeweza kufundisha bure, hata kama watalipwa na serikali ni sh. ngapi??

  we have challenge mkuu, kutokana na culture yetu, ndiyo maana huwa nasisitiza kiongozi mzuri ni yule anayejua haya matatizo na kutafuta mbinu ya kuyatatua
   
 3. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Waperoya,
  Nahukuru Mtanzania mwenzangu umeona hili mimi sidhani kama ubepari ni tatizo sijawahi kuona watu wanaojitolea kama wamarekani na ni "wabepari". Kuna watu wengi sana wa Kimarekani wanachukua likizo na kwenda kufundisha nchi zinazoendelea kuanzia wafanyakazi hadi ma professor. Nakumbuka nilivyokuwa Ilboru tulikuwa na walimu wengi wa nje. Mimi natakiwa nilitolee lakini ningependa Serikali ianzishe kitu kama peace corp. Lakini pamoja na yote haya tulikuwa na JKT ni kwanini tusiwe na hili swala la muhimu kwa karne hii.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nadhani hii kitu si kwa wanafunzi peke yao tupo wengi na tunaweza kusaidia sana kuijenga nchi yetu ambayo mafisadi wanaimaliza. Mimi najipanga na mwezi januari lazima niombe kibali wizara ya elimu ili nifundishe sekondari itakayokuwa karibu na ofisini kwangu. Nawaomba watanzania kila mtu kwa fani yake tuvamie hii sekta ya elimu na kutoa ujuzi wetu, baada ya miaka kumi mabadiliko tutayaona.
   
 5. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #5
  Oct 26, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Wazo lako zuri sana tena sana ,ila mie kwa kuongezea juu ya wazo lako ningependelea iwe hivi-
  Badala ya mhitimu kulipa mkopo inabidi mhitimu kokote anakoajiliwa awe na masaa ya ziada ya kufundisha shule yoyote kwa mda ambao atakamilisha deni la mkopo.

  Nafikiri si lazima kulipa mkopo kama serikali ilivyojipanga ila kuulipa mkopo kwa staili ya kufundisha nafikiri utakuwa ulipaji wenye efficiency nzuri zaidi.
   
 6. s

  smalnama Member

  #6
  Oct 26, 2009
  Joined: Oct 6, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  WAZO zuri. Ila tusisahau kufundisha ni fani. You need to be trained to teach. Labda vyuo viongeze kozi ya muda kwa wahitimu, kama mwezi ili wahitimu wajue basics za kufundisha. vinginevyo itakuwa chaos mashuleni.
   
 7. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Pamoja kufundisha ni fani lakini kwa asilimia kubwa mhitimu wa chuo kikuu ataweza kufundisha bila kuhitaji kozi nyingine.Ni wazo
   
 8. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Hii ya wanafunzi wa vyuo kufundisha kwa muda na watu kujitolea sijui kama itawezekana, ni wazalendo wachache watakaokubaliana na hili.


  Nafikiri ni vizuri serikali kuboresha hii sector ya ualimu, ili watu wakimbilie huko. Wapange mishahara mizuri kwa walimu.Watu wengi tu wanasomea ualimu, ila wanaobaki kwenye hii kazi ni wachache wengi wanakimbia na kwenda kufanya kazi nyingine.

  Walimu wengine wanaamua kukimbilia International/academy school maana huko angalau pato lao zuri.Kwa mtindo huu kama serikali haitaki kuboresha hii sector ya ualimu, kila siku watakuwa wanapiga kelele kwa ukosefu wa waalimu.
  Serikali yetu ina pesa na inaweza kuboresha hii sector badala ya hizo pesa kwenda kwa mafisadi.
   
 9. M

  MkamaP JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2009
  Joined: Jan 27, 2007
  Messages: 7,313
  Likes Received: 1,452
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu kujitolea ni kazi ngumu hasa ukizingatia asili yetu.Lakini mimi nashauri kuhusu mkopo badala ya kulipa mkopo watu wafundishe hata kama ameajiliwa kwingine awe na kipindi shuleni.

  Kama hataki kufundisha basi alipe mkopo strictly.
   
 10. K

  Kamundu JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2009
  Joined: Nov 22, 2006
  Messages: 2,112
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Kama umepata mkopo wa serikali na hutaki kufundisha kwa miezi sita basi hupewi cheti mbona tulilazimisha watu waende JKT tumepata nini? Watoto hawana walimu na serikali inatumia pesa kusomesha wanafunzi wengi ambao hawalipi madeni na kukimbilia nje, kuna madactari wengi tu wako Botswana na USA na wamesoma bure kwa gharama zaidi ya $20,000 siwangeweza kufundisha Biology!. Mimi sioni ubaya wa serikali kuzuia vyeti kwani hii ni kama vita sasa nchi nyetu haitaweza kuendelea kwa madini au gas pekee inahitaji Human Resources.
   
 11. O

  Ogah JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hili suala la kujitolea ni muhimu sana.......JF Foundation?
   
 12. Gudboy

  Gudboy JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 799
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Jamani nashauri tuanze na hapa wana JF itajenga sana heshima na pia hata mafisadi wataipenda hii JF maana itakua ni mfano wa kuigwa na yenye tija kwa jamaii na sio yenye kusema huku haionyeshi mfano, charity begins at home, JF is our home and TZ is our country mazee
   
 13. Pretty

  Pretty JF-Expert Member

  #13
  Oct 27, 2009
  Joined: Mar 19, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 135
  Basi mfanye kweli wazalendo, isiwe typing tu kwenye keyboard halafu matendo zero.
   
 14. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  What a thread!!!


  Asante sana Mzalendo Kamundu kwa thread hii; na wale wote waliochangia tayari. Kuna yule aliyezungumzia wamarekani pamoja na ubepari wao. Huu ni mfano mzuri sana. Community service kwao ni kitu wanachokipa kipaumbele cha hali ya juu. Haya ni mawazo ya kujenga kweli kweli kwa sababu yanalenga mwananchi wa kawaida kabisa.

  Nadhani kama kukiwa na utaratibu mzuri kama alivyosema Ogah (wazo la foundation), hii kitu inaweza kuanza taratibu na baadae lobbying ikafanyika serikalini ili iweze kusimamia uendeshaji wake.

  Inabidi pawepo na mtaala pia wa kufundishana uzalendo wa kuipenda nchi yetu pamoja na maendeleo yake (Tuwe na moyo wa kujitolea pale tunapopata fursa ya kufanya hivyo bila malipo). ... Ni kwa vile nchi kama Amerika zina vitu kama hivi, na kila mgeni anayeingia hataki kuondoka maana anahisi amefika nchi ya ahadi.

  Sasa hivi tunaongelea uhaba wa walimu katika taasisi mbalimbali za elimu ya msingi hadi ya vyuo vikuu; lakini je ni walimu wangapi wa vyuo vikuu wamekuwa wakilipiwa na serikali na kupata mishahara yao kila mwezi wakiwa masomoni, lakini wakishamaliza masomo yao wanaamua kujilipua huko huko ili waendelee kula neema zilizoasisiwa na wenyeji wao. Kuna haja ya kubadili system tuliyo nayo ili kila mmoja wetu atambue kwamba maisha mazuri hayako Amerika au Uropa tu.

  Ubinafsi ndiyo mwishowe unazaa ufisadi.
   
 15. T

  Tom JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2009
  Joined: May 14, 2007
  Messages: 472
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wanafunzi wanatakiwa kujilipia lakini kama wamekopa ada hamna sababu ya kumlazimisha mtu kwa kumyima cheti maana deni halifutwi.
  Hata kama wanavyuo watajitolea hamna faida yeyote kwa sababu tutasoma sana lakini bila uzalishaji hatufiki kokote, tutaendelea tu kushangilia misaada ya vyandarua vya (Bush) mbu toka USA.
  Matatizo yote haya ya kukosa waalimu na mengineyo, bila serikali ya CCM kubadilika na kujali uzalishaji ama kuacha ufisadi hatutafika popote. Tutajitolea sana lakini kama mafisadi na serikali yao ya CCM wanaendelea kufyonza basi haina maana yeyote. Dawa nyingine ni kuiondoa CCM madarakani, ili kuwazindua usingizini.
   
 16. M

  Magezi JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nadhani ni wazo zuri kuna mdau amesema tuwe na JF Foundation itakayo ratibu mipango ya wale wote watakao kuwa tayari kuanza kufundisha kwa kujitolea ktk shule ambazo ziko karibu na ofisi/biashara zao.

  Basi napendekeza tuanze kupata mawazo ya jinsi ya uanzishwaji wa JF Foundation na ningependa by January 2010 iwe tayari ili watakao kuwa tayari waanze kupiga chaki.

  Naomba JF Founder utusaidie jinsi ya kuunda JF Foundation ambayo haita athiri activities zingine za JF.
   
 17. I

  Ilongo JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 25, 2007
  Messages: 292
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Well kuna watakaofaidika, angalau, badala ya kuendelea kuteseka kwa kukosa elimu na upeo wa kuchanganua mambo itawasaidia hata kuelewa madhila unayoyazungumzia. Wengine hiyo misaada ya mbu wala hatuihitaji sababu ya hii elimu tuliyo nayo inatusaidia kujimudu katika hali mbalimbali ... na kumbuka kwamba hivyo vyandarua vyenyewe (na misaada mingine) unavyovizungumzia siyo vyote vinawafikia walengwa. Hata wakipata hawatadumu navyo maisha yao yote. So, kinachotakiwa ni elimu ambayo pamoja na hayo itamkomboa kiakili kuweza kujua jinsi ya kupata chandarua chake mwenyewe badala ya kuendelea uwa mtumwa wa misaada.

  Wakati mwingine najiuliza kwamba kama si hii elimu niliyoipata, labda sasa hivi ningekuwa kijijini nabanana na ndugu zangu kwenye mali ya urithi (kwa maana ndiyo utamaduni wetu huo, aidha unakatiwa kipande chako na kujenga mji wako mwenyewe au unasubiri mzazi afariki ndipo ugawiwe kilicho chako). Ndicho kipimo cha uelewa katika level hiyo. Lakini mtu anapoelimika zaidi kuna faida zaidi zitokanazo na elimu hiyo ikiwa ni pamoja na kuyatambua mazingira yanayomzunguka na kuweza kupambana nayo.

  Kelele zitapigwa saaaana kuhusu ufisadi, sijui siasa, lakini kama walengwa wanakosa uelewa katika mambo ya msingi watabaki kukushangaa maana kupitia ufisadi wengine wanapata angalau pilau na fulana once in 5 years!
   
 18. M

  Magezi JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Nafikiri hili wazo ni muhimu kama tulivyo kwisha sema hapoawali nadhani cha msingi sasa kila mmoja wetu ambaye yuko tayari ajiandae kwa kazi ikiwa ni pamoja na kushughulikia kibali cha kufundia hapo mwakani.

  Tujaribu tuone nadhani mambo yatakuwa mazuri tu, mimi niliwahi kufanya hivi miaka ya 1996 huko kagera sehemu fulani japo nilikuwa nawafundisha vijana wawili tu lakini nilifurahi kufanya hivyo.
   
 19. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kujitolea siwazo sahihi sana kwa hali ya sasa na maisha ya Kitanzania. Suala lamsingi ni kuomba wasomi walioko maofficini wenye nafasi waombe kazi za part time teaching. Namaanisha walipwe pia. Hi ni approach ambayo inatumiwa sana na vyuo mfano Tumaini University inatumia sana part time lecturers. Kwa maana nyingine tuextend huu mfumo kwa shule zetu za secondary na colleges.

  Hatahivyo kuwa na waalimu wakutumu bado ni suala mhimu ili kuboresha elimu nchini.
   
 20. M

  Mugo"The Great" JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2009
  Joined: Oct 7, 2007
  Messages: 263
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Wazo hili ni zuri sana. Kinachotakiwa ni coordination kama wenzangu walivyotangulia kutoa opinions zao. kama JF Foundation itaundwa then itatumika kuratibu Volunteers online na hii itawapatia muda wa kuapnga ratiba/likizo zao vizuri ili kuendana na mihula ya masomo huko Tanzania.
   
Loading...