SoC01 Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na vijana wawaze kujiajiri na sio kuajiriwa

Stories of Change - 2021 Competition

M37

New Member
Jul 17, 2021
2
4
WANAFUNZI WA VYUO VIKUU NA VIJANA TUWAZE KUJIAJIRI KULIKO KUAJIRIWA.
Habari za wakati huu Watanzania wenzangu.

Leo nimeamua kuja kuandika chapisho hili ili kuweza kuwafungua akili wanafunzi wengi wa vyuo vikuu pamoja na wahitimu wa vyuo ambao hawana ajira waliopo mtaani wanaosubiri ajira.
Wanafunzi wengi pamoja na Vijana huwa mitazamo yao wengi wanawaza kuajiriwa serikalini au katika mashirika au makampuni ya binafsi kitu ambacho kimepelekea vijana wengi kukosa uwezo wa kufikiria namna ya kujiajiri na kupelekea wengi wanaohitimu masomo yao kukaa nyumbani kusubiri ajira kwa muda mrefu badala ya kutafuta njia ya kujiajiri. Mfano mtu amemaliza chuo tangu mwaka 2017 au 2018 mpaka Leo yupo nyumbani anasubiri serekali ije impe ajira kwahiyo kwa wakati wote huo tangu amalize chuo anategemea wazazi, kitu ambacho si kizuri kwa kijana hususani wakiume.

BASI WANAVYUO PAMOJA NA VIJANA WAFANYE NINI ILI WAWEZE KUJIKWAMUA KATIKA UKOSEFU WA AJIRA?

1.KUBADILISHA FIKRA NA MITAZAMO
Kwa maana ya kwamba mwanafunzi anatakiwa tangu akiwa chuoni awake kujiari kwa 70% na kuajiriwa 30% , hii itamsaidia kuweza kuondokana na mawazo ya kutegemea ajira za serekalini. Pia wanachuo wengi hawapendi kuonekana wanafanya kazi za watu wa kawaida mfano kulima, upishi , umachimga n.k mtu anajiona yeye kwa elimu yaks aliyonayo kufanya kazi hizo ni kujidhalilisha kitu ambacho si kweli.

2. KUANGALIA FURSA ZINAZOPATIKA KATIKA MAZINGIRA ULIYOPO NA KUZIFANYIA KAZI .
Hapa ndipo wanachuo wengi wanapokosea , mtu anaona kuna fursa fulani lakini anashindwa kuzifanya kwa sababu anajiona yeye ni mtu wa hadhi ya juu ana degree hawezi kufanya baadhi ya kazi. Mfano unakuta mahali mtu anapoishi Kuna shida ya mboga za majani lakini ukimwambia kijana mhitimu wa chuo kwa nini usilime mboga za majani ukawauzia watu mtaani? Anakwambia mimi na degree yangu siwezi kwenda shamba na wakati huo yuko tu mtaaani hana jambo lolote analolifanya la kumuingizia kipato zaidi ya kuzurura.

3. KUANZA KUWEKA MIPANGO MAPEMA YA MAMBO AMBAYO UNGEPENDA UYAFANYE SIKU ZA MBELENI . mwanafunzi anatakiwa akiwa chuoni aanze kuweka malengo ya miradi ambayo anaweza akajiri kwayo baada ya kuhitimu masomo yake ya chuo kikuu pia anatakiwa ajue miradi hiyo itagharimu kiasi gani cha fedha ? Na je atazipata wapi fedha za kuendesha miradi hiyo. Hii itamsaidia kujua ni vitu gani anahitajika kutafuta ili akimaliza chuo asisumbuke.

JE NI MIRADI GANI AMBAYO MWANACHUO ANAWEZA AKAJIAJIRI NAYO INAYOHITAJI MTAJI MDOGO AU WA KAWAIDA?

KILIMO CHA MBOGAMBOGA.
Huu ni mojawapo ya miradi ya muda mfupi na inahitaji mtaji mdogo Sana kama ukipata eneo lenye uhakika wa maji kwa ajili ya kumwagilia. Mfano kilimo cha mboga za majani kama vile mchicha, spinach , Chinese, au Sukuma wiki ni mboga ambazo zinatumika na zinahitajika kila siku mijini na vijijini. Mboga hizi hutumia muda wa mwezi mmoja tu kuanza kuvuna . hivyo basi ndani ya muda mchache kabisa mtu unaanza kujiingizia kipato.

KILIMO CHA MATUNDA
Kana baadhi ya matunda hayahitaji uangalizi mkubwa lakini yana faida kubwa sana mfano zao la Papai linachukua muda mrefu shambani kuanzia miezi sita hadi nane ndipo unaanza kuchuma kwa mara ya kwanza lakini ukishaanza kuvuna unaweza kuendelea hadi miaka mitatu inategemea na matunzo yako ya shamba , ambapo unaweza ukajipatia mpaka kiasi cha Zaidi ya shilingi milioni kumi kwenye ekari moja tu.

Ama zao lingine la matunda lisilohitaji matunzo sana ni nanasi hili kwanza lina stahimili sana ukame na pia magonjwa yake sio mengi ukilinganisha na mazao kama vile tikiti maji. Zao hili hutumia muda wa mwaka mmoja hadi mwaka mmoja na nusu ili kukomaa ambapo kwa ekari moja mtu anaweza kujipatia mpaka shilingi milioni 6 .

Nimejaribu kuonyesha haya mazao mawili tu ili yawe mfano na tuone ni kwa jinsi gani vijana tunashindwa kuzitumia fursa kama hizi wakati mashamba tunayo ya kutosha hapa nchini.

MRADI WA UFUGAJI WA KUKU WA KIENYEJI AU CHOTARA
Ufugaji wa kuku siku hizi umekuwa fursa kubwa sana kutokana na uhitaji wake kuongezeka sana siku hadi siku kwa kuwa vyakula kama vile chips vimeongeza sana uhitaji wa mayai pamoja na nyama ya kuku na hivyo kufanya upatikanaji wa soko kuwa mwepesi. Mtu akiwa na mtaji wa kama laki nne anaweza akaanza kufuga kuku kama 50 hivi ambao wanakaribia kutaga hivyo baada ya muda mchache wataanza kutaga hivyo kumuingizia kupato kwa kuuza mayai. Pia anaweza akaanza kutamishia hawa kuku walau watano kila mwezi ili kuongeza idadi ya kuku wake na kuweza kuongeza ukubwa wa mradi. Uzuri mmoja ni kwamba kuku wakishaanza kutaga utauza mayai na kuweza kupta hela ya kuwanunulia chakula chao pamoja na dawa au chanjo mbalimbali ambazo zitakuwa zikihitajika. Na napendekeza zaidi kwa mfugaji kufuga kuku wa kienyeji au chotara maana wenyewe huwa ni wavumilivu kwa magonjwa na hali mbalimbali za mazingira.

Hizo hapo juu ni baadhi ya miradi mitatu ambayo mtu wa uchumi mdogo anaweza akaanzisha na akaweza kuimudu vizuri kabisa japo kuwa kuna mingine mingi ila kwa upande wangu nimeona nikuletee walau hiyo ya kilimo ambayo ni rahisi kufanyika katika maeneo mengi hapa nchini kwetu kwa kuwa tuna mashamba ya kutosha. Chamsingi ni kuwa na ukaribu na maafisa kilimo ili wakusaidie baadhi ya masuala ambayo huna ujuzi nayo ili kupunguza hasara zinazoweza kujitokeza.

PENDEKEZO. NI VIZURI MKULMA AKACHANGANYA UFUGAJI PAMOJA NA KILIMO CHA MAZAO YA BUSTANI ILI KUMSAIDIA KUPATA MBOLEA YA KAMA VILE YA KUKU ILI KUONGEZA RUTUBA SHAMBANI NA KUPUNGUZA UTUMIAJI WA MBOLEA ZA VIWANDANI.

KWANINI VIJANA WANASHINDWA KUJIAJIRI WAKATI KUNA FURSA KAMA HIZO TULIZO ZITAJA HAPO JUU?

1.Kutokujiamini , kitu ambacho kinapelekea mtu kutokuwekeza nguvu ya kutosha katika wazo au mradi wake na kupelekea mradi kufa mapema.
2. Ukosefu wa mtaji , hii imekuwa changamoto kubwa kwa vijana wengi wanaotaka kujiajiri, unakuta kijana ana wazo zuri lakini mtaji wa kuliendeleza hakuna.
3. Kukata tamaa, Vijana wengi tunapenda kuona matokeo na mafanikio ya haraka kitu kinachopelekea mtu akikutana na changamoto kidogo tu kukata tamaa na kuachana na mradi.
4. Kutokukuwa na tabia ya kujiwekea malengo , unakuta kijana anasoma au yupo mtaani lakini hana mawazo yoyote ya maendeleo yupo tu anasubiri kitakachojitokeza mbele yake ndicho anakifanya kitu ambacho kinampelekea kushindwa kuwa na ndoto za maisha na hivyo kuishi maisha duni.

SULUHISHO LA HIZO CHANGAMOTO HOPO JUU?
Kuwa ni nia madhubuti ya jambo ulilopanga kulifanya
Jifunze kuweka akiba kidogo kidogo tango ukiwa chuoni ili unapomaliza mtaji isiwe changamoto ya kukukwamisha wewe kujiajiri au ikishindikana muombe ndugu yakow a karibu ambaye ataweza kukusaidia .
Kutumia mitandao ya kijamii na internet kujifunza mambo mbalimbali kuhusiana na mradi wako au kazi yako ili kuongeza ufanisi.
Kuomba ushauri kwa wataalamu wanaohusiana na mradi wako ili kuweza kuepuka baadhi ya changamoto zinazoweza kujitokeza kama vile magonjwa n.k
Kujifunza kutoka kwa watu waliofanikiwa na kutafuta na kuzijua changamoto zinazopelekea watu wengine kushindwa ili wewe uweze kuziepuka.
Fanyia kazi ushauri unaopewa na pia usichukie unapokosolewa .

KWAHIYO, Kwa hayo machache naomba niishie hapo na mawazo haya ukiyafanyia kazi naamini yatakusaidia na kukupa mwongozo mzuri wa kuanzisha mradi wako wa kilimo au ufugaji wa kuku.
Mwisho kabisa nipende kukukumbusha kuwa anza kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu kwa kila jambo lako unalolifanya kwa hakika yeye ndiye muweza wa kila jambo lako.

SHUKRANI SANA ,
NATUMAI CHAPISHO LANGU HILI LITAWANUFAISHA WATU WENGI HUSUSANI WANAVYUO WENZANGU.
NAOMBA KURA YAKO KWA KAZI YANGU HII.
AHSANTE
 
KUNA JAMBO MUHIMU UMELISAHAU WAZAZI NA JAMII KWA UJUMLA NDIO WANAWEZA KUA MSAADA MKUBWA KWENYE HILO KWASABABU WAZAZI WENYEWE NDIOWANAKUA CHACHU YA KUMUAMINISHA MTOTO KWAMBA SOMA UJEKUA MTUFULANI NDIOMAANA MZAZI AKIWA NA MTOTO ANASOMA. UNAKUTA HAMSHIRIKISHI SAAAANA KAZI ZA NYUMBANI KAMA KUPIKA,KUFUNGA KUKU YAANI ANAMKAZANIA ASOME TUUUUU....

UTASIKIA UKITOKA SHULE JISOMEE HUKO BANDANI YUPOKIJANA TUNAMLIPA ACHA AFANYE KAZI....UNAMZEMBEESHA NDIO MWISHO WANAONGOZA KUA HATA MASHOGA...

JAMII....

SISI JAMII TUNATAKIWA TUWE WAKWELI TUSIWAFICHE KITU KUHUSU MTAA NA TUSIJITENGE NAO KISA WANASOMA AU WASOMI KIUHALISIA HAWA WANAOJIITA WASOMI WANAHITAJI MSAADA WETU SISI WATU WA MTAA BAHATI MBAYA WAO HAWAJUI KAMA SISINDIO TUNAWEZAKUA MSAADA WAO SIKU WAKIJUA HILO WATATHAMINI MTAA NA KUUTUMIA KUJUA KESHOYAO BAADA YA KUMALIZA MASOMO YAO...

Sent from my Infinix X650B using JamiiForums mobile app
 
  • Thanks
Reactions: M37

Much thanks
 
Back
Top Bottom