kinepi_nepi
JF-Expert Member
- Aug 16, 2007
- 869
- 235
Baada ya serikali ya CCM kufikiri kutowarudisha vyuoni wanafunzi wa vyuo vikuu inawakomoa wogombea wa vyama vya upinzani, imejikuta kwenye wakati mgumu baada ya kutawanya wapiga debe wa mageuzi Tanzania nzima bila kujijua.
Ilikuwa ni vigumu sana kumfikia kila mtu kule kijijini, ila baada ya serikali kuwanyima haki ya msingi wanafunzi hawa moja na muhimu ni ya masomo yao, na ya pili ni ile ya kura. Wanafunzi walio zaidi ya 60000 waliotawanyika Tanzania nzima hasa vijijini wanatoa elimu ya urai na kuonyesha ubaya wa serikali ya CCM na kuhamasisha base zote za wapenda demokrasia na mageuzi ya kiutawala.
Vyama vya upinzani sasa vinatakiwa kuwatumia wanafunzi hawa Kulinda na kusimamia kura, Kuwa Mawakala wa vyama vya upinzani. Kwa hali ilivyo sasa wanafunzi wengi wanaweza kuwa waaminifu, wakiwa ni taifa la sasa la wasomi wanaelewa wazi elfu 20 ya rushwa ili kusaini uongo haiwezi kumpa ajira wala kumsomesha.
Wanafunzi mlio mitaana tumieni elimu yenu kwa faida yenu na kizazi chetu kijacho. Kumbuka mizwengwe ya vyuo imeanza tokea enzi za kale, matokeo yake ni kuzalisha vilaza, wanaoshindwa kupambana na dunia ya sasa.
Shule zikifunguliwa utasikia CRUSH Program ili tuweze kumaliza kwa sababu ya muda. Kazini hakuna Crush Program, kampuni za uzalishaji za ukweli zinataka matokeo swala la kwamba mtaala haukufuatwa kwa sababu ya serikali hakuna atakayesikia wala kujua. Tulinde vizazi vyetu vijavyo viepuke hii adha.