Wanafunzi wa Vyuo Vikuu binafsi 2020 tusimpigie kura kiongozi anayedharau vyuo vyetu

Kwani nani asiyejua kuwa 2015 mlimpigia Lowas endeleeni tu hata 2020 na hata 2025 lakini Mh.JPM ndo mpango mzima hadi 2025
 
Salary Slip usomi wako una walakini uwezo wako wa kufikiri na kutoa maamuzi sahihi ni mdogo na popote utakapoajiriwa utakuwa ni hasara kutokana na wewe kuonesha huwezi wa kupambanua na kutoa maamuzi sahihi
 
Kuja kufikia 2020, mtakuwa mmesahau hata mtamzira kwa lipi!

Mnalia lia sana bwana kila kitu lazima kususa au kuandika hapa.JF!
 
Kama ukifikilia kwa mlengo wako huo upo sahihi, Ila Mr President ana nia njema kabisa, kwan chuo imekuwa secondary? Tuanze kupangiana pakusoma?, lakn kama haitosh n kweli fika kabisa kuna vuo vingne bado havina sifa ya kuitwa vyuo vikuu, unakuta chuo hata mwl mwenye Phd hakna hata mmoja zaid n masters tu, lakn vilijikuta vinapata wanafunzi wa ktosha na kupewa ruzuku kama vyuo vingne,
 
Awe Rais asiwe rais Tz tushapotea kisiasa yani tunazid kupiga hatua za kurudi nyuma kila siku saivi ni bora liende kwasabu ndio tulioyachagua haya maisha....hatutaki kushirikiana ktk maendeleo tunamalia majungu na upuuz
 
Hivi kunukuu mtu vizuri huku Tanzania imekuwa shida nilitegemea mfurahie alichozungumza Rais kumbe kimewauma alichosema rais ni hivi TCU ina tabia ya kupeleka wanafunzi kwenye vyuo ambavyo hawachagua kwa kuwa ni private badala yake ametaka waangalie chaguzi za wanafunzi wawapeleke kwanza walikochagua pakijaa ndio waende huko, nyie mmekimbilia kuona ni havina sifa kumbe ada yake ni kubwa... tuwe na fadhila kwa kweli tusitafute mabaya tu
 
Akutakane hakuchugalii tusi.Hili leo limedhihirika wazi hivyo ni wazi wanafunzi mlioko vyuo vikuu binafsi na hata mliosoma katika vyuo hivi siku za nyuma mjue wote mmedharauliwa.

Baba anabagua watoto badala ya kuwa mlezi wa wote!!

Kwa mantiki hii 2020 tuungane kumkataa mtu huyu.

Pole sana Mzee wa Msoga ulijitahidi kukuza sekta binafsi ila mwenzako yuko busy kuingamiza.

Hivi wasomi wa hicho chuo anachokisifia wameifikisha wapi nchii yeye akiwemo?

Sio kila mtu anafaa kuwa kiongozi.
Na huyo Bashite wake naye si kasomea huko huko anakoponda...
 
Kweli tunaishi juzi wakati wenzetu wanaitafuta keshokutwa!
Sawa, hatuwezi kuwafanya role model wetu kuwa Harvard au Oxford lakini basi walau tujilinganishe na Makerere, kuamini kuwa UDSM ndio kilele cha elimu tunakuwa tumelenga low sana. Kuna mtu aliwahi kuniambia kuwa Chuo cha Kairuki kinatoa madaktari wazuri sana kwa Tanzania.
Pamoja na hayo nilidhani bashite naye angelikuwa katokea UDSM lakini hata hicho alicho nacho ni utata mtupu!
 
Kauli ya Rais ichukuliwe kama motivation kwa vyuo vingine kuongeza ubora ili vifikie mafanikio ya UD ,na wala sio kulalamika,kama wanafunzi watapewa nafasi ya kujichagulia vyuo ni ukweli usiopingika kuna vyuo vitakosa wanafunzi ,lakini ili vipate wanafunzi vita anza kufanya maboresho na hatimaye wanafunzi na wazazi watavielewa na kuanza kuvichagua na kuleta ushindani,hii ni fursa kwa wenye vyuo kuonesha weledi wao na kuendelea kuleta wanafunzi bora.Elimu si swala la kisiasa kwa hiyo lisiingizwe kisiasa.Tuboreshe mazingira ya kusomea na wenye vyuo wawe na uchungu na wanachokifanya sio kuchukua pesa za wanafunzi na kuwaacha bila kujali elimu wanayoipata inakidhi mahitaji au la.
 
Hakili zako unazijua mwenyewe, ila contribution ya private sector hasa taasisi za dini ni za kutolewa mfano more than 70% ya vyuo vikuu tz ni private, Na vimechangia kuondoa gap nililoachwa Na serikali toka 2005, vimesajiliwa Na mamlaka ya umma. Nenda kama Saut mz see the content. Liganisha Na hao Wa Udsm kwenye same entry. Hakuna logic, yes Udsm is best but never deny mchango Wa vyuo vingine, nenda field, you learn something.
Hakili=Akili
 
Akutakane hakuchugalii tusi.Hili leo limedhihirika wazi hivyo ni wazi wanafunzi mlioko vyuo vikuu binafsi na hata mliosoma katika vyuo hivi siku za nyuma mjue wote mmedharauliwa.

Baba anabagua watoto badala ya kuwa mlezi wa wote!!

Kwa mantiki hii 2020 tuungane kumkataa mtu huyu.

Pole sana Mzee wa Msoga ulijitahidi kukuza sekta binafsi ila mwenzako yuko busy kuingamiza.

Hivi wasomi wa hicho chuo anachokisifia wameifikisha wapi nchii yeye akiwemo?

Sio kila mtu anafaa kuwa kiongozi.
Mmeanza kampeni uchwara. Hatudanganyiki. Sisi Magufuli mbele kwa mbele.
 
20 Reactions
Reply
Back
Top Bottom