Wanafunzi wa Vyuo/Sekondari waruhusiwe kufanya kazi kuchangia elimu yao? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wa Vyuo/Sekondari waruhusiwe kufanya kazi kuchangia elimu yao?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Jun 9, 2011.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kuna kundi kubwa la watu ambao wanasubiri serikali iwapatie fedha za masomo n.k na wazazi wao wakati wana uwezo wa kufanya kazi. Kwa muda mrefu mfumo ulioundwa na serikali ya CCM unazuia na kufanya iwe ngumu sana kwa wanafunzi kufanya kazi. Matokeo yake, walinzi kwenye vyuo wanaajiriwa nje, wasafisha madarasa na vyoo ni watu wa nje, wakata majani ni watu wa nje wakati kuna nguvu kazi ambayo ipo tu.

  Tumetengeneza mfumo wa kundi tegemezi ambalo linachukua tu kutoka kwenye jamii lakini halirudishi. Wengi wa hawa wanapata nafasi ya kufanya kazi kidogo kama sehemu ya kutimizwa matakwa ya elimu yao (research, internships n.k). Je, umefika wakati wa kutengeneza mfumo wa wanafunzi kuchangia elimu kwa kuwapatia nafasi za kazi humo humo mashuleni na kuweka kiwango cha chini cha mishahara ya wanafunzi (iwe tofauti na kima cha chini cha mtu wa kawaida).

  Kwa mfano, badala ya kuwapatia posho bila kufanyia kazi kwanini posho za wanafunzi nchini zisiingizwe kama sehemu ya mapato yao wanayofanyia kazi?

  je wanafunzi watakuwa tayari kusafisha vyoo, kufagia, kukata majani, kulisha wanyama, kufanya kazi za uwaiter/bartender n.k ili wajipatie kipato cha matumizi?

  Je, tunaweza kuweka utaratibu hata wanafunzi wa sekondari nao waruhusiwe kufanya kazi na kujipatia kipato badala ya kutegemea fedha za posho toka kwa familia, wadau na wapambe?
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Mkuu Mwanakijiji naunga hoja yako hapo juu tena kwa nguvu zote. System ya kuruhusiwa wafanye kazi itaondoa idadi ya mategemezi nchini pia itainua kipato kwa wanafunzi/itapunguza ukali wa maisha kwa wanafunzi hawa. Hapa Tanzania ni Chuo kimoja tu ndio kifuatacho hiyo system. St.John's kimewaajiri wanafunzi wake ktk idara zake kutoa usaidizi, mfano 85% ya wafanyakazi wa maktaba ya St.John's University ni wanafunzi wafanyao kazi under part-time bases! Hii system tukiifata itakuwa poa sana!
   
 3. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #3
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  Inafikirisha ,
  inawezekana wakafanya kazi japo itachukua muda vijana kuelewa mantiki ya swala kama hilo hasa ktk kizazi kinachovuka toka ktk fikra za kua ni wajibu wa serikali kubeba mzigo wa elimu. . .
   
 4. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #4
  Jun 9, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Mkuu mwanakijiji hoja yako ni nzuri ila ni impractical kwa Tanzania. Zamani miaka ya 80 kurudi nyuma wanafunzi wengi wa chuo kikuu, nikiongelea chuo kikuu kwa wakati huo unanielewa (yaani UDSM) walikuwa wana muda wa kufanya kazi za ziada na baadhi yao walikuwa wanafanya kazi. Kilichokuja kuharibu ni baada ya migomo na watawala kutukanwa. Ikaonekana kuwa wanafunzi wa chuo kikuu wana muda mwingi wa ziada ndiyo unaowafanya kufanya mambo ya kipuuzi kama migomo, n.k. Mkakati ukawa dawa ni kuwa keep busy na shule, wataalam wa mitaala wakaanzisha kitu kinachomuweza busy mwanafunzi kuanzia saa moja asubuhi mpaka saa mbili usiku. Anachofikiria ni chakula na darasani tu kama yupo serious na elimu.

  wakaanzisha mfumo wa semester kutoka term system, wakaongeza idadi ya kozi, unakuta mtu ana kozi mpaka nane kwa semester na zote hizo anatakiwa kuhudhuria, lecture, seminar/tutorials, katika course assessment anakuwa na homework plus tests. Hii inamfanya mwanafunzi 24hrs a day kufikiria jinsi ya kupangua issue moja ya elimu baada ya ingine, je saa ngapi atapata muda wa kufanya part time job?.

  Kingine ni suala la uchumi, kutokana na hali kuwa ngumu waajiri hawaajiri tena, maana kama kuna mtu kamaliza masomo miaka miwili iliyopita na bado hajapata kazi unatarajia aliyeko shuleni atafanikiwa?. Nakumbuka mimi enzi zetu unakuta mtu bado hajamaliza hata mitihani tayari ana offer tatu au nne za kazi mpaka anachanganyikiwa lakini si sikuhizi, tena kibaya zaidi waajiri wameanzisha mchezo wa kuangalia GPA (Grand Points Average) ili mtu awe shortlisted for an interviews, the higher the GPA the higher the chance of being called for the interviews, sasa mtu akiangalia kufocus katika part time kutampunguzia uwezo wa kutengeneza GPA kubwa.

  Kwa ujumla tu katika mazingira ya mfumo wa elimu ya Tanzania wa leo hii, hii mada yako wengi wataiona ni kituko japo there is very important suggestions in it.
   
 5. jamii01

  jamii01 JF-Expert Member

  #5
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 1,836
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  INAWEZEKANA ILA VIJANA WABADIRI MTAZAMO WAO NA FIKIRA ZAO..waache maisha ya omba omba na mizinga..
   
 6. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #6
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  mkuu imefikia hatua tusiwe watu wakukata tamaa kwa kila kitu.
  haya mambo yanazungumzika na yanaweza kupangwa yakafanyika, ni system tu tunaibadilisha kukidhi maitaji yetu, hata serikali ya magamba wanaweza ili sio issue ya kushindikana kabisa
   
 7. VIKWAZO

  VIKWAZO JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2011
  Joined: Apr 9, 2011
  Messages: 1,910
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  i hope huna maana wasipewe msaada na familia zao na serikali ?
  sidhani kama mzee mwanakijiji ana maana wawe full time employed in ajira ya kupata uzoefu wa maisha/kazi na
  hela ya pipi/mkate maana hata nchi zinazofanya hivyo bado wanafunzi ni tegemezi kwa kiasi furani ila sio 100%
  kama tanzania, lakini pia inaleta ukuaji bora yaani kujenga hali ya kuwajibika toka utotoni
   
 8. MPIGA ZEZE

  MPIGA ZEZE JF-Expert Member

  #8
  Jun 9, 2011
  Joined: May 16, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 515
  Trophy Points: 280
  Sio tu katika miaka ya 70 na 80 vijana walikuwa wanafanya kazi za ajira, bali pia walikuwa wanajitolea hadi vijijini wanachimba barabara, wanajenga zahanati, wanasafisha vyanzo vya maji ya kula, nk. Kadri ubadhirifu wa mali ya umma na ufisadi vilivyozidi, ndivyo na moyo wa wananchi kujitolea ulizidi kudhoofika, na ndivyo fikira za kwamba 'serikali ina pesa ndio inapaswa kufanya kila kitu' zilivyozidi kutawala. Utamaduni wo wote ule (uwe chanya au hasi) unaochipua na wakati mwingine kukomaa katika jamii ni muhimu uangaliwe katika muktadha mpana zaidi.
  Nyongeza tu ya hoja nyepesi: tukisema wanafunzi wa vyuo vikuu wafanye kazi kama hizo na hata kuwa mabaa meidi - huo umati wa wanaomaliza darasa la saba si wote watakuwa vibaka na ma-cd. Hilo utalielezaje?:confused2:
   
 9. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #9
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Kazi zitatoka wapi iwapo wahitimu wa drs 12, 14, na vyuo hawana kazi.
   
 10. Tausi Mzalendo

  Tausi Mzalendo JF-Expert Member

  #10
  Jun 9, 2011
  Joined: May 23, 2010
  Messages: 1,471
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  umesema vema kabisa.Nikiangalia aina ya kazi alizotaja MMKJJ - sijui kama vijana wa siku hizi watataka kujihusisha nazo.Bado kuna fikra hasi kuhusu kazi kama hizo.Watanzania kwa ujumla au waafrika tuseme, wanachagua kazi na kuona kazi kama hizo ni za wasio na elimu yoyote! Inabidi kuanzia mahali hata hivyo. Wanafunzi toka shule za msingi wajengewe fikra za kuthamini kazi yoyote inayompa mtu kipato bila kujali elimu.Utegemezi utapungua kama kila mtu ataona fursa kwenye kazi yoyote,Huenda isiishie kwenye vyuo tu.Kuna kazi za usafi maeneo mengi ya miji yetu.Huenda wasomi wakaweza kuleta fikra mpya katika utendaji na ufanisi wa kazi zile zisizoonekana kuhitaji elimu ambazo ufanywaji wake umekuwa wa kulipua lipua mno.

  Na kwa wasichana ambao siku za karibuni wamejivunia sifa ya kupenda vya mteremko kwa kujishushia heshima na kujitweza kwa wanaume pengine kazi hizi zitawarejeshea heshima.Ukitizama wasichana wengi wa vyuoni, inasikitisha aina ya maisha wanayoishi.Wapo wanaoishi maisha ya uchangudoa ati wajipatie vipato vya kukogana na kushindana kwa mavazi, mapambo na hata magari! AIBU JAMANI WANAWAKE WENZETU!
   
 11. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #11
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 864
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana nawe kwenye hoja ya pili lakini hii ya Kwanza siyo kweli.
   
 12. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #12
  Jun 9, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa; nilikuwa nafikiria hicho vile vile; kwamba yaweza ikawapa uhuru mabinti zetu kuweza kuishi maisha ambayo yanaendana na utu wao. Nimependa hili.
   
 13. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #13
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkjj hii hoja ni nzito na inahitaji ifanyiwe kazi maana si tu kuondoa utegemezi bali hata zile fikra za wakati wa uhuru zilizodumu mpaka leo kwamba msomi lazima afanye kazi ofisini. Inachekesha pale unakuta jitu zima linamtukana baa medi kisa kwa kujiona limeshushiwa hadhi wakati linakaa mjin i kwa dada yake bila kazi yeyote ile. Kuna mijitu pale TZ iko kwenye NGO's ina vitambi vikubwa vikubwa na kutembelea magari makubwa makubwa lakini haijui kwamba hela hiyo wanayotanulia imechangwa na wakata majani, bartenders, waosha vyoo na wengi wao wakiwa wanafunzi tena wengine in high schools.

  To me hii scheme kama ilivyopendekezwa ndiyo huko zipitishiwe hata hela za the so called mikopo. Well we can argue about time, lakini inawezekanaje nchi zilizoendelea watu wanasoma, wanafanya kazi, wanacheza michezo na bado wanaenda vacations?
   
 14. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #14
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  This is a bit off-topic, Watu wako SUA pale hawajawahi kushika jembe wala kuji-involve na maswala yeyote ya kilimo na hawatawahi kushika jembe wla ku-operate jembe. Sasa kwa nini mlipakodi amlipie mtu kama huyu kusomea kilimo?
   
 15. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #15
  Jun 9, 2011
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  C;moon eti nilikuwa najiuliza tumefikaje hapa, nagundua kumbe hatujawahi hata kuwepo huko kwenye other side of the wall.
   
 16. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #16
  Jun 9, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,949
  Likes Received: 1,274
  Trophy Points: 280
  You are so intelligent with your topics
   
 17. Kinyasi

  Kinyasi Member

  #17
  Jun 9, 2011
  Joined: Nov 22, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 15
  Mkuu Kichuguu,
  Kwa mujibu wa maelezo ya Mzee mwanakijiji na uzoefu wangu huku ughaibuni ni kwamba kazi zinapatikana ndani ya chuo kwa kugawana ama kuwapunguza kama si kuwa-lay off kabisa hao watu wasio wanafunzi walioajiriwa ndani ya vyuo kufanya kazi zilizo ndani ya uwezo wa wanafunzi kama vile uhudumu wa vyakula na vinywaji kwenye migahawa, lab assistants, tutorial assistants, utunzaji bustani na majengo, uhudumu maktaba na maduka ya vitabu chuoni n.k Mkjj kapendekeza na hao Sekondari Darasa la 12 na 14 wafikiriwe pia japo ni suala gumu sana hasa ukizingatia uchache income resources zilizopo na ufinyu wa muda (saa 11 alfjr mchaka mchaka; saa 12 asbh kujiandaa; saa moja Brekafast-Uji/Chai; saa 1asbh parade; saa 1:40asbh darasani; saa 5:20asb break; saa 6 mchn darasani kumalizia ngwe ya siku hadi saa 8:20mchn; saa 8:30 mch Lunch; Saa 10 jion Usafi wa mazingira hadi saa 11:30; Saa 12 jion dinner; saa 2 uck Prepo (kujisomea, homework wengine wanatongozana kwenye viunga vya dark corners-omba usishikwe na kiranja wa ulinzi n.k) na saa 4 na kuendelea watu wanarudi vitandani(speaking to my experience kule Govt boarding school pande za kaskazinI TZ)
  Kwa wanafunzi wa chuo wengi wao hawana ratiba ngumu kama za hao drs la 12 na 14. Unakuta Mwanafunzi anaanza na kozi ya kwanza saa 2 asbh kozi ya pili saa 10 jion au anaweza akawa na kozi moja au hasiwe na kzoi kwenye siku fulani. Kwa mfano J'3, J'5 na Ijumaa yupo darasan J'4, J'5 na wikiendi akawa anazurura Kahumba Night club- watu wa SUA, Jolly Club, Bills, Maisha club ama Mlimani City -IFM/UDSM, au Mnadani na kushangaa jengo la Bunge-UDOM badla ya kulitumia hilo gap angalau kujishhugulisha na vibarua vitakavyomuingizia kipato ambacho kiasi fulani kinapunguza utegemezi wa familia au hata kuwalipia ada wadogo zao walio sekondati.
   
 18. K

  Kakalende JF-Expert Member

  #18
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 1, 2006
  Messages: 3,259
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 135
  Hii inawezekana kabisa lakini kazi zenyewe ziko wapi?
  Halafu hawa vjana wetu 'MASHAROBARO' kazi nyingine hawapendi kuzifanya. Laiti kama wangepitia JKT labda hili wazo lingewezekana.
   
 19. C

  Campana JF-Expert Member

  #19
  Jun 9, 2011
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 207
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Wanavyuo wanaweza pia kusambazwa shule za kata ili wafundishe kwa mshara, kwa ile mikoa ambayo vyuo hivi vipo. Wanafunzi wa sekondari wanasema kuwa wanafunzi waalimu hujituma zaidi (wakiwa field) kuliko walimu waajiriwa. Ni wazo zuri sana hili
   
 20. T

  Taifa_Kwanza JF-Expert Member

  #20
  Jun 9, 2011
  Joined: Sep 3, 2010
  Messages: 443
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nakubalina na wewe MM
  Ila kama alivyodokeza mmoja wetu hapo juu, mitaala ni lazima irekebishwe
  ili kuwezesha mazingira ya hii kitu.
  Niongezee vitu viwili
  1. Mitaala ibadilishwe such that, mtu anaweza akasitisha masomo
  kwa muda baada ya term au semester kama amekamata kazi
  inayomlipa.

  2. Kwenye hili la ajira za wanafunzi wa secondary, isiishie hapo tu
  watoto kuanzia miaka hata kumi na tano waruhusiwe kufanya kazi
  hii itawapatia on the job training and expertise, mfano halisi tunao
  kwamba mafundi magari wengi hapa nchini ni watu ambao wameanza
  kama maspaner boys lakini wanapata shule ya uhakika na kuwatoa kimaisha.

  hii ni muhimu sababu, badala ya nchi kuzalisha watoto wa mitaani ambao
  baadae watabadilika na kuwa vibaka wazoefu tutakuwa tunajenga jamii
  ya wafanyakazi endelevu. Ila wasiruhusiwe kiholela tu kama ilivyo sasa
  bali kuwe na policy ya kitaifa ama kimkoa itakayoweka muda wa mtoto
  kufanya kazi, idadi ya watoto wanaoruhusiwa kufanya kazi kisheria,
  na kila muwekezeji alazimishwe kisheria kuwa na serious training
  program kwa watoto hawa n.k
   
Loading...