Wanafunzi wa vyuo kutopiga kura ni ukiukwaji wa katiba ya jamhuri ya muungano wa tz | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wanafunzi wa vyuo kutopiga kura ni ukiukwaji wa katiba ya jamhuri ya muungano wa tz

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by marshal, Nov 6, 2010.

 1. marshal

  marshal JF-Expert Member

  #1
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 350
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  NILISIKITISWA SANA NA KITENDO CHA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI KUTOWARUHUSU WANAVYUO WALIOKUWA WAMEJIANDIKISHA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KUPIGA KURA SEHEM NYINGINE KAMA HAKI YAO YA MSINGI NA KIKATIBA.
  KATIBA YA JAMHURU YA MUUNGANO INASEMA YAFUATAYO JUU YA HAKI YA KUPIGA KURA.
  "
  5​
  .-(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa miaka
  kumi na minane anayo haki ya kupiga kura katika uchaguzi
  unaofaywa Tanzania na wananchi. Na haki hii itatumiwa kwa
  kufuata masharti ya ibara ndogo ya (2) pamoja na masharti
  mengineyo ya Katiba hii na ya Sheria inayotumika nchini
  Tanzania kuhusu mambo ya uchaguzi.
  (2) Bunge laweza kutunga sheria na kuweka masharti
  yanayoweza kuzuia raia asitumie haki ya kupiga kura kutokana
  na yoyote kati ya sababu zifuatazo, yaani raia huyo-
  (a) kuwa na uraia wa nchi nyingine;
  (b) kuwa na ugonjwa wa akili;
  (c) kutiwa hatiani kwa makosa fulani ya jinai;
  (d) kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoa
  kitambulisho cha umri, uraia au uandikishwaji kama
  mpiga kura,
  mbali na sababu hizo hakuna sababu nyingine yoyote
  inayoweza kumzuia raia asitumie haki ya kupiga kura.
  (3) Bunge litatunga Sheria ya Uchaguzi na kuweka
  masharti kuhusu mambo yafuatayo-
  (a) kuanzisha Daftari la Kudumu la Wapiga kura na
  kuweka utaratibu wa kurekebisha yaliyomo katika
  Daftari hilo;
  (b) kutaja sehemu na nyakati za kuandikisha wapiga
  kura na kupiga kura;
  (c) utaratibu wa kumwezesha mpiga kura
  aliyejiandikisha sehemu moja kupiga kura sehemu
  nyingine na kutaja masharti ya utekelezaji wa

  utaratibu huo"
  KATIKA YOTE YALIYOTAJWA NA KATIBA YA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA IBARA YA 5 KIPENGELE CHA 3 (C) KINALITAKA BUNGE KUWEKA UTARATIBU WA WATU KUWEZA KUPIGA KURA SEHEMU TOFAUTI NA ZILE WALIZOJIANDIKISHIA.
  JAMANI EMBU WATAALAM WA SHERIA MNISAIDIE KWA HILI
   
 2. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #2
  Nov 6, 2010
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Ha ha haaaaaaa kaka sheria ya uchaguzi inasema upige kura ulipi jiandikishia na si penginepo. Badilisheni sheria kwanza msiilaumu tume mkuu.
   
 3. Tundapori

  Tundapori JF-Expert Member

  #3
  Nov 7, 2010
  Joined: Aug 12, 2007
  Messages: 521
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Mkanganyiko wa sheria za kibongo!!!!!!!!!!!!!!!!!
  Naamini katiba ya nchi ni ya muda mrefu sana na hizi sheria mpya za uchaguzi ni za jana tu na hazitelerezeki !!!!!! kwa sababu zinavunjwa kiurahisis sana tu.

  Ilikuwa inatakiwa sheria ya uchaguzi ilipoandikwa wange angalia je katika kipengele cha uchaguzi katiba inasema nini ndiyo waweze kubadilisha ipasavyo. Vinginevyo inakuwa kukinzana kwa sheria mambo yanaendeshwa kama mboga ya mlendalenda.
   
 4. Utotole

  Utotole JF-Expert Member

  #4
  Nov 7, 2010
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 6,344
  Likes Received: 3,178
  Trophy Points: 280
  Katiba imepitwa na wakati na serikali ya CCM haitaki kuruhusu mabadiliko kwa kuwa utata uliomo unaifaidisha CCM.

  Ikibidi tudai mabadiliko kwa kila namna
   
Loading...