Konseli Mkuu Andrew
JF-Expert Member
- May 10, 2013
- 740
- 855
Mimi pia ni mnufaika wa mkopo wa Elimu ya juu unaotolewa na serikali.Nimeona kumekuwa na minong'ono mingi na kuna kipande cha video kikitembea kikionesha baadhi ya wanafunzi wakiandamana kuhusu kukatwa pesa ya kujikimu kutoka Laki tano na ushirini 520000/= mpaka laki tatu na tisini na moja 391000/=.
Kinachonishangaza minong'ono imekuwa mingi tena ya chini chini kuliko vitendo.Tujikumbushe mkataba tuliosaini na bodi ya mikopo Kuna kipengele kinasema 'Utalipwa kutokana na idadi ya siku utakazo kaa chuo" ambapo mwanafunzi wa chuo kikuu kwa siku anapata 8500/=.
Sasa jiulize hii semester unakaa siku ngap mpaka kuelekea kwenye UE? alafu piga mahesabu ukiona hiyo laki tatu inaendana na siku utakazo kuwa chuo basi kaa chini tulia na ukiona haindani basi tafuta mamlaka husika na wakufafanulie Ila ukijifanya mzee wa maandamano utapoteza chuo na Kama unavyojua wengi tunatoka familia duni Sana hivyo kufukuzwa chuo kutaenda kuwaumiza wazazi wetu.