Wanafunzi wa UDSM na kamba za vitambulisho kila sehemu

Deadbody

JF-Expert Member
May 30, 2015
4,276
6,585
Jamani wanafunzi wa UDSM hivi zile ID holders zinavaliwa kila sehemu uendako? Maana nakutana na wanafunzi hawa wanavaa hizi kila sehemu iwe Kawe, Mwenge, Kariakoo, Mlimani City hata Kigamboni na Posta.

Kuna haja gani ya kuvaa hivi vitambulisho vyenu kila sehemu? Au ni ushamba tu na kutaka kujionyesha kwamba mnasoma UDSM?
 
Wivu na chuki, wewe kama mfanyakazi na una gari lako unavaa id muda wote bila aibu tatizo nyie mnaosikia Gari kwa jirani ndio mnalalamika, wanavaa kwa kuwa wanapenda chuo chao Udsm na wameridhika na chuo chao, Sasa mtu avae id ya Tumaini wakati yeye mwenyewe hakipendi tumaini ila low marks zilimpeleka hawezi vaa id,
 
Unaweza ukadhani wanapenda, lakini kutundika kitambulisho chuoni wakati wote ni lazima. La sivyo unakamatwa na Auxiliary Police. Sasa kama umeshajizoesha kuvaa shingoni maana yake ukumbuke kukivua ukifika getini. Kwa maneno mengine, ukitoka tu getini akili yako iji-tune kuwaza kutoa kitambulisho shingoni. Not practical!
 
Hehee
Kuna kipindi nilipita maeneo mkoa pendwa aisee wale watu walobobea kwenye sayansi wamevaa makoti meupe mtaani mgongoni ana begi ka mpanda mlima wapo tuu mtaani utadhani askari kanzu
 
Kinachofanya wavae zile ID kwanza ni Uzuri wa chuo, Sifa nzuri za chuo, Ufaulu mzuri wa chuo, Chuo namba moja kwa ubora Tanzania...hata mimi enzi zangu kungekuwa na ID holder na kamba yake imeandikwa kabisa UDSM STUDENT ningevaa popote pale. UDSM raha bana waache wavae tu kwa kweli hata kama ni ushamba.
 
Back
Top Bottom